51Թ

Kutumia mfumo wa teknolojia wa ufahamu bandia kuboresha kilimo Afrika

Get monthly
e-newsletter

Kutumia mfumo wa teknolojia wa ufahamu bandia kuboresha kilimo Afrika

Afrika Upya: 
26 March 2021
An irrigation channel in Chad.
Fatoumata Thiam.

Fatoumata Thiam (kutoka Senegal) anazungumza kuhusu utafiti wake wa msingi katika mtandao na elimu ya mfumo wa teknolojia ya ufahamu bandia katika kilimo, na athari kubwa kwa matajario ya Afrika ya kukubali mapinduzi ya 4 ya viwanda (4IR).

Fatoumata Thiam
Fatoumata Thiam

Unaweza kutueleza kidogo kuhusu wewe?

Nilizaliwa Dakar, mji mkuu wa Senegal. Nilikulia kati ya jiji na kijiji chetu, Diofior, umbali wa takriban kilomita 150.

Ni nini kilikuhamasisha kuhusu sayansi na taaluma hii maalum?

Nilijihusisha na sayansi nikiwa na umri mdogo sana kwa sababu baba yangu ni mwanasayansi wa kompyuta.Nilipokuwa mdogo, alikuwa akinipeleka ofisini kwake ambapo aliniruhusu kufanya chochote - kuchora, kuandika, kuchapisha na kucheza na kompyuta. Alikuwa pia na vifaa vya kisasa vya teknolojia, ambavyo nilikuwa navitumia, maadamu sikua naviharibu. Matokeo yake, nikachagua kusomea sayansi ya kompyuta katika chuo kikuu.

Mwalimu wangu wa hisabati katika shule ya sekondari alinishawishi kupenda masomo ya hisabati na sayansi kwa sababu alitufundisha kwa uvumilivu na shauku.

Namna gani safari yako ya mapema ya sayansi iliendelea?

Nilipata shahada yangu ya sayansi katika uhandisi wa kompyuta mwaka 2013 katika chuo cha Université de Thiès, huko Senegal. Kisha nikaendelea katika Chuo Kikuu cha Cheikh Anta Diop hukohuko Dakar Senegal, kwa shahada ya uzamili ya sayansi (Mifumo ya Habari), ambayo nilipata mwaka 2015.

Nilifanya kazi kwenye usanifu wa kupitisha sauti kwa kutumia intaneti (VoIP), hii ni mitandao ambayo haitegemei sana seva za kuwezesha mawasiliano. Kwa ajili ya utafiti ili kumalizia shahada yangu ya uzamili ya sayansi, nilifanya kazi katika mbinu za uhifadhi kwa mitandao ya kihisia isiyo na waya (WSN).

Nachukulia mafanikio yangu makubwa ni miaka miwili niliyokua nikifanya kazi kama mhandisi wa mitandao ya mawasiliano na huduma katika Idara ya Huduma za Habari katika Chuo Kikuu cha Thiès nchini Senegal. Dhamira yetu ilikuwa kuanzisha mfumo wa uthibitishaji uliosambazwa chuo kikuu. Ulikuwa mradi mgumu sana ambao tuliutekeleza vyema

Malengo yako ni yapi juu ya utafiti wako wa uzamifu (PhD)?

Mwaka 2018, nilianza masomo yangu ya Uzamifu kupitia Mfuko wa Udhamini wa masomo ya Sayansi kwa kanda ya Afrika (RSIF), uliosajiliwa katika Chuo Kikuu Gaston Berger nchini Senegal. Utafiti wangu ulikua kuhusu mtandao wa Vitu (the Internet of Things) na mfumo wa teknolojia wa ufahamu bandia au Artificial Intelligence (AI) kama vinavyotumika katika kilimo. Ninakagua ufanisi wa nishati ndani ya mitandao ya umwagiliaji maji na nishati safi ndani ya mifumo inayotokana na jua.

Lengo ni kukuza mfumo wa umwagiliaji unaojiendesha wenyewe (kiautomatiki) ambao utanakili kiwango halisi cha maji na ukuaji wa mazao kwa jumla, kuhakikisha kuwa ni kiasi tu cha maji kinachohitajika kinanyunyiziwa kwenye mimea. Lengo ni kupendekeza suluhisho ambalo litaboresha na kugeuza dhana ya umwagiliaji katika eneo la Niayes kaskazini magharibi mwa Senegal.

Niayes ina hali nzuri ya hewa kwa kilimo na inawakilisha mazingira asili kwa ajili ya uzalishaji wa kilimo nchini Senegal. Hatahivyo, mkoa huo unakabiliwa na kuongezeka kwa viwango vya chumvi na uharibifu wa miti ya Casuarina [ambayo husaidia kuzuia mmomonyoko], inayosababishwa na uuzaji wa ardhi usio rasmi.

Hadi sasa, nimeweza kuanzisha mfumo wa kihesabu wa uhakika na unaopatikana kutokana na ufanisi wa nishati. Pia nina vitu na miradi kadhaa ambayo iko katika majaribio ya kisayansi na miradi mbalimbali inaanzishwa kwa ajili ya machapisho mapya katika muktadha wa mtazamo wetu wa utafiti.

Namna gani utafiti wako unachangia Malengo ya Maendeleo Endelevu?

Utafiti wangu una athari mtambuka katika nyanja mbalimbali za maendeleo endelevu(SDGs). Haja ya kudhibiti na kuboresha rasilimali za maji, na pia kuelekea kwenye mifumo endelevu zaidi ya kilimo ni suala linalotia wasiwasi nchi nyingi zinazoendelea ulimwenguni kote. Utafiti huu utachangia maarifa yanayohitajika hasa katika kufikia lengo hili.

Je! Ni zipi maana pana za utafiti wako?

Janga la COVID-19 limesababisha kuonekana kwa umuhimu wa matumizi ya mtandao kulinganisha na mwelekeo wa jadi wa matumizi ya viwandani. Matumizi zaidi ya kibinadamu ya mtandao yameibuka, kwa mfano, katika kufanya wavuti ionekane na uhusiano wa kibinadamu kama sehemu muhimu ya mikakati ya kufuatilia na kudhibiti kuenea kwa virusi.

Ingawa utafiti wetu unajikita kwenye kilimo, pia tunatathmini matumizi mengine ya mtandao katika muundo wa pamoja, na uwezo mkubwa wa uhamishaji mpana wa programu ambazo tutazitengeneza.

Kwa ujumla, utafiti huu unatoa ushahidi thabiti wa uwezekano wa mabadiliko makubwa ya mapinduzi ya nne ya viwanda (4IR) barani Afrika na hitaji la bara kuwekeza sana katika miundombinu, uwezo na sera zinazohitajika.

Mada: