51³Ô¹Ï

Kubadilisha Kilimo Afrika kwa kutumia Mashine

Get monthly
e-newsletter

Kubadilisha Kilimo Afrika kwa kutumia Mashine

Serikali na wafanyabiashara sharti wazidishe uwekezajai katika sekta hii
Busani Bafana
10 June 2019
Factory worker in Ethiopia explaining tractor use to colleagues.
IFPRI/Xiaobo Zhang
Mtaalamu wa viwanda nchini Ethiopia anaelezea matumizi ya trekta kwa wenzake.

Kwa mujibu wa hayati Calestous Juma, ambaye alikuwa msomi na prefesa katika Chuo cha Harvard Kennedy, ishara inayowakilisha kilimo Afrika ni mwanamke aliyebeba jembe mkononi. Bw. Juma alitumia picha hiyo kuonyesha hali ngumu ya kilimo wanayokumbana nayo wanawake wa Afrika.

Wanawake wanazalisha asilimia 70 ya chakula Afrika katika mashamba madogomadogo, kazi ambayo ni ngumu mno.

Idadi ya watu Afrika inatarajiwa kuwa mara dufu kufikia 2050 na hivyo bara hili lazima liachane na jembe na kutumia teknolojia ya kisasa ambayo itafanya kazi hiyo kwa ubora zaidi.

Mabadiliko kutoka kilimo cha chakula cha matumizi katika mashamba madogo hadi kilimo kinachotumia mashine kwa kusudi la biashara kinawezekana, wanasema wataalamu katika Kituo cha Mageuzi ya Kiuchumi kilichoko Ghana.Ìý Ìý

Hivi sasa Ìýkilimo cha kutumia mashine kipo chini sana Afrika. Idadi ya matrekta yaliyoko Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara ni 1.3 kwa kilaÌý kilomita za mraba nchini Rwanda hadi 43 kwa kila kilomita za mraba Afrika Kusini yakilinganishwa na 128 kwa kila kilomita za mraba kule India na 116 kwa kila kilomita za mraba nchini Brazil.Ìý

Kulingana na Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), shirika la Umoja wa Mataifa ambalo linasaidia juhudi za kuangamiza njaa, Afrika kwa ujumla ina matrekta chini ya mawili kwa hekta 1,000 za mashamba. Kule Asia ya Kusini na Marekani Kusini kila hekta 1,000 zina matrekta 10. Bila kilimo cha kutumia mashine, mazao hupungua sana na kupunguza mapato ya wakulima, kama inavyoelezwa na muungano wa Alliance for a Green Revolution in Africa ambalo ni shirika linalofadhiliwaÌý na Wakfu wa Bill & Melinda Gates na Rockefeller wanaopania kugeuza kilimo na kuimarisha usalama wa chakula Afrilka.

Kwa sasa, Afrika inatumia $35 bilioni kila mwaka kuagiza chakula. Haya ni kwa mujibu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ambayo inakadiria kuwa ikiwa hali hii itaendelea, uagizaji wa chakula utaongezeka hadi $110 bilioni kufikia 2050. Afrika inafaa kuwa gala la chakula duniani, anasema Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Bw. Akinwumi Adesina.

"Teknolojia za kufikia mabadiliko ya mbinu za kilimo zipo lakini zimebakia kwenye rafu. Changamoto ni ukosefu wa sera saidizi za kuhakikisha kuwa zimeimarishwa kufikia mamilioni ya wakulima," anaongeza Bw. Adesina.

Azimio laÌý Maputo

Mnano 2003, viongozi wa Afrika walipitisha Azimio la Maputo kuhusu Kilimo na Usalama wa Chakula ambalo lilitaka mataifa kutenga angalau asilimia 10 ya matumizi ya fedha za umma kwa kilimo kwa lengo la kufikia asilimia 6 ya ukuaji katika sekta hiyo kila mwaka.

