51³Ô¹Ï

Wajasiriamali wachanga wa Afrika waweza kusaidia ukombozi wa baada ya COVID-19

Get monthly
e-newsletter

Wajasiriamali wachanga wa Afrika waweza kusaidia ukombozi wa baada ya COVID-19

¡ª Jason Pau, Afisa katika Wakfu wa Jack Ma
Kingsley Ighobor
Afrika Upya: 
22 September 2020
Waliohitimu wa 50 bora wa 2020 ANPI (Africa Netpreneur Prize Initiative) inayodhaminiwa Ushindani wa
Jack Ma Foundation
Waliohitimu wa 50 bora wa 2020 ANPI (Africa Netpreneur Prize Initiative) inayodhaminiwa Ushindani wa Mashujaa wa Biashara wa Afrika.

Wajasiriamali wachanga wa Afrika wanaweza kutekeleza wajibu muhimu katika kulisaidia bara hili kujikomboa kutoka kwa COVID-19, kwa mujibu wa Jason Pau, Mshauri Mkuu wa Mipango ya Kimataifa, Wakfu wa Jack Ma, shirika la misaada linalomilikiwa na Jack Ma, mfanyabiashara wa Kichina na mwasisi wa shirika kuu la biashara za mtandaoni, Alibaba.?

¡°Wawekezaji wachanga wa Afrika ni wabunifu na werevu, na siishi kuvutiwa na ubora wao,¡± bwana Pau aliiambia?AfrikaUpya.

Bwana Pau anahusika sana katika shughuli za wakfu huo barani Afrika, ikiwa ni pamoja na mpango wa African Netpreneur Prize Initiative (ANPI), ambao huandaa shindano la Africa¡¯s Business Heroes ambalo huwapa fursa wajasiriamali chipukizi kuonyesha vipaji vyao.

Na kufuatia kuzuka kwa janga hili, bwana Pau alisaidia kupanga na kugawa vifaa vya kimatibabu vilivyotolewa na Wakfu wa Jack Ma katika mataifa ya Afrika.

Jason Pau
Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika litakuwa neema kwa wajasiriamali, biashara huria itasuluhisha changamoto karibu na malipo, vifaa, ucheleweshaji wa forodha.
Jason Pau

Kwa kuzingatia changamoto zinazotarajiwa katika ukombozi wa baada ya COVID-19, alisema bara hili ¡®linahitaji viongozi zaidi wachanga wa biashara wanaoweza kuonyesha njia tofautu za kufaulu na njia tofauti za uongozi.¡±

Ni lazima Afrika ¡°kutumikisha vipengele muhimu katika idadi yake ya watu kujikuza kiuchumi. Kutakuwa na haja ya kufanya mabadiliko makuu katika sekta kama elimu, afya, teknolojia, na miundomsingi,¡± alisema.?

Aliorodhesha elimu, miundomsingi na huduma ya e-government kama vipengele muhimu vya kuuwezesha ujasiriamali barani Afrika.

Afrika inastahili kukielimisha kizazi kijacho kuwa kibunifu, chenye huruma na kinachotambua utamaduni wake. ¡°Hisabati na uainishaji ni muhimu, lakini nadhani tunastahili kuwafundisha watoto kuwa watu,¡± alisisitiza.

Zaidi ya hayo ni haja ya kupata mtandao na kuwepo kwa taratibu za ugavi na usafirishaji katika bandari. ¡°Hatuwezi kuyasisitiza hayo zaidi,¡± alisema.

Aidha, aliyahimiza mataifa kukumbatia chumi za kidijitali, akitambua kuwa huduma ya e-government itawezesha ¡°uwazi na kuisaidia serikali kuwa na utendaji bora, mbali na kushirikiana na jamii.¡±

Eneo Huru la Kibiashara la Bara Afrika litakuwa na manufaa mengi kwa wajasiriamali, alitabiri, kwa sababu, ¡°biashara huru zitasuluhisha changamoto kuhusu malipo, taratibu za ugavi na usafirishaji, usafiri na uchewasheji wa forodhani.

¡°Vikwazo vinapovunjwa, na ninawazia wajasiriamali niliokutana nao (barani Afrika), masoko yao yataongezeka mara tano hadi 10.¡±?

Africa's Business Heroes
Temie Giwa-Tubosun (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Lifebank Africa, kampuni inayotoa damu hospitalini nchini Nigeria, ilishinda tuzo ya kwanza mnamo 2019. Picha: Mashujaa wa Biashara Afrika

Aliwashauri wajasiriamali Waafrika ¡®kufanya biashara zaidi na wajasiriamali wengine Waafrika. Nimegundua kwamba wafanyabiashara wengi wa kike na wa kiume, wajasiriamali wanaelekea kufanyia shughuli zao kwao zaidi.¡± Biashara kati ya mataifa ya Afrika ni takriban asilimia 18 tu, kulingana na

ANPI ni jitihada ya mkakati wa Ma wa kuwahimiza Waafrika wachanga kutumia nguvu zao za kiujasiriamali kuyasuluhisha matatizo ya kijamii.??

