51Թ

Mitindo na kitambaa: Historia ya Afrika yasimuliwa kupitia kwa mavazi yaliyopigwa chapa kwa nta

Get monthly
e-newsletter

Mitindo na kitambaa: Historia ya Afrika yasimuliwa kupitia kwa mavazi yaliyopigwa chapa kwa nta

Nguzo ya mitindo ya Afrika, vitambaa vya “ankara,” “wax hollandais” au “kitenge” ni kioo cha historia
Franck Kuwonu
Afrika Upya: 
17 September 2020
Maonyesho ya nguo katika She Designs 2018, maonyesho ya wabunifu zaidi ya 50 wa wanawake kutoka nchi
IC Publications, www.icpublications.com
Maonyesho ya nguo katika She Designs 2018, maonyesho ya wabunifu zaidi ya 50 wa wanawake kutoka nchi 30 za Afrika huko Sharm El Sheikh, Misri.

Katika maduka ya nguo ya Afrika Magharibi na Kati au hata mtandaoni, ni rahisi kununua mikoba ya Michelle Obama, viatu vya Michelle Obama au mavazi yanayobana ya [Kwame] Nkrumah.

African bags and clothes
Mifuko na vifaa vingine kutoka Fafa Creations ya Johannesburg

Ila hizi sio bidhaa haswa ambazo zimewahi kutumiwa na mke wa Rais mstaafu wa Marekani au Rais wa kwanza wa Ghana. Wala si viatu, mikoba au mavazi halisi yanayobana mwili.

Hata hivyo, katika ziara ya asubuhi moja ya ununuzi Januari iliyopita, Hawa Diallo na rafiki yake Naa Ayorkor Tetteh walitembea katika vichochoro vya watu wengi vya Marché HLM (Soko la HLM) katika jiji la Senegal, Dakar, wakitarajia kupata bei nzuri kwa bidhaa yoyote kati ya hizo. Soko hilo linajulikana kama mahali bora pa kupata vitambaa.

Kwa hakika, viatu, mikoba na mavazi yanayobana mwili waliyokuwa wakitafuta haswa ni majina maarufu kwa mitindo tofautitofauti na ruwaza za rangi zinazohusiana tu na moja kati ya kitambaa cha muda mrefu na kilichoenea kwingi kutoka Afrika Magharibi na Kati: inayobainishwa kwa rangi maridadi na kuundwa kwa makini kwa kitambaa asilimia 100 cha sufu almaarufu kama “wax hollandais”, “ankara” au “kitenge”.

“Yenye rangi kwa fujo, ruwaza nyingi nyingi, na nzuri ajabu,” ndivyo Sara Archer, mwandishi wa Sanaa, alivyoeleza “wax hollandais” katika ripoti mwaka wa 2016 ya Hyperallergic, jarida la Marekani la mtandaoni kuhusu Sanaa na utamaduni. Wakati huo, kitambaa na mtindo yake vilikuwa sehemu ya maonyesho rasmi katika Makaavazi ya Sanaa ya Philadelphia, mwendo wa saa moja na nusu kwa gari kutoka Jiji la New York.

Asili ya kitambaa hicho kilichopigwa chapa na umaarufu wake barani Afrika ulianza katikati ya miaka ya 1800 wakati kampuni ya Kiholanzi, ambayo sasa inaitwa Vlisco, ilipokiuza katika miji ya pwani ya Afrika Magharibi. Tangu wakati huo, kitambaa hicho kimekuwa nguzo ya mitindo ya Afrika.

Urejelezi wa ainasafu “wax hollandais” ulichimbuka wakati huo. Lakini jina hilo limepanuliwa kurejeleea vitambaa vingine vilivyopigwa chapa, bila kujali mtindo wake wa upigwaji chapa wala mzalishaji wake.

Katika mwongo mmoja uliopita, umaarufu wa kitambaa hicho umekua hadi nje ya bara Afrika, ikiwa ni pamoja na Waafrika walio nje ya Afrika na jamii za Wamarekani Waafrika nchini Marekani.

Zaidi ya mitindo hata hivyo, utamaduni maalum wa kuipa mitindo mbalimbali majina kadri inavyojitokeza, unaifanya moja kati ya tarihi bora ya matukio ya kihistoria na ya sasa, ukikumbusha kuhusu mitindo ya kijamii au kusherehekea kanuni za kimpito.

