51Թ

Uchumi wa raslimali zihusianazo na maji: Wataalam wahimiza matumizi endelevu

Get monthly
e-newsletter

Uchumi wa raslimali zihusianazo na maji: Wataalam wahimiza matumizi endelevu

5 February 2019

Kukiwa na usimamizi mzuri, matumizi endelevu ya raslimali za baharini, maziwani na mitoni— ambayo pia huitwa uchumi wa raslimali zihusianazo na maji—waweza kuchangia hadi dola trilioni 1.5 katika uchumi wa ulimwengu.

Huo ndio uliokuwa mwafaka wa maelfu ya wataalamu, maafisa wa serikali, wanaharakati wa mazingira, waundaji sera na wasomi waliojumuika jijini Nairobi, Kenya, mnamo Novemba 2018 katika Kongamano lililohusu Uchumi Endelevu wa Raslimali zihusianazo na Maji

Huku likiwa na kaulimbiu “Uchumi wa Raslimali zihusianazo na Maji na ajenda ya 2030 kwa Maendeleo Endelevu,” kongamano hilo lililoratibiwa na kuandaliwa na nchi ya Kenya ikishirikiana na Kanada na Japani, liliangazia teknolojia mpya na uvumbuzi baharini, kwenye maziwa na pia mito. Kongamano hilo vilevile liliangazia changamoto, nafasi zinazoweza kupatikana, masuala ya kupewa kipumbele na ushirikiano kuhusu raslimali zihusianazo na maji.

47,000. Ufuo huo mrefu unatoa nafasi kubwa kwa bara hilo kuendeleza sekta zinazohusiana na uchumi wa Raslimali zinazohusiana na Maji,” anasema Cyrus Rustomjee, mtaalamu wa Uchumi wa raslimali zinazohusiana na Maji, ambaye pia ni mhadhiri mkuu katika Kituo cha Kimataifa kuhusu Utawala na Uvumbuzi.

“Bara la Afrika lina mataifa 38 yenye fuko na visiwa na kanda za pwani zenye urefu ulio zaidi ya kilomita “Kupanua uvuvi, kilimo cha majini, utalii, usafirishaji na bandari za baharini na za nchi kavu kunaweza kupunguza umaskini barani Afrika na kuimarisha usalama wa chakula na kawi, nafasi za ajira, ukuaji wa uchumi na uuzaji wa bidhaa nje ya nchi, afya baharini na matumizi endelevu ya raslimali za baharini,” anaeleza Dkt. Rustomjee.

Anasema kwamba watu milioni 12 wanaajiriwa na uvuvi pekee. Hii ni sekta kubwa ya Uchumi wa raslimali zihusianazo na maji Afrika, inayotoa usalama wa chakula na lishe kwa zaidi ya Waafrika milioni 200 na kuzalisha thamani iliyongezwa kwa zaidi ya takribani dola bilioni 24, au 1.26% ya mapato ya mataifa yote ya Afrika.

Jambo lililohofisha katika kongamano lililofanyika Nairobi ni matumizi mabaya yanayoendelea kwa upana sasa katika maeneo ya maji ya dunia, hasa katika nchi zinazoendelea.

Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenyatta, alieleza hofu yake kuhusu ‘uchafuzi mkubwa wa maeneo ya maji yetu; matumizi mengi mabaya ya raslimali za maji pamoja na wanyama na mimea iliyo katika mazingira fulani ya maji. Alisikitikia zaidi changamoto maalumu ya ukosefu wa usalama, hasa katika bahari makuu.

Utetezi wa awali uliofanywa na Kenya, Kanada na Japan, waandalizi wakuu wa shughuli hiyo, kabla ya kongamano lenyewe, ulilenga masuala mengi muhimu kwa mendeleo ya bara la Afrika, yakiwemo usalama wa chakula kwa makundi na jamii zinazokabiliwa na hatari, ukosefu wa lishe bora, uzalishaji endelevu wa chakula na usawa wa kijinsia katika viwanda vinavyohusiana na Uchumi wa Raslimali zihusianazo na maji.

