51Թ

Ikiwa ni pamoja na mshikamano wa ulimwengu, Msumbiji waweza kushinda majanga

Get monthly
e-newsletter

Ikiwa ni pamoja na mshikamano wa ulimwengu, Msumbiji waweza kushinda majanga

Kuzishinda changamoto za kiafya, kibinadamu, tabianchi na kiuchumi
Afrika Upya: 
6 May 2021
Winnie Byanyima
UNAIDS
Winnie Byanyima speaking.

Msumbiji imekuwa na dhima kuu katika historia ya bara letu, na nchi yenye msukumo na inayopendeza kiasi kwamba kufika kwangu hapa hunipa furaha kuu. Lakini katika ziara hii, japo nina furaha kuu kujumika tena nanyi, ninauhisi uchungu wenu na ninafadhaishwa na janga la kibinadamu linalotokana na mzozo wa Cabo Delgado.

Kama Katibu Mkuu Mwandamizi wa UN, na kama kiongozi wa kazi ya UN kuangamiza ukimwi, nimekuja Msumbiji kuudhihirisha umoja wetu nanyi, na kujifundisha njia bora za kuimarisha usaidizi wetu kwenu. Katika kipindi hiki cha uchungu kwa Msumbiji, sisi Umoja wa Mataifa tuko nanyi.

Kama Wamsumbiji kutoka serikali, mashirika ya kiraia na jamii mbalimbali walivyotueleza, athari za janga la kibinadamu zinasadifiana na athari za kijamii na kiuchumiza za janga la tabianchi, na la COVID-19, mlipuko unaoendelea wa virusi vya ukimwi (HIV), na hatari ya deni kubwa ambalo nchi yenu ilikuwa inakabiliana nalo kabla ya kuzuka kwa janga hili. Aidha, kama walivyotaja, huku athari za majanga haya zikihisika katika jamiii yote, hayahisiki na watu wote kwa njia sawa, bali yanaongeza pengo kubwa lililopo la ukosefu wa usawa.

Kuishi na VVU

Wamsumbiji takriban milioni 2.2 wanaishi na VVU ambayo ni idadi kubwa duniani ya watu walio na VVU baada ya Afrika Kusini. Wasichana waliovunja ungo au wanawake wachanga wanne wanaambukizwa VVU kila baada ya saa. COVID-19 na mzozo wa Cabo Delgado umerejesha nyuma hatua za maendeleo ya kuokoa maisha na za kuyabadilisha maisha zilizokuwa zimechuliwa katika Msumbiji kushinda VVU na ukimwi.

Huduma muhimu zikiwemo zinazohusiana na afya ya kingono na ya kizazi pamoja na matibabu ya VVU zimetatizwa, watu wengi wanaoishi na VVU na wale walio hatarini wanakabiliwa na unyanyapaa zaidi , na athari zake kwa mahudhurio shuleni zimeongeza hatari ya maambukizi mapya ya VVU miongoni mwa wasichaana waliovunja ungo. Nimelezwa kwamba ikilinganishwa na mwaka 2019, kumekuwa na ongezeko la asilimia 18 ya visa vya dhuluma za Kijinsia.

Na wakati huu, fedha za serikali zimebanwa na ongezeko la mzigo wa deni ambalo tayari lilikuwa ngumu nchini Msumbiji kabla ya COVID-19 na huku kukiwa na kitulizo fulani kwa deni katika Mpango wa Kusitisha Ulipaji Deni, hakijatosha kutoa fursa ya kifedha inayohitajika na Msumbiji, hususan kufuatia kupungua kwa sana kwa mapato yaliyokusanywa 2020 na 2021.

Lakini kuna matumaini

Kwanza, tunashuhudia namna hatua za uwajibikiaji zinazoongozwa na jamii zinavyosaidia kukabiliana na COVID-19 na katika janga la kibinadamu. Tajriba iliyothibitishwa ya miongo kadhaa kutokana na uwajibikiaji bora wa VVU unaoongozwa na jamii imeisaidia jamii hii, na kwa hakika jamii zilizoathiriwa na VVU zimetekeleza majukumu ya uongozi.

UNAIDS inayasaidia mashirika ya kijamii kutoa huduma za kuzuia VVU na kuwafuatilia wagonjwa wa maradhi ya zinaa ambao wamewacha matibabu na kuwarudisha tena kwa matibabu ikiwa ni pamoja na kuwapa bidhaa muhimu za matumizi ya mwezi. Huku tukiongeza maarifa kutokana na kupunguka kwa vifo viinanavyohuisana na ukimwi kwa asilimia 20 katika Msumbiji tangu 2010, juhudi za majaribio ya kupunguza madhara na kukabiliana na unyanyapaa zinaonyesha namna bora ya kuchukua hatua dhidi ya majanga.