African fashion and fabric
Kutoka kushoto kwenda kulia: begi la Michelle Obama; Penseli ya Nkrumah; Viatu vya Michelle Obama; Farasi anayeruka; Ubongo wa Kofi Annan.

“Ubongo wa Kofi Annan”

Kitambaa cha kishujaa, kinachotambulika kote ulimwenguni, ni Angelina, pambo lenye muundo mkuu wa V na utepe wa vitone pembeni, kinachosemekana kupata msukumo kutoka kwa utamaduni wa nguo wa Uhabeshi. Jina lake lilitokana na wimbo maarufu wa bendi kuu ya Ghana uliozinduliwa katika kipindi ambacho vitambaa hivi vilikuwa vikiuzwa.

Angelina kinapatikana katika mjumuiko wa rangi mbalimbali na aghalabu huvaliwa kwa mtindo wa kidashiki. Dashiki ni vazi la sufu – ama shati au rinda – lililo na muundo wa V katika ukosi wa mbele na muundo uo huo kudhihirika katikati nyuma.

Muundo mwingine, unaoonyesha fungu la miti iliyokusanywa pamoja katika muundo wa ubongo, unaitwa ubongo wa Kofi Annan. Jina hili litokana na hali kwamba mtindo huo ulikuwa maarufu sokoni wakati Bwana Annan alikuwa akimalizia muhula wake wa pili kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Muundo wa ubongo ulichukuliwa kama ishara ya akili zake pevu.

Kufuatia uchaguzi wa kihistoria wa Rais mstaafu wa Marekani Barack Obama mwaka 2008, wateja walipata njia ya kumtukuza yeye na mkewe Michelle Obama. Miundo miwili ya vitambaa iliyokuwa maarufu sokoni katika kipindi hicho iliitwa moyo wa Barack Obama na mwingine ukaitwa mikoba ya Michelle Obama.

Baadaye Bi. Obama aliyazuru mataifa machache barani Afrika, na muundo mwingine ukapewa jina kutokana na viatu vyake, kuashiria kufika kwake katika bara Afrika. Kuhusu mavazi yanayobana ya Nkrumah, muundo huo unasherehekea ustadi wa kiakili wa shujaa huyu wa mwelekeo wa Waafrika wote.

Kitambulisho cha vitambaa, kinachotambulika ulimwenguni kote, ni Angelina, muundo kuu wa umbo la V-umbo na bendi iliyotiwa alama pembeni, iliyoripotiwa kuongozwa na mila ya mavazi ya Ethiopia.

Hakuna hata jina moja kati ya haya lililotoka katika kampuni husika bali yalitoka kwa wateja waliohusisha mitindo kwa historia kistadi, kuwasherehekea watu mashuhuri au kudhihirisha mitindo ya wakati huo.

Umaridadi wa Kiafrika

Miundo hii ina majina mbadala katika mataifa tofautitofauti

Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kwa mfano, mtindo wa Angelina unaitwa “Ya Mado” kwa sababu wachezaji densi katika video ya wimbo huo walikuwa wamevaa kitambaa cha muundo huo.

Muundo mwingine, maarufu cha cha cha, unaibua hisia za wimbo maarufu wa rumba ya Kongo miaka ya 1960 uitwao “Independence cha cha”. Nchini Ghana muundo huo unaitwa Senchi Bridge kutokana na daraja ya kuning’ini katika Mto Volta inayobembea katika eneo pana unapotembea juu yake. Katika nchi jirani ya Togo cha cha cha inajulikana kama mgongo wa kinyonga.

Iwe DRC, Ghana au Togo, majina haya yanasajili matukio maishani, yakitafakari kuhusu matukio muhimu kama uhuru au mwisho wa vita, au mabadiliko katika matokeo au hali za kibinafsi na zaidi.

Mtu aliyehudhuria maonyesho ya She Designs 2018 amevaa à la Afrochic, Sharm El Sheikh, Misri. Picha: IC Publications, www.icpublications.com

Wanawake ndio waliokuwa wateja wakuu wa kitambaa hiki kwa muda mrefu kwa sababu ya mavazi yake yaliyoundwa kwa mtindo sahili – aghalabu vipande viwili vya sketi na blauzi, au vipande vitatu vya blauzi, sketi na vazi la kiunoni.

Wanaume mara nyingi wangeshona mashati sahili kutokana na kitambaa hiki au mkusanyiko wa shati na suruali zinazovaliwa katika hafla muhimu.