Waziri wa Masula ya Nje wa Kenya, Monica Juma, alisema kwamba majadiliano yalikusudia kutimiza uwezo usiotimizwa unaopatikana katika bahari, maziwa na mito yetu; na yalilenga kujumuisha maendeleo ya kiuchumi, ujumuishwaji kijamii na uendelevu unaopigajeki uchumi wa raslimali zihusianazo na maji unaofana, jumuishi na endelevu.

Huku akisisitiza haja ya kutimiza uwezo kamili wa uzalishaji wa maeneo ya maji ya Afrika, Waziri wa Masuala ya Kigeni wa Kenya Bi. Monica Juma, alisema kwamba alitarajia hasa kuona uhusika ulioongezeka wa wanawake na vijana katika shughuli zote za uchumi wa raslimali zihusianazo na maji.

Ujumbe uliokaririwa katika kongamano hilo ulikuwa kwamba uchumi wa raslimali zihusianazo na maji waweza kuongeza ukuaji wa kiuchumi wa nchi na uhifadhi wa mazingira, na zaidi ya hayo, kusaidia kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Ajenda ya 2030.

Kwa mujibu wa Macharia Kamau, Katibu Mkuu wa Wizara ya Masuala ya Kigeni wa Kenya, kwa jumla kongamano hilo liliwasilisha “nafasi nyingi kwa ukuaji wa uchumi wetu, hasa katika sekta kama vile uvuvi, utalii, usafiri wa baharini, uchimbaji madini karibu na bahari, miongoni mwa mengine, kwa njia ambayo uchumi wa nchi kavu umeshindwa.”

Umuhimu wa kimkakati wa uchumi wa raslimali zihusianazo na maji kwa biashara ni dhahiri kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Baharini, shirika maalumu la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia uratibu wa safari za meli. Kwa mfano, kufikia 90% ya uwezeshaji wa biashara ya ulimwengu kwa wingi na 70% kwa thamani hutekelezwa kwa bahari.

Changamoto moja ni kuwa bahari hufyonza takribani 25% ya dioksidi ya kaboni ya ziada inayoongezwa katika hewa ya dunia kupitia uchomaji wa makaa ya visukuku. Bado mafuta na gesi ndizo asili kuu ya kawi, takribani 30% ya uzalishaji ukifanyiwa karibu na bahari.

Kabla ya kongamano hilo, waandalizi walisisitiza changamoto za sasa katika uchumi wa raslimali zihusianazo na maji, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ufanisi wa pamoja, ukosefu wa usalama wa safari za meli na shughuli zisizo endelevu za mwanadamu karibu na ndani ya bahari, maziwa na mito, pamoja na kuvua kupindukia.

Changamoto nyingine ni uchafuzi, viumbe vamizi, na ongezeko la asidi baharini, ambalo husababisha upoteaji wa jumla ya mimea na wanyama katika mazingira mahususi na kuhatarisha afya ya wanadamu na usalama wa chakula. Isitoshe, mfumo dhaifu wa kisheria, kisera, kirekibishaji na kitaasisi pamoja na maendeleo mabaya ya pwani yasiyodhibitiwa yanakuza changamoto zilizopo.

Ili kukabili matatizo haya, washiriki waliwataka viongozi na waundaji sera kutekeleza sera sahihi na kutenga mtaji mkuu katika uwekezaji endelevu katika sekta hiyo kwa nia ya kuimarisha uzalishaji, ujumuishaji na uendelevu.

Kongamaano la Nairobi lilivutia makini ya ulimwengu kwa uchumi wa raslimali zihusianazo na maji, changamoto kuu kwa sasa ni kuhakikisha kwamba utekelezi wa dhati unaandamana na majadiliano hayo kabambe yaliyoendelea.

More from this author