Hatua za haraka, za pamoja za kuendeleza haki za kijinsia zilijadiliwa katika Kongamano la kwanza la Kimataifa la Uongozi wa Wanawake lililofanyika jijini Juba, Sudan Kusini.
Takribani viongozi 400 wanawake kutoka nchi 15 za Afrikawalihudhuria kongamano la siku tatu liliofadhiliwa na Umoja wa Mataifa, ambalo lilifunguliwa Jumatatu, wakiwemo marais wa zamani na wa sasa.
Lengo nikusukuma mbele maendeleo, kukabiliana na matatizo na kutafuta suluhisho endelevukwa masuala yanayowaathiri wanawake na wasichana nchini Sudan Kusini na kote Afrika.
Mada ya kongamano ilikuwa ‘Guwa Ta Mara’, ikimaanisha uwezo wa wanawake.
Katika kongamano hilo, wazungumzaji walikubaliana kwambachangamoto zinaendeleakatika uongozi na utawala, mabadiliko ya tabianchi, changamoto za kiuchumi, upatikanaji wa elimu na unyanyasaji wa kijinsia.
"Ulinzi wa haki za wanawake ni muhimu kwetu tulio Serikalini," Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit alisema. “Nchi yetu haiwezi kukubali unyanyasaji wa kijinsia, kwani unazuia amani na maendeleo. Tuendelee kufanya kazi tukilenga kuwepo kwa hali bora ya maisha kwa wanawake na wasichana.”
Huku mkataba wa amani wa mwaka 2018 ukiingia katika awamu yake ya mwisho, alisema kuwa Serikali itajitahidi kutatua changamoto zinazowakabili wanawake na kuwawezesha kote nchini.
Juhudi zinazoendelea zinajumuishakuwapa wanawake fursaya kukuza ujuzi wao ili kushindana vyema katika soko la ajira.
Tayari Serikali ilikuwaimeongeza asilimia ya uwakilishi wa wanawake kutoka asilimia 25 hadi 35, bighairi ya changamoto za ukosefu wa usalama na ukosefu wa mamlaka zinazowakabili.
"Ingawa hatujafikia kiwango hiki kikamilifu, tutajitahidi ili kutimiza na kuruhusu wanawake kushindana kwa asilimia 65 iliyosalia," alisema Rais Kiir.
'Mahali pazuri pa kuanzia'
“Ushiriki wa wanawake katika mabunge ya Afrika umeongezeka maradufu katika miongo iliyopita, lakinilazima itihada zaidi itiwe,” alisema Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed, katika taarifa aliyotoa mbashara kwenye kongamano hilo.
"Mambo mengi yanaendelea kukwamisha uongozi na ushiriki wa wanawake kwa usawa na wenzao wa kiume," alisema, akisisitiza haja ya kuongeza juhudi za kurekebisha hali hii.
"Tunahitajikuunda vuguvugu la kuleta mabadiliko katika uongozi, naSudan Kusini ni mahali pazuri pa kuanzia," alisema, na kuahidi kuwa Umoja wa Mataifa ungeunga mkono nchi ya Sudan Kusini katika juhudi zake zinazoendelea na mafanikio ya baadaye. "Tunahitaji wanawake kushiriki katika utafutaji wa suluhisho zinazofaa kwa wote. Kwa pamoja, tunaweza kubadilisha matamanio kuwa vitendo."
Naibu Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa, Sara Beysolow Nyanti alisema uthabiti naazma ya wanawake wa Sudan Kusini unatia moyo.
"Ni matumaini yangu kwamba Sudan Kusini itabadilika na kuwa na amani wanawake wakiwa kwenye mstari wa mbele," alisema, akiongeza kuwa bila ushiriki wao kamili na sawa na uongozi, Sudan Kusini haitasonga mbele katika safari yake kutoka kwenye mizozo hadi amani na maendeleo.
Hata hivyo, changamoto nchini Sudan Kusini bado zinatatiza. Kipaumbele cha juu ni kuongeza uwakilishi wa wanawake katika taasisi za kisiasa na usalamaili kufikia na kuzidi lengo la asilimia 35 lililowekwa katika makubaliano ya amani ya 2018, ambayo yalimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa muda wa miaka mitano na vilivyosababisha vifo au kuhamishwa kwa mamia ya maelfu ya watu.
Majadiliano pia yatazingatia maandalizi ya uchaguzi wa kwanza wa Sudan Kusini kama nchi huru, unaotarajiwa kufanyika mnamo Disemba 2024.
‘Mikononi Mwao’
Onyesho jipya la video na pichalililoitwa “Mikononi Mwao” liliasisiwa katika kongamano hilo na liliangazia wanawake wanaoongoza juhudi za kueneza amani. Kwa kuakisi mada ya kongamano hilo, nguvu za viongozi wanawake ni nyingi. Wanawake wa Afrika waliwezeshaBaraza la Usalama kupitisha azimio muhimu namba 1325 (2000) linalohusu wanawake, amani na usalama, Wanawake wanazidi kutekeleza majukumu muhimu katika kuimarisha amani. Maonyesho hayo pia yanaangazia changamoto zinazowakabili wanawake.
"Vita vimeua matumainina kugeuza maisha yetu kuwa janga, lakinikazi yangu inanisukuma kuvumiliana kunifanya niwe na matumaini kuhusu siku zijazo,” alisema Olla al Sakkaf, mwanaharakatikijanamwenye umri wa miaka 27 kutoka Yemen, aliyeshuhudia vita vya wenyewe kwa wenyewe vikisababisha uharibifu mkubwa kwa jamii tangu 2014.
"Kila mabadiliko madogo ninayoyaleta katika jamii yangu yananipa matumaini ya maisha bora ya baadaye kwangu na kwa wanawake na vijana kama mimi," alisema.
Alokiir Malual, mwanamke wa pekee aliyetia saini mkataba wa amani wa 2015 nchini Sudan Kusini, pia aliangaziwa katika maonyesho hayo.
"Tunakua," alisema. "Tumetumia mchakato wa amani vizuri, na kuhakikisha mafanikio zaidi kwa wanawake. Tulifikia mgawo wa ushiriki wa asilimia 35 kwa kuungana kama wanawake na kama vikundi, na kuunda masimamo mmoja, dai moja.Mafanikio makubwa ya wanawake wa Sudan Kusini.”