Bunge kutotekeleza mapendekezo ya ripoti ni jambo la kusikitisha- Profesa Assad
Get monthly
e-newsletter
Bunge kutotekeleza mapendekezo ya ripoti ni jambo la kusikitisha- Profesa Assad
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali nchini Tanzania, CAG Profesa Musa Assad amezungumzia kitendo cha baadhiÌý ya ripoti zinazoonyeshaÌý ubadhirifu kutoshughulikia ipasavyo na Bunge la nchi hiyo. Taarifa zaidi na Arnold Kayanda.
Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi nchini Tanzania kila mwaka hukabidhi ripoti zake za ukaguzi wa taasisi za umma ambazo pamoja na kuonyesha matumizi ya fedha pia hutoa mapendekezo.
Hata hivyo kumekuwepo na shaka shuku kutokana na kitendo cha baadhi ya mapendekezo kutotekelezwa ambapo katika kusaka ufafanuzi nilizungumza hivi karibuni na Profesa Musa Assad, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali Tanzania wakati akiwa New York, Marekani na kumuuliza kulikoni hayatekelezwi?
“Sasa hilo ni jambo ambalo kimsingi ni kazi ya Bunge. Kama tuantoa ripoti inaona kuna ubadhirifu na hatua hazichukuliwi huo kwangu mimi ni udhaifu wa Bunge. Bunge linatakiwa lisimamie na lihakikishe kwamba pahali penye matatizo basi hatua zinachukuliwa. Sisi kazi yetu ni kutoa ripoti tu. Na huo udhaifu nafikiri ni jambo la kusikitisha, lakini ni jambo ambalo tunaamini muda si mrefu huenda litarekebishika.â€
Na je tatizo ni nini?
“Tatizo kubwa tunahisi kwamba Bunge linashindwa kufanya kazi yake kama inavyotakiwa.Na sitaki kuwa labda nasema jambo hili kwa sababu linahusisha watu fulani, hapana ni kwamba Bunge likifanya kazi yake vizuri hata udhaifu ambao unaonekana utakwisha kabisa.â€