51Թ

'Napenda kuufahamisha umma’

Get monthly
e-newsletter

'Napenda kuufahamisha umma’

- Merveille-Noella Mada-Yayoro, 29, mwandishi wa habari na mtayarishaji wa Guira FM huko CAR.
Afrika Upya: 
27 May 2021
Merveille-Noella Mada-Yayoro, 29, is a journalist and a producer with Guira FMMerveille-Noella Mada-Yayor, journalist and a producer with Guira FM, CAR
Merveille-Noella Mada-Yayoro, 29, ni mwandishi wa habari na mtayarishaji wa Guira FM

Merveille-Noella Mada-Yayor, miaka 29, ni mwandishi na mtayarishaji wa Habari wa kituo cha redio. Guira FM cha Ujumbe wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA). Anasema kwamba kuwasiliana na kusambaza habari za kuaminika ndio mchango wake katika kutafuta amani ya kudumu katika nchi yake:

Wewe ni mwandishi na pia mshika usukani katika Guira FM, kituo cha redio cha kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Ni nini ilikuleta kufanya kazi katika ujumbe wa kulinda amani?

Kutokana na janga ambalo nchi hii imepitia, sisi sote tunataka kuchangia katika kurejesha amani ya kudumu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, hii ndiyo sababu yangu ya kufanya kazi katika ujumbe huu unaofanya kazi kurejesha amani. Kwa hiyo, kufanyia MINUSCA kazi ni mchango wangu katika kurejesha amani katika nchini mwangu.

Je, unadhani umetoa mchango kupitia kazi yako?

Naam, mchango chanya. Watu ambao wanajua kuwa mimi ni mwandishi wa habari mara nyingi huja kwangu ili kuthibitisha habari. ''Unaweza kutwambia, habari hii ni kweli au uongo?'' huwa wanauliza. Hata kanisani ninakoshiriki, watu hunipigia simu kupata habari za kuaminika mara kwa mara. Na ikiwa kila mtu anakuja kuuliza habari na mwongozo, inamaanisha kuwa kazi yangu ina mchango muhimu mahali fulani.

Ulitaja ndugu zako kanisani. Mzozo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wakati mwingine huangaliwa kwa mtazamo wa kidini. Je, ni kwa kubadilishana maoni ambapo umeweza kupata msimamo wa katikati?

Katika kanisa langu, huwa nahudumia watoto. Pia tuna muungano unaowaletwa pamoja vijana walio kanisani na kushiriki majadiliano ya kila wiki. Kwa hivyo, kila wikendi, tunakutana wakati wa mazoezi na kujadiliana masuala kadhaa, ikijumuisha amani na uwiano wa kijamii. Daima tunajitahidi kadiri tuwezavyo kuhamasisha watu na kuwafanya waelewe kwamba hakujawahi kutokea mzozo baina ya Wakristo na Waislamu. Mzozo huu ni wa kisiasa. Kwamba sisi sote ni wa nchi hii na kwamba tuna wito wa kufanya kazi pamoja. Hata hivyo, mara nyingi haiwi rahisi.

Je, nini unachopenda zaidi kuhusu kazi yako?

Napenda kuwasiliana na kutaarifu watu, kuwa karibu sana na watu. Nikiwa hewani kwenye redio, nikiwa mbele ya kipaza sauti, nazungumza na watu wengi kwa wakati mmoja, nafurahia sana kufanya hivyo. Pia ninachopenda zaidi ni kuleta habari kutoka nyanjani. Napenda maeneo ya vijijini kwa sababu nikiwa huko napata fursa ya kushuhudia maisha ya kila siku ya watu na mapambano yao.

Je, kuwa kijana na mwanamke kunachangia kitu maalum katika kazi yako?

Kunachangia. Nitakupa mfano. Wakati fulani nilipewa kazi kwenda Kaga-Bandoro [mji ulio kilomita 245 kaskazini mwa mji mkuu, Bangui], eneo ambalo wenzangu wa kike hawawezi kuthubutu kwenda. Lakini nakuhakikishia kwamba ninapoenda nyanjani, watu huwa tayari kunipa habari ninayohitaji. Wao husema: ''Tazama, ni kijana. Aliiacha familia yake huko Bangui na kukubali kuja kufanya kazi na sisi. Tutampa habari zote.'' Watu huwasiliana nami, wanajaribu kuwa karibu nami na kusaidia pale wanapoweza na wakati mwingine huomba mwongozo. Kwa ujumla, watu huwa na wasiwasi huu na hutaka kusaidia na kukuweka katika hali tulivu.

Je, hii pia inakuwezesha kuwasiliana na vijana vijijini? Idadi kubwa ya watu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ni vijana.

Inanisaidia kuwasiliana moja kwa moja na vijana. Kwa sababu mimi ni kijana, vijana huja kwangu. Tunazungumza lugha moja na tunaweza kuwasiliana kwa urahisi.

Katika mahojiano ya awali ulisema, ''sote tunataka amani.'' Ni taswira gani inakujia akilini ukiwazia haya?

Niliwahi kuzuru kambi ya wakimbizi wa ndani na nikakutana na mtoto mchanga, mwenye umri wa karibu mwaka mmoja. Alikuwa uchi akilia na kunitaka mimi, mimi tu, nimbebe mikononi mwangu wakati nikimuhoji mama yake. Kwa hivyo, nilimchukua mtoto huyo na kumbeba huku nikiwa nafanya mahojiano na mamake. Nilijiambia, kama kungekuwa na amani mtoto huyu hangekuwa anaishi katika kambi hiyo. Angekuwa na familia yake katika nyumba yao, wakiishi kwa amani, pengine kule Bangui. Kwa hiyo niwazapo kuhusu amani, nawaza kuhusu wale watoto wote waliohamishwa makwao na ambao wanataka kurudi nyumbani.


Mahojiano haya yamehaririwa na kufupishwa.

More from this author