51Թ

Jinsi wanakijiji wa pwani ya Kenya wanavyoingiza pesa kutokana na malipo ya kaboni

Get monthly
e-newsletter

Jinsi wanakijiji wa pwani ya Kenya wanavyoingiza pesa kutokana na malipo ya kaboni

Mradi wa mikoko wa Mikoko Pamoja unatarajia kuzalisha mapato ya kila mwaka ya takriban $130,000
Afrika Upya: 
19 January 2023
Restored Mangrove trees.
Haji Abdikarim
Restored Mangrove trees at Dabaso Restaurant.

Wazungumzaji wa Kiswahili katika Afrika Mashariki wamebuni neno jipya, “hewa kaa,” kuelezea malipo ya kaboni.

Hewa kaa ni bidhaa ambayo wanakijiji katika eneo la pwani ya Kenya wanayauzia mashirika ya kimataifa kama kichochezi cha kifedha kwao kupunguza utoaji wao wa kaboni. Wanakijiji hawa wakiulizwa wanafanya biashara gani, wanasema, "Tunauza hewa."

Wanakijiji hawa ni baadhi ya wanakikundi kiitwacho Mikoko Pamoja ambao ni mpango wa miradi ya maendeleo katika maeneo ya Gazi na Makongeni katika pwani ya kusini ya Kenya. Mradi huu wa kuigwa unakuza uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za mikoko ili kufikia malengo matatu: kupunguza mabadiliko ya tabianchi, kuhifadhi bayoanuwai na kuimarisha maisha ya jamii.

Kikundi cha Mikoko Pamoja kinahifadhi hekta 117 za mikoko inayomilikiwa na serikali, na hii inawakilisha karibu asilimia 16 ya mfumoikolojia katika Ghuba la Gazi. Katika kipindi cha miaka 20 kuanzia 2013 hadi 2033, mradi huo unalenga kulinda hekta 107 za misitu ya asili ya mikoko na kuhifadhi hekta 10 za mashamba ya mikoko miekundu ambayo yalianzishwa katika maeneo yaliyokuwa bila mimea mwanzoni mwa miaka ya 1990.

Faida za kaboni kutokana na kulinda na kupanda mikoko ni nyingi kwa sababu mikoko huhifadhi kaboni kwenye majani yake na kuifungia kwenye matope ya baharini. Kulingana na Mpango wa Ikweta, zaidi ya tani 1,500 za kaboni kwa hekta huhifadhiwa chini ya misitu ya mikoko, ambayo ni zaidi ya mara nane ya misitu ya nchi kavu.

Kama matokeo ya juhudi hizi, Mikoko Pamoja umekuwa mpango wa kwanza kabisa wa kaboni ya samawati duniani ambao unaopata malipo ya kaboni kutoka kwa shughuli za uhifadhi wa mikoko kwa maendeleo ya jamii, kulingana na Mpango wa Ikweta. Huku miradi mingi ya biashara hii ikiegemezwa katika mifumoikolojia ya nchi kavu, uhifadhi wa bahari ni pamoja na uhifadhi na urejeshaji wa makaro ya kaboni yanayotokana na bahari, kama vile misitu ya mikoko.

Mradi wa Ikweta (Equtor Initiative) ulioanzishwa mwaka wa 2002, ushirikiano wa sekta mbalimbali, unaongozwa na Umoja wa Mataifa, unaleta pamoja serikali, mashirika ya kiraia, wasomi, wafanyabiashara na mashirika ya mashinani ili kutambua na kuendeleza masuluhisho ya uasilia ya maendeleo endelevu ya kijamii kwa watu, asili na jamii nyumbufu.

Why mangroves?
  1. Mangroves, also called the “blue forests,” typically grow in the intertidal zone along tropical and subtropical coastlines.
  2. About 75 per cent of mangroves worldwide are concentrated in just 15 countries, and barely 7 per cent lie in protected areas, according toEquator Initiative. These trees are essential for both human and marine life.

Mangroves:

  • Provide a nursery habitat for much commercial fish and shellfish during their early life stages and contribute to abundance of seafood.
  • Support accumulation of tree debris and bacteria in the water and are an essential food source and refuge for juvenile fish; the knotted mangrove roots protect fish from predators. As such, mangroves help to sustain the fishing industry upon which coastal communities depend for livelihood.
  • Act as a buffer between land and sea. When strong waves turn towards land, mangroves diffuse their force protecting the shoreline and human settlements. This prevents erosion and reduces damage to infrastructure.
  • Protect water quality by removing nutrients and pollutants from storm water runoff before they reach seagrass habitats and coral reefs. Their complex systems also shelter a range of wildlife species, including birds and honeybees.
  • Serve as high-quality carbon sinks, a critical resource for climate change mitigation.

Faida za kaboni kutokana na kulinda na kupanda mikoko ni nyingi kwa sababu mikoko huhifadhi kaboni kwenye majani yake na kuifungia kwenye matope ya baharini. Kulingana na Mpango wa Ikweta, zaidi ya tani 1,500 za kaboni kwa hekta huhifadhiwa chini ya misitu ya mikoko, ambayo ni zaidi ya mara nane ya misitu ya nchi kavu.

Plan Vivo, shirika linazilosaidia jamii kupanda miti na kupata malipo ya kaboni, liliidhinisha Mikoko Pamoja kuuza angalau tani 3,000 za kaboni safi kwa mwaka kuanzia 2013 hadi 2033. Mpango huu unatarajiwa kuzalisha mapato ya kila mwaka ya takriban $130,000.

