51Թ

UNCTAD: Uwekezaji wa Kigeni katika bara Afrika watarajiwa kushuka mno

Get monthly
e-newsletter

UNCTAD: Uwekezaji wa Kigeni katika bara Afrika watarajiwa kushuka mno

Africa Renewal
3 August 2020
Kality Dry Port, Addis Ababa, Ethiopia
UNCTAD
Chanzo: UNCTAD, Repoti ya Uwekezaji wa Dunia 2020.

Hali inayoendelea ya kupungua kwa uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI) katika bara Afrika inatarajiwa kuwa mbaya zaidi mwaka 2020 kutokana na athari hasi za janga la COVID-19 linalosababisha kushuka kwa bei ya bidhaa, haswa mafuta.

Uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni katika bara hili unatarajiwa kudidimia kati ya 25% na 40% kwa msingi wa makadirio ya ukuaji wa mapato ya kitaifa (GDP) pamoja na vipengele mahususi vya uwekezaji, kwa mujibu wa Ripoti ya Uwekezaji wa Dunia 2020 ya Tawi la Bishara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNCTAD).

“Japo sekta zote zinatarajiwa kuathirika, sekta kadhaa za huduma zikiwemo usafiri wa ndege, hoteli, utalii na burudani zimeathirika zaidi na hii ni hali inayotarajiwa kuendelea kwa kipindi kirefu katika siku za usoni,” alisema James Zhan, Mkurugenzi wa uwekezaji na biashara wa UNCTAD.

Viwanda vya uzalishaji vyenye uwezo mkuu katika mikondo ya kuongeza thamani kimataifa, vimeathirika sana, ishara ya kutia hofu katika juhudi za kusaidia kupanua biashara na ukuaji wa viwanda katika Afrika. Kwa jumla, kupungua huku kwa kukua kunaokekana katika robo ya kwanza ya mwaka wa 2020 katika miradi iliyotangazwa ya mashirika yanayowekeza katika bidhaa mpya barani Afrika, japo thamani ya miradi (-58%) imepungua sana kuliko idadi yake (-23%) (mchoro 1).

Vivyo hivyo, kufikia Aprili 2020, miradi ya mashirika kuungana au kununuliwa baina ya mataifa (M&A) ya Afrika ilikuwa imepungua kwa kiwango cha 72% kutoka wastani wa kila mwezi mnamo 2019 (mchoro 2).

Matumaini ya kujenga upya

Lakini, vipengele viwili mahususi vinatoa matumaini ya kurejesha uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni katika kipindi cha wastani na cha muda mrefu. Kwanza ni thamani ya juu inayowekwa katika bara hili na chumi kuu ulimwenguni, hivyo kusaidia uwekezaji katika miundomsingi, raslimali, na maendeleo ya viwanda.

Uwekezaji kutoka kwa mataifa haya, mataifa yenye viwango vinavyotoafautiana vya usaidizi wa kisiasa, licha ya kuathiriwa na muungano wa COVID-19 na bei za chini za bidhaa, kwa kiasi fulani waweza kuwa nyumbufu zaidi.

Pili ni kuimarisha miungano ya kikanda kwa sababu ya kuanzishwa kwa biashara chini ya Soko Huru la Bara Afrika (AfCFTA) baad ya miaka mingi ya mazungumzo na kutamatishwa kwa mwafaka wake wa uwekezaji unaotarajiwa.

Katika kipindi kifupi kijacho, itakuwa muhimu kudhibiti kudidimia kwa uwekezaji na kupunguza gharama ya kiuchumi na ya kibinadamu ya janga hili.

Katika kipindi kirefu kijacho, kupanua sekta za uwekezaji barani Afrika na kuitumia kwa mageuzi ya kimuundo kutakuwa shabaha muhimu. Haya malengo mawili yatahitaji uwajibikaji wa busara, kwa wakati ufaao na ulioshirikishwa kwa mataifa ya bara hili.

Uwekezaji wa Kigeni wa moja kwa moja ulikuwa umeanza kupungua hata kabla ya janga

Hatari ya COVID-19 imewasili wakati Uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja (FDI) ulikuwa unadidimia, huku bara hili likiwa limepata upungufu wa 10% mwaka wa 2019 kufikia $ bilioni 45.

Athari hasi za ukuaji wa wastani wa mapato ya kitaifa ya ulimwengu na ya kikanda pamoja na ukosefu wa utashi wa bidhaa ulizuia uwekezaji katika mataifa ya uwekezaji uliopanuliwa sawia na ule unaoegemea raslimali, ingawa mataifa machache yalipokea pesa nyingi kutokana na miradi mipya.

