Mwalimu Peter Tabichi ambaye amepata umaarufu mkubwabaada ya kutunukiwa tuzo ya mwalimu bora duniani mwaka 2019,sasa ameibuka kidedea tena na kuwamshindi wa tuzo ya mtu bora kwa Umoja wa Mataifa nchini Kenyamwaka huu. Tuzo ambayo hutolewa nchini humo kwa mtu ambaye ameleta mabadiliko chanya katika jamii yake.
Akizungumza na kituo cha habaricha Umoja wa MataifaUNICjijini Nairobi Kenya pindi tu baada ya kupokea tuzo hiyo Alhamisi, Bwana Tabichi ameelezea maana ya tuzo hiyo kwake.
(Peter Tabichi)
Ama kweli mafanikio ya mtoto ni juhudi za mzazi na baba yake mzazi Lawrence Tabichi hakuficha furaha yake.
(Baba Tabichi)