Lakini miaka 16 baadaye, ni mataifa 13 tu ambayo yamefikia angalau asilimia 6 ya ukuaji katika sekta ya kilimo jambo linalolemaza ndoto ya Afrika ya mapinduzi ya chakula. Mataifa hayo ni Burundi, Cape Verde, Misri, Gambia, Ghana, Liberia, Mali, Niger, Nijeria, Rwanda, Sierra Leone, na Togo.

Pamoja na Azimio laÌý Maputo, Jopo la Malabo Montpellie, kundi la wataalamu wa Afrika na kimataifa, lilipendekeza mnamo 2014 kwamba mataifa ya Afrika yaunde mipango ya kitaifa ya uwekezaji katika mashine kama hatua muhimu ya kuongeza uzalishaji.

Katika ripoti ya 2018 Jopo la Malabo Montpellie liliorodhesha mataifa 12 ikijumuisha Misri, Malawi, Mali, Morocco, Rwanda, Tanzania na Zambia kama yaliodhihirishaÌý ukuaji bora katika kilimo cha kutumia mashine na hatimaye kufikia uzalishaji mkubwa.

Ufanisi wa kilimo cha kutumia mashine utakuwa muhimu katika kukabiliana na changamoto barani, ripoti hiyo inahitimisha, kuanzia kuongezeka kwa gharama ya uagizaji wa chakula hadi ukosefu wa ajira. Ripoti hiyo inapendekeza kutumia ushirikiano wa sekta ya kibinafsi na ya umma kuunda viwanda vya kinyumbani vya mashine kuhakikisha kuwa teknolojia ya bei nafuu na inayofaa inatumika. Pia inapendekeza kuhamasisha sekta ya kibinafsi kuwekeza katika mashine kwa kuondolewa ushuru.

Mwishowe, kutokana na maendeleo ya nishati na teknolojia ya kidijitali, Afrika inaweza kuanzisha hatua za maendeleo ya kiteknolojia yaliyoafikiwa na maeneo mengine na kufanya mchakato wake wa kutumia mashine kuwa wa haraka na wa kuvutia zaidi, kulingana na ripoti hiyo.

Dkt. Katrin Glatzel, kiongozi wa Programu ya Jopo la Malabo Montpellie ambaye pia ni mtafiti katika Taasisi ya Kimataifa ya Sera ya Chakula, ambalo ni shirika la utafiti wa chakula lililoko Marekani, anasema kuwa zaidi ya nusu ya matunda na mboga zinazozalishwa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara zinapotezwa kutokana na utunzaji mbovu wa baada ya mavuno na ukosefu wa vifaa vya usindikaji.Ìý

Bi. Glatzel anasema kuwa mashineÌý hazitumiki tu katika kulima, bali pia katika kupanda, kuvuna, kusindika na kuhifadhi mazao.

"Kuongeza viwango vya kutumia mashine kutaimarisha michako ya kijamii na kiuchumi katika kazi zinazofanywa shambani na nje ya shamba katika jamii, kupitia upunguzaji wa ugumu wa kazi za shamba na kuongeza mazao," Bi. Glatzel aliiambia Afrika Upya.

"Kutumia mashine hakutasababisha ongezeko la ajira tu bali kutaimarisha usimamizi wa ardhi na mazao pamoja na ubora wa mazao yanayozalishwa pia," aliongezea.

Ili kufikia malengo haya, wakulima katika mataifa yanayostawi lazima watumie fedha zaidi kwa mbolea, mbegu na kemikali za kilimo, FAO lasema.

Baadhi ya Mikakati ya kupendeza

Baadhi ya sekta za kibinafsi zimeanzisha mikakati ya kuingilia kati ili kuziba mwanya ulioletwa na jitihada mbovu za kuendeleza matumizi ya mashine za serikali na wafadhili.