Lakini “mambo yamebdilika,” Mwanamitindo wa Johannesburg, Tanya Kagnaguine aliiambia AfrikaUpya kutoka Afrika Kusini. “Mtindo hauhusu tu vipande viwili au vipande vitatu tena. Unahusu kutoa mitindo mipya ya kisasa yenye uwezo wa kushindana na mavazi yaliyoshonwa tayari kutoka bara Uropa.”

Hii mitindo mipya, Tanya anaiita umaridadi wa Kiafrika, ni mchanganyiko wa mitindo ya kitamaduni ya Afrika na mavazi mapya ya ubunifu.

Wasanii wa Marekani Beyonce Knowles, Rihanna, Madonna; wanasiasa na viongozi ulimwenguni kama Nelson Mandela, Rais wa Ghana Nana Addo Dankwa Akuffo Addo, mke wa Rais mstaafu wa Marekani na pia mke wa Makumu wa Rais mstaafu, Michelle Obama na Jill Biden, wamekikumbatia kitambaa hiki na mitindo yake ya umaridadi wa Kiafrika.

Select Author: 

Ufufuzi wa ankara/kitenge ulipokuwa ukifanyika katikati ya miaka ya 2000, Tanya aliwacha kazi ya mshahara mzuri ya kimataifa na akaianzisha kampuni yake mwenyewe “Fafa Creations” kushughulikia utashi asilia baada ya miaka ya ubaguzi wa rangi.

Cha Afrika Kweli?

Ingawaje ankara/kitenge kinachukuliwa kama kitambaa maarufu zaidi kati ya vitambaa vyote vya Kiafrika, wahakiki wachache wanadokeza kuwa Vlisco, ambayo bado inafanya biashara karne kadhaa baadaye, si ya Kiafrika wala haiko Afrika.

Waanadokeza pia kwamba mtindo wa batik ambao unavibainisha vitambaa asilia unasemekana kuwa ulitoka India, ukatambulishwa mwanzo Indonesia ila haukufaulu kuvutia, kabla ya kuhamishiwa Afrika Magharibi, na kudokeza kuwa fahari ya Kiafrika katika vitambaa hivyo haifai.

“Ni wetu, hata hivyo kwa sababu tuliamua hivyo,” Esi Atiase, mjasiriamali wa kidijitali anayezifanyia shughuli zake Senegal ajibu.

“Vitambaa hivi vimekuwa sehemu ya maisha yetu kila mara, sehemu ya utamaduni wetu, na sehemu ya nyakati zetu za sherehe na huzuni,” anasema. Kulingana naye, inafaa na ni sawa kudai na kusherehekea urithi huo.

Hizi ni hadithi zetu

Ili kutukuza utamaduni huo na kusherehekea urithi huu,Esi na wenzake waliunda video ya vibonzo ya kupitanisha michoro inayoonyesha baadhi ya miundo mashuhuri. Waliionyesha kwa mara ya kwanza katika tamasha za Sanaa zinazofanyika kila baada ya miaka miwili za Dakar mwaka 2016 kabla ya kuionyesha tena baadaye mwaka huo katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jijini Paris, Ufaransa.

Miongoni mwa Sanaa mashuhuri walizotengenezea vibonzo kidijitali ilikuwa the Jumping Horse, ambayo pia huitwa “Je cours plus vite que ma rivale,” yenye maana “Ninakimbia upesi kuliko mshindani wangu.

Katika Afrika Magharibi, mtindo huo uliibuka katika kipindi cha miaka iliyotangulia mkutano wa wanawake wa Beijing 1995, wakati wa mjadala kuhusu haki za wanawake na hadhi ya ndoa za mitala kisheria.

Mtindo mwingine unaohusiana na mjadala huo wa umma ulikuwa Si tu sors, je sors, wenye maana wazi Ukiondoka, nitaondoka. Ingawaje katika kiwango sahili yaweza kuonekana kama kumtahadharisha mpenzi dhidi ya ukosefu wa uaminifu, ilionekana kama tangazo la uamuzi miongoni mwa wanawake wachanga katika eneo hilo kutaka haki zao kuheshimiwa.

Kwa kupitanisha video juu ya vitambaa, Esi anaamini kuwa anahamasisha umma kuhusu umuhimu wa kijamii wa kitambaa hiki, huku akitukuza ubunifu, uzalishaji wa kisanii na chaguo la mteja kutoa maoni yao na kusherehekea maisha kupitia kwa mavazi yao.

“Hiki ni chetu, hizi ni hadithi zetu,” alisema.