Biashara zinazoangazia mbele hununua malipo haya, mashirika yasiyo ya kiserikali pia, pamoja na vyuo vikuu na watu binafsi ambao wanataka kudhibiti kaboni, huku wakisaidia watu na mali asili.

Mikoko Pamoja imefadhili mabomba, kutoa maji safi ya kunywa kwa mamia ya watoto katika shule za msingi huko Gazi na Makongeni na karibu watu 5,400 katika jamii pana. Mradi huo pia umesaidia katika ununuzi wa vitabu vya kiada, sare za michezo na vifaa vingine vya kujifunzia kwa watoto 700.

Taasisi ya Utafiti wa Majini na Uvuvi ya Kenya inashirikiana na jamii katika mradi wa mikoko. Dkt. James Mwaluma, mwanasayansi mtafiti na mtaalamu wa masuala ya bahari na mifumo ya pwani katika taasisi hiyo, anaelezea ushirikiano huo: "Siyo tu kwamba tunapanda mikoko mahali ambapo mingine imekatwa, tunashirikisha jamii katika kuuza kaboni kwa jumii ya kimataifa."

Dkt Mwaluma anausifia mradi wa Mikoko Pamoja ambao mapato yake kutokana na mauzo ya malipo ya kaboni yanarudishwa kwa jamii kwa ajili ya kuzijenga shule na hospitali.

Kabla ya kuzinduliwa, upatikanaji wa maji safi na vifaa vya elimu katika kijiji cha Ghuba la Gazi ulikuwa fursa kwa wachache. Mradi huo umepata zaidi ya asilimia 30 ya faida ya mauzo ya kaboni katika elimu, usambazaji wa maji safi, upandaji miti ya mikoko na fursa sawa za ajira kwa watu wengi huko Gazi.

Mikoko Pamoja imefadhili mabomba, kutoa maji safi ya kunywa kwa mamia ya watoto katika shule za msingi huko Gazi na Makongeni na karibu watu 5,400 katika jamii pana. Mradi huo pia umesaidia katika ununuzi wa vitabu vya kiada, sare za michezo na vifaa vingine vya kujifunzia kwa watoto 700.

Mikoko Pamoja ni mojawapo ya miradi mingi ya kijamii ambayo inaungwa mkono na mkakati wa serikali ya Kenya wa Uchumi wa Baharini ambao unalenga kufungua uwezekano wa fursa za ardhi ya bahari katika eneo la pwani kwa ukuaji endelevu, jumuishi na endelevu wa kiuchumi. Pia inapanga kuunda ajira, huku ikihifadhi na kutumia mazingira ya pwani na baharini kwa njia endelevu.

Ikiwa na kilomita 640 za ukanda wa pwani, Kenya iko tayari kuvuna kutoka Bahari ya Hindi kwa kiwango cha viwanda, na kunufaisha jamii za ufukweni. Baadhi ya wanakijiji wanauza malipo ya kaboni kwenye soko la ulimwengu na kurejesha matumbawe ambayo binadamu na mabadiliko ya tabianchi yameharibu, ilhali wengine wakilima na kuuza nyama ya kaa na kufuga samaki wa thamani kubwa.

Dkt. Mwaluma anasema kwamba vijana huko Dabaso, kaskazini zaidi katika ukanda wa pwani, wananufaika na programu nyingi ambazo mpango huo unaunga mkono.

“Katika Dabaso, vijana kutoka kijiji hiki wanajihusisha na kilimo cha kaa na kuzalisha nyama ya kaa ambayo wanaiuza kwenye mikahawa yao wenyewe. Wateja wao hasa ni watalii wanaotembelea miji ya pwani kaskazini ya Watamu na Malindi. Wameanzisha biashara ambayo inazalisha, kwa wastani, $360,000 kwa mwaka na imewaondoa katika mzunguko mbaya wa umaskini.”

Mikoko Pamoja umekuwa mpango wa kwanza kabisa wa kaboni ya samawati ulimwenguni kuuza kaboni kutoka kwa shughuli za uhifadhi wa mikoko kwa maendeleo ya jamii, kulingana na Mpango wa Ikweta. Pamoja na miradi mingi ya biashara ya malipo ya kulingana na mifumoikolojia ya nchi kavu, uhifadhi wa bahari ni pamoja na uhifadhi na urejeshaji wa makaro ya kaboni yanayotokana na bahari, kama vile misitu ya mikoko.

Kama mradi mkuu na kielelezo, mtindo wa Mikoko Pamoja unaigwa katika Msitu wa Vanga Blue, kilomita 60 kusini mwa Ghuba la Gazi, karibu na mpaka na Tanzania. Upanuzi wa Vanga utaongeza mara tatu eneo la mikoko iliyohifadhiwa na kiasi cha malipo ya kaboni inayouzwa, na kuongeza mapato zaidi.

Sayansi nzuri, kukumbatiwa na jamii, ujasiriamali wa kijamii na usaidizi wa serikali umetambuliwa kama misingi ya ukuaji wa mradi ambao unaweza kuigwa na maeneo mengine ya mikoko barani Afrika na Amerika Kusini.

Tangu kuanzishwa kwake, washiriki wa Mikoko Pamoja wameendelea kubadilishana tajriba zao katika ukanda huo, wakibadilishana ziara na jamii za Gambia, Madagascar, Msumbiji, Senegal na Tanzania.


Bw. Newton Kanhema ni Naibu Mkurugenzi, Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa - Nairobi.