Nchini Nijeria, ÌýHello Tractor, ni biashara mpya ya kiteknolojia inayozidi kupanuka. Inafanana na programu ya Uber na huwapa wakulima uafikiaji wa muda wa matrekta wanapoyahitaji.

Wakulima wanaweza kuitisha trekta kwa ujumbe mfupi wanaotumia wakala ambaye huzikusanya jumbe hizo. Jukwaa la kiteknolojia linaunganisha matrekta yaliyopo na wanaoyaitisha na kufuatilia kila kifaa kinavyotumika.

Kwa kutumia trekta, shamba ambalo lingetumia siku 40 kuandaliwa kwa mikono kwa upanzi linaweza kulimwa kwa masaa 8. Pia ni nafuu kukodisha trekta kuliko kukodisha walimaji wa shamba, anasema Jehiel Oliver, mwanzilishi wa Hello Tractor, mwenye umri wa miaka 35. "Inaonekana kuwa njia pinzani katika masoko haya yaliyo na wafanyakazi wa gharama ya chini, lakini kulipa binadamu bado ni ghali kuliko trakta."

Inakuwa vigumu kupata wafanyakazi kadri wenyeji wa Nijeria wanavyozidi kuhamia mijini na wakulima walioko kuwa wazee. Kutumia trekta kunaweza kusaidia wakulima kupanda kabla ya mvua kuanza. Kwa sababu kupanda kwa trekta kunafaa zaidi kuliko kutumia mikono, kunaongeza pia mazao.

Kule Zambia, Rent to Own, shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa 2010, hukodisha wakulima vifaa kama vile, pampu, mashinikizo, matrekta, mabomba na baiskeli.

Mojawapo ya faidaÌý za kilimo cha kutumia mashine ni kuwa kinaweza kuwavutia vijana shambani na kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana wa Afrika,Ìý ambao ni asilimia 60 ya jumla ya watu waliokosa ajira.

Mfano wa vijana wajasiriamali wa Zimbabwe ni mfano mzuri. Miaka mitatu iliyopita, Kituo cha Kimataifa cha Uimarishaji wa Mahindi na Ngano (CIMMYT) kiliwakopesha Gift Chawara, Shepard Karwizi na Pinnot Karwizi mitambo ya kupanda na kutoa maganda ambayo walitumia kuanzisha biashara.

Kwa sasa kampuni yao inatoa huduma ya kutoa maganda na kupanda kwa familia zipatazo 150 katika kijiji cha Mwanga, kaskazini magharibi mwa jiji kuu la Harare.

Walikuwa wamefuzu kutoka kwa mafunzo ya kilimo cha kutumia mashineÌý yaliyosimamiwa na CIMMYT.Ìý Msimu uliopita watatu hawa walipata karibu dola za Marekani 7,000 kutokana na kutoa maganda zaidi ya tani 300 za mahindi, kwa mujibu waÌý CIMMYT.Ìý

Lakini vijana hawa wenyeji wa Zimbabwe waweza kuwa wa kipekee, anasema Frédéric Baudron, mkuu wa mitambo ya kilimo cha biashara katika CIMMYT. Ametambua kuwa matumizi ya mashine na wakulima wa mashamba madogo nchini Zimbabwe yangali duni.

Programu ya Mafunzo ya Matumizi ya Mashine ya CIMMYT inatekelezwa chini ya Mradi wa Matumizi ya Mashine Shambani pamoja na Kulinda Kilimo na Uzidishi Endelevu na inafadhiliwa na Kituo cha Kimataifa cha Australia cha Utafiti wa Kilimo. Mradi huu umewafaidi zaidi ya vijana 100 kutoka Misri, Kenya, Tanzania na Zimbabwe.

Jitihada kama hizi zikifanywa kote Afrika,Ìý zinaweza kuongeza mazao ya kilimo.Ìý Hata hivyo, serikali zinafaa kuongeza uwekezaji katika sekta hii.

Ni wakati kwa Afrika kutafakari tena kuhusu jembe.

Ìý