Alieleza, ¡°Tulipata maombi 10,000 mwaka 2019, kutoka kwa mataifa 50 ya Afrika ¡­ Mwaka huu, tumeridhishwa hata zaidi na baadhi ya kazi tulizofanya na washirika asilia wa bara Afrika. Tulipokea maombi 20,000, yakiwakilisha kila moja kati ya mataifa 54 ya Afrika.¡±

Ufanisi wa shindano la mwaka wa 2019 uliuhimiza wakfu wetu kuongeza idadi ya jumla ya msaada utaokaogawiwa washindi kutoka dola milioni 1 mwaka wa 2019 hadi dola milioni 1.5 mwaka wa 2020.

Temie Giwa-Tubosun, Afisa Mkuu Mtendaji wa Lifebank Africa, kampuni inayowasilisha damu kwa hospitali nchini Nijeria, alishinda tuzo ya kwanza mwaka wa 2019. Bi. Giwa-Tubosun aliiambia AfrikaUpya kwamba tuzo ya $250,000 pesa tasmilu alizopokea kutoka kwa wakfu huo zilimwezesha kupanua utendakazi wa biashara yake. ¡°Zilisaidia pakubwa.¡±

Washindi wengine walipokea kati ya $65,000 na $150,000.

Select Author: 

Wakati kampuni ya Bi. Giwa-Tubosun ilipohitaji vipumulio kwa dharura katika kilele cha janga la Covid-19, alisema kwamba, ¡°Wakfu wa Jack Ma ulituunganisha na watengenezaji mwafaka nchini Uchina ¡­ hilo lilitusaidia sana.¡±

Bwana Pau alithibitisha kwamba mbali na kutoa tuzo za kifedha, wakfu huo ulikuwa ¡°ukiunda mifumo ya vielelezo, mitandao ya kitaaluma na mbinu za kupata mafunzo kuhusu raslimali.

Kufuatia kuzuka kwa COVID-19, wakfu huo ulitoa vifaa vya kimatibabu takriban milioni 19, ikiwa ni pamoja na barakoa, vipumulio, mavazi ya kujilinda, vifaa vya kupima miongoni mwa vifaa vingine kwa mataifa ya Afrika.

Bwana Pau alimpongeza Waziri Mkuu wa Uhabeshi, Abiy Ahmed, kwa kuuwezesha utoaji huo. ¡°Tulimwona Waziri Mkuu Abiy akiwa kiongozi imara na mwenye maono, na Bwana Ma akaamua kushirikiana naye kuanzisha na kutekeleza mpango wa ugavi katika bara zima.¡±

Aliongeza kuwa kiongozi huyo wa Uhabeshi alishirikiana na ¡°Umoja wa Afrika, Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Maradhi vya Afrika, Mpango wa Chukula Duniani, Shirika la Ndege la Uhabeshi, na bila shaka, Shirika la Afya Duniani.¡±

Aliuita ushirikiano huo ¡°Kielelezo cha ushirikiano wa umma na sekta ya kibinafsi.¡±

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat alisema kuwa vifaa hivyo vya kimatibabu viliimarisha ¡°mkakati wa hazina ya Vituo vya Kudhibiti Maradhi vya Afrika kuyasaidia mataifa wanachama katika vita dhidi ya COVID-19."?

Wakfu wa Jack Ma ulishirikiana pia na shirika lenzake, Wakfu wa Alibaba, kuanzisha Global MediXchange for Combating Covid-19¡ªjukwaa la wataalamu wa tiba kupokezana maarifa na tajriba muhimu kuhusu vita dhidi ya COVID-19 kidijitali.

¡°Uchina lilikuwa taifa la kwanza kukabiliana na mkurupuko huu kwa kiwango kikubwa. Uchina lilikuwa limeumia kwanza, lilikuwa limepata mafunzo muhimu kuhusu naamna ya kuwatibu wagonjwa, namna ya kuanzisha hospitali, namna ya kushughulikia vifaa vya kujilinda (PPEs), madawa ya kutumia, na kadhalika,¡± bwana Pau alieleza zaidi.

¡°Kwa hivyo, tulijiambia, ¡®mbona tusiyatoe baadhi ya mafunzo kutoka kwa madaktari wa Uchina kwa ulimwengu?¡¯¡±