Afrika Kaskazini

Uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja (FDI) katika eneo la Afrika Kaskazini ulipungua kwa 11% kufikia $ bilioni 14, huku ukipungua katika mataifa yote isipokuwa Misri, ambalo lilisalia kupata Uwekezaji wa Kigeni wa moja kwa moja wa juu kabisa barani Afrika mwaka wa 2019, huku ukiongezeka kwa $ bilioni 9.

Chini ya Jangwa la Sahara na Kusini mwa Afrika

Baada ya ongezeko kubwa mwaka wa 2018, uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja katika eneo lililo chini ya Jangwa la Sahara ulipungua kwa 10% mwaka wa 2019 hadi $ bilioni 32. Kanda ya Kusini mwa Afrika pekee ndiyo iliyopata uwekezaji mkuu mwaka wa 2019 (ongezeko la 22% hadi $ bilioni 4.4) ila kutokana na kupungua kwa uwekezaji kutoka Angola. Uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja kuelekea Afrika Kusini ulipungua kwa 15% hadi $ bilioni 4.6 mwaka wa 2019, licha ya uwekezaji muhimu katika uchimbaji madini, uzalishaji viwandani (magari, bidhaa za matumizi) na huduma (za kifedha na benki).

Afrika Magharibi

Uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja katika Afrika Magharibi ulipungua kwa 21% hadi $ bilioni 11 mwaka wa 2019. Hili lilichangiwa sana na kudidimia pakubwa kwa uwekezaji nchini Nijeria, kwa sababu ya taratibu mpya za uwekezaji kwa makampuni ya kimataifa katika sekta ya mafuta na gesi.

Afrika Mashariki

Uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja katika Afrika Mashariki pia ulipungua kwa 9% hadi $ bilioni 7.8. Uwekezaji katika Uhabeshi ulididimia kwa asilimia nne hadi $ bilioni 2.5 kutokana na misukosuko midogo ya kisiasa katika baadhi ya maneneo nchini humo. Vivyo hivyo, uwekezaji nchini Kenya ulipungua kwa 18% hadi $ bilioni 1.3 licha ya miradi kadhaa mipya katika teknolojia ya habari na huduma za kiafya.

Afrika ya Kati

Afrika Kati ilipokea $ bilioni 8.7 za uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja, ambao ni upungufu kwa 7%. Muhimu katika kanda hii lilikuwa kupungua kwa uwekezaji uliolelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (9% hadi $bilioni 1.5).

Uholanzi ilipiku Ufaransa kama mwekezaji mkubwa katika hisa

Kwa msingi huu wa uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja, data ya hisa kutoka mwaka 2018 inaonyesha kuwa Uholanzi ilipiku Ufaransa kama mwekezaji mkubwa wa kigeni barani Afrika.

Hisa zinazomilikiwa na Marekani na Ufaransa barani Afrika zilipungua kwa 15% na 5% mtawalia, kutokana na faida iliyotumwa nyumbani na kuuza vitengo vya biashara. Kwingineko, hisa za Uingereza na Uchina ziliongezeka kwa 10% kila moja.

Uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja nje ulipungua pia mwaka wa 2019, kwa takriban thuluthi

Uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja nje ya Afrika ulipungua kwa 35% hadi $ bilioni 5.3. Afrika Kusini iliendela kuwa mwekezaji mkuu nje ya Afrika licha ya kupungua kwa uwekezaji kutoka $ bilioni 4.1 hadi $ bilioni 3.1.

Uwekezaji kutoka Togo uliongezeka, kutoka $ milioni 70 hadi $ milioni 700, ongezeko mara kumi. Afrika Kaskazini, Moroko iliongeza uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja, hadi takriban $ bilioni 1 kutoka $ milioni 800 mwaka wa 2019.

Mchoro 1 – idadii wastani ya kila robo ya mwaka kwa uwekezaji wa miradi ya kuuza vitengo vya kibiashara, 2019 na robo ya kwanza mwaka 2020 (nambari)

Chanzo: UNCTAD, Ripoti ya Uwekezaji wa Dunia 2020.

mchoro 2 – Idadi wastani ya kila mwezi ya miungano na ununuzi wa makampuni kati ya mataifa, M&As, 2019 na Januari-Aprili, 2020 (nambari)

Chanzo: UNCTAD, Repoti ya Uwekezaji wa Dunia 2020.

Mchoro 3 – Wapokeaji wa mwanzo 5 wa Uwekezaji wa kigeni wa moja kwa, 2018 na 2019 (mabilioni ya dola)

Chanzo: UNCTAD, Ripoti ya Uwekezaji wa Dunia2020.
Mada: