Duka langu la vitambaa ni chanzo cha ajira pia kwa vijana Somalia- Amino
Get monthly
e-newsletter
Duka langu la vitambaa ni chanzo cha ajira pia kwa vijana Somalia- Amino
Harakati za ujenzi wa Somalia zikiendelea, wananchi wakiwemo wanawake wanachangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo kwa kufanya biashara na kulipa kodi badala ya kusubiri misaada.Ìý
Amino Abdulle Maow, alÌý maaruf Amino Maow akijitambulisha akiwa kwenye duka lake la kuuza vitambaa vya nguo za wanawake, duka ambalo pia linatoa huduma za ushoni wa mitindo mbalimbali ya nguo hizo.
Amino, akiwa amevalia vazi lake maridadi kabisa na hijab za rangi ya zambarau mpauko anasema kuwa biashara ni kitu muhimu na duka hili ni biashara yake ya kwanza.
"Nauza haya magauni ya kike ambayo unaona, wanawake wengi wanafika hapa dukani kufanya manunuzi yao. Nisingalikuwa naweza kufanya hii biashara iwapo ningalikuwa silipi kodi. Kodi inatumika kusaidia shule, elimu, afya na pia kulipa mishahara ya majeshi ya usalama.â€
Pamoja na kuchangia kwenye kulipa kodi, duka la Amino limekuwa pia fursa ya ajira kwa vijana wa kisomali ambao wanaonekana wakiwa kwenye cherehani wakishona nguo za wateja, kwenye video hii ambayo ni mfululizo wa video zinazoonyesha kile ambacho kinafanyika Somalia kuleta mabadiliko baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa zaidi ya miongo miwili.
Amino anasema..
“Nimeanzisha fursa ya ajira kwa viajna ambao wanahitaji kuajiriwa. Nadhani nimeajiri vijana kama 20. Nashukuru Mungu naweza kuwalipa mishaharaÌý yao na wanafurahia kazi yao.â€
Mfanyabiashara huyu wa kisomali anaamini kuwa wanawake wako mstari wa mbele kuanzia kusimamia na kuendesha familia zao pamoja na kufanya biashara na wao ni tegemeo kubwa Somalia.