51Թ

Jinsi polisi Kenya walivyomnasua raia aliyekuwa amesafirishwa kiharamu

Get monthly
e-newsletter

Jinsi polisi Kenya walivyomnasua raia aliyekuwa amesafirishwa kiharamu

UN News
Afrika Upya: 
1 August 2020
By: 
Jiji la Nairobi, Kenya
World Bank/Sambrian Mbaabu
World Bank/Sambrian Mbaabu Jiji la Nairobi, Kenya

Na sasa ni wasaa wa mada yetu kwa kina ambayo leo inaangazia usafirishaji haramu wa binadamu na changamoto zake. Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na madawa na uhalifu UNODC inasema hili ni tatizo mtambuka linaloikumba dunia nzima na linalohitaji jududi za pamoja za kimataifa kupambana nalo.

Kwa mujibu wa takwimu za ofisi hiyo watu milioni 40 kote duniani wamekwama katika janga la usafirishwaji haramu wa binadamu huku waathirika wakubwa wakiwa ni wanawake na wasicha takribani asilimia 70, ambao wengi huingizwa katika biashara ya ukahaba, kutumikishwa kama watumwa majumbani, mashambani na katika kazi nyingine ngumu kwa ujira mdogo na wakati mwingine bila malipo yoyote. Mwandishi wetu wa Nairobi Jason Nyakundi amezungumza na mmoja wa waathirika Rachel Olusa ambaye kwa msaada wa polisi alifanikiwa kuponyoka na kurudi nyumbani Kenya na pia mwanaharakati wa kupigania masuala ya wanawake na haki za binadamu Ruth Mumbi. Kwako Jason.