Pili, tumeona, ongezeko la kampeni za kimataifa za utetezi, ambazo Msumbiji ni mtetezi mkuu, kwa Chanjo ya Watu ya COVID-19, kuongeza kasi ya kupata dawa kwa kuzitaka kampuni kuondoa hatimiliki na kutoa fursa za kushiriki maarifa na uelewa. Kuongeza uzalishaji ndio njia ya pekee za kuhakikishia watu wote chanjo na matibabu.

Kituo cha Kudhibiti Maradhi cha Afrika kimetoa mwongozo kuhusu namna Uzalishaji wa Afrika unavyoweza kuimarishwa huku vikwazo vikiondolewa. Kikundi cha “Wazee” cha viongozi wa awali wa kimataifa kikiwakilishwa na Graça Machel, kimesaidia kusaka nadhari ya ulimwengu. Sehemu kubwa ya umma katika mataifa ya kimagharibi, pamoja na wabunge katika mataifa hayo, wanazihimiza serikali zao kutoa fursa ya mataifa kuvifahamu viambata vya chanjo ili kuusaidia ulimwengu kutoka ndani ya janga hili. Wanafahamu kwamba tunaweza kulishinda tu janga hili tukiwa pamoja.

Tatu, tunashuhudia kushirikana kwa vuguvugu pana linalotetea elimu ya wasichana na uwezeshwaji katika Afrika yote. “Education Plus” ni mpango mkuu wa kisera, unaoshinikizwa na kampeni kuu ya haki, kwa sera hizo na ongezeko la uwekezaji ambao utahakikisha kutamatishwa kwa elimu, kupitia mpango wa elimu bora bila malipo ya shule za upili kwa wasichana wote na wavulana, na kuliimarisha kwa: mazingira yasiyo na vurugu, kupata elimu kamilifu ya masuala ya ngono, kutimizwa kwa afya ya kingono na ya kizazi na haki ya kupata huduma, na uwezeshwaji wa wasichana kupitia mpito wa shuleni hadi kazini.

Hatua hizi kwa pamoja, zitapunguza kwa kiwango kikubwa maambukizi ya VVU na zitapunguza pia mimba za mapema. Kwa sasa asilimia 14 ya wasichana nchini Msumbiji wanapata watoto kabla ya kutimu miaka 15, na asilimia 57 ya wasichana wanawapata kabla ya miaka 18.

Watu wote wa Msumbiji wamejitolea kuwatendea mema wasichana. Kuna ushahidi usiotetereka kwamba elimu na uwezeshwaji wa wasichana utachochea maendeleo na ukuaji wa kiuchumi. Na kwa wasichana na wanawake wachanga wenyewe, thamani ya usawa haikadiriki.

Nne, ulimmwengu unapojadiliana kuhusu changamoto za hali ngumu ya kifedha iliyozidishwa na COVID-19, tunaona utambuzi mkuu kwamba uwekezaji katika afya, elimu na uwezeshwaji sio matumzi ghali yasiyoweza kumudiwa, ila uwekezaji muhimu kwa ukombozi na maendeleo ya kitaifa. Aidha tunaona utambuzi mkuu kwamba mishtuko ya hatari za madeni haiwezi kudhibitiwa tu na wakopeshaji pekee, na kwamba hatua za kusitisha ulipaji deni bado ni chache mno.

Kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alivyotaja, ulimwengu unahitaji mchakato wa “kumaliza mawimbi hatari ya madeni, hatari ya deni la ulimwengu na miongo iliyopotea.” majanga yetu mengo hayamaanishi fursa ya kupiga nyuma hatua za uwekezaji huduma ya umma ya ulimwengu bali fursa ya kuongeza juhudi.

Kwa Pamoja, tunastahili kupata na kutenga fedha ili kuhakikisha kwamba hakuna anayesalia nyuma. Sio katika semi, bali katika uhalisia. Misaada zaidi, kufutilia mbali madeni, kuhakikisha kwamba kuna utoaji zaidi wa Haki ya Kuchota katika Hazina Maalum (SDR)– sarafu ya UN – na mgao upya na mkubwa kwa Afrika, asili mpya na bora za mapato ya nchini, na kukabiliana na maenezi haramu ya fedha na ukwepaji kulipa ushuru, yote ni muhimu nay a dharura kabisa.

Kama UN hatuko nanyi sasa tu, bali katika miaka ijayo pia. Tuko nanyi mnapojaribu kusuluhisha janga hili la kibinadamu; tuko nanyi, pia, mnapojaribu kukabiliana na ukosefu wa usawa, na athari za mabadiliko ya tabianchi, ili tuweze kushinda COVID-19, VVU/ukimwi, na umaskini pamoja.

Tukiwa jasiri, pamoja, tunaweza kuyashinda majanga tunayokabiliana nayo.


Bi. Byanyima ni Mkurugenzi Mkuu wa UNAIDS

More from this author