Mrakibu Sangya Malla wa Nepal, ambaye kwa sasa anahudumu katika Ujumbe wa Uimarishaji wa Shirika la UN katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO), ndiye Askari wa Kike wa Mwaka wa UN 2021.
Kulingana na Idara ya Mipango ya Amani ya UN, Mrakibu Malla atakabidhiwa tuzo hiyo na Katibu Mkuu wa UN António Guterres katika sherehe ya mtandaoni tarehe 9 Novemba.
Kwa sasa yeye ni Mkuu wa Kitengo cha Afya na Mazingira cha Askari wa MONUSCO, ambacho alisaidia kukianzisha katika jiji kuu la DRC, Kinshasa.
Kitengo hicho kina jukumu la kutekeleza sera na hatua zinazohusiana na afya na ustawi wa wahudumu pamoja na mipango ya kimazingira ya polisi wa UN. Michango yake imeongezea umuhimu wa moja kwa moja katika DRC katika uhalisi wa janga linaloendelea la COVID-19 pamoja na mikurupuko ya awali ya Virusi vya Ebola, pamoja na hali za hatari za kibinadamu na za kiasilia kama mlipuko wa volkeno katika Goma mwezi wa Mei, ambapo kitengo chake kiliwajulisha wenyeji na wahudumu wa UN kuhusu hatua za tahadhari.
“Alisaidia kuanzisha na sasa anaongoza Kitengo cha Afya na Mazingira cha MONUSCO, huku akiimarisha usalama na ustawi wa wadumisha amani na kupunguza hatari kutokana na COVID-19 pamoja na hatari nyinginezo,†Bwana Guterres alisema. “Na anawakilisha jambo kubwa mno — michango mingi ya maafisa wa kike wa askari katika kuendeleza amani na usalama ulimwenguni kote. Kupitia kwa kazi yake, Mrakibu Malla ni kielelzo cha ubora wa Umoja wa Mataifa.â€
Nina fahari kuipokea tuzo hii, na ninatumai itawahimiza vijana wa kike zaid katika nchi yangu na ulimwenguni kuandama taaluma ya polisi, ambayo bado unazingatiwa sana kama ‘kazi ya wanaume'.
Akiwa mtaalamu wa tiba, Mrakibu Malla alisaidia kuanzisha mwongozo wa kuzuia na kupunguza kuenea kwa COVID-19. Ameandaa zaidi ya vikao 300 vya uhamasishaji mwaka huu kuhusu namna ya kuzuia COVID-19 pamoja na ulinzi wa mazingira kwa manufaa ya wenyeji, watawala wa Kongo na wahudumu wa UN. Kama kitovu cha polisi wa MONUSCO kuhusu COVID-19, amekuwa akieneza habari kuhusu chanjo na kusaidia juhudi za utoaji chanjo.
“Nina fahari kuipokea tuzo hii, na ninatumai itawahimiza vijana wa kike zaid katika nchi yangu na ulimwenguni kuandama taaluma ya polisi, ambayo bado unazingatiwa sana kama ‘kazi ya wanaume,†alisema Mrakibu Malla.
Tuzo ya Afisa wa Polisi wa Kike wa Mwaka ya UN ilianzishwa mwaka 2011 ili kuitambua michango aula ya maafisia wa polisi wa kike katika operesheni za amani kusaidia uwezeshaji wa wanawake.
“Kama wadumisha amani wengi katika kipindi hiki kigumu cha janga la COVID-19, Mrakibu Malla amejitolea zaidi ya wajibu kuzihudumia jamii za wenyeji,†alisema Luis Carrilho, Mshauri wa polisi wa UN. “Kwa pamoja na timu yake, juhudi zake katika kuimarisha uhamasishwaji kuhusu afya ya umma na hatari za kiasilia kwa jumla zimewafanya maafisa wenzake pamoja na watu wa Kongo kuwa salama zaidi— jukumu muhimu la kazi ya polisi.â€
Awali Mrakibu Malla alihudumia Ujumbe wa Uimarishaji nchini Haiti (MINUSTAH) tangu 2016 hadi 2017, ambako alikuwa mwanachama wa timu ya matibabu ya Kitengo Kilichoundwa cha Polisi. Alijiunga na Polisi wa Nepal mwaka wa 2008 kama inspekta
Atakabidhiwa tuzo hiyo katika hafla ya 16 ya Juma la Polisi wa UN kuanzia tarehe 8 hadi 12 mwezi wa Novemba. Katika hafla hiyo ya kila mwaka, wakuu wa vitengo mbalimbali vya Polisi wa UN na wataalamu wa operesheni za kudumisha amani, jumbe maalumu za kisiasa na ofisi za kikanda na viongozi wakuu wa UN hujadili masuala ya utendakazi, mienendo na nidhamu, ulinzi wa raia, uzuiaji wa mizozo, kuhakikisha amani endelevu na mada nyinginezo na masuala ya kipaumbele yanayoathiri shughuli za polisi wa UN.Ìý
Karibu polisi 7,300 wa UN , ambao karibu 27% yao ni wanawake, kwa sasa wametumwa katika operesheni za UN za amani ulimwenguni ambako wanajibidiisha kuimarisha amani na usalama wa kimataifa kuyasaidia mataifa wenyeji katika hali za mizozo, baada-mizozo na hatari nyinginezo.Ìý
Kufikia leo, UNPOL tayari imetimiza shabaha ya 2025 iliyowekwa Katika Mkakati wa Usawa wa Kijinsia Miongoni mwa Polisi wa Idara husika kwa wahudumu wa vitengo vyote. Polisi wa kike wanajumuisha asilimia 30 ya polisi na asilimia 15 ya wanachama wa Vitengo vya Polisi Vilivyoundwa. Polisi wa kike wanashikilia asilimia 40 ya nyadhifa za kitaalamu katika Makao Makuu ya UN na asilimia 33 nyanjani. Aidha wanawake wanaongoza nusu ya vitengo vya polisi wa UN katika operesheni za amani za UN.