UNAIDS na PEPFAR kwa pamoja wamechapisha makala yanaoeleza matendo 41 ya mashirika ya kidini katika kutambua watoto ambao hawajatambuliwa; kuboresha mwendelezo wa matibabu, kusaidia vijana kupata usaidizi wa kisaikolojia, huduma na matibabu, na kuwezesha makundi ya usaidizi wa marika.
Jamii za kidini na mashirika ya kidini yana historia ndefu ya kutunza watoto na vijana wanaoishi na kuathiriwa na VVU.
Hata hivyo, jitihada hizi hazijahifadhiwa vizuri katika maandishi na hivyo michango yao haijaeleweka vizuri. Hadi kufikia sasa.
UNAIDS na PEPFAR kwa pamoja wamechapisha zinazosaidia katika kukabiliana na upungufu huu wa habari.
Makala hayo yanaoeleza matendo 41 ya mashirika ya kidini unaotoa ithibati za wajibu muhimu ambao umetekelezwa na mashirika ya kidini katika kutambua watoto ambao hawajatambuliwa wanaoishi na VVU, kuboresha mwendelezo wa matibabu, kusaidia vijana kupata usaidizi wa kisaikolojia, huduma na matibabu, na kuwezesha makundi ya usaidizi wa marika ili kuwawezesha watoto na vijana wanaoishi na VVU.
Makala hayo pia yanaeleza jinsi viongozi wa kidini walivyoendesha utetezi wa kupambana na unyanyapaa na ubaguzi na kushinikiza serikali ili zitimize malengo. Baadhi ya matendo yenyewe yanajumuisha:
- Nchini Zambia, kwa kupanua utoaji wa huduma jumuishi za afya kupitia vituo vya afya ndani ya maeneo ya ibada, watoto wengi zaidi walitambuliwa walipopimwa VVU katika maeneo ya jamii za kidini ikilinganishwa na wale waliopimwa katika maeneo ya jamii zisizo za kidini na kufikia wastani wa 15% na 7%, mtawalia katika kipindi cha nusu mwaka wa Mwaka wa Fedha wa 2021.
- Nchini Nijeria, mtazamo unaozingatia ushirika wa kidini wa kupima VVU kwa wanawake wajawazito, kwa kutumia Sherehe za Kabla ya mtoto kuzaliwa, uligundua hatua bora ya upimaji wa VVU miongoni mwa wanawake wajawazito (pamoja uunganishi kwa 93%) na wapenzi wao wa kiume, ambao walikuwa na uwezekano mara 12 zaidi wa kujua hali zao, ikilinganishwa na wapenzi wa wanawake wanaojifungua ambao hawakushiriki katika hatua hizi.
- Viongozi wa kidini na mashirika ya kidini katika nchi kadhaa wamejiandikisha kama Mabingwa Madaktari wa Watoto wa Kidini wameimarisha ushirikiano wa kijamii kupitia makundi mbalimbali wakati mwingine - Wakristo na Waislamu - ikijumuisha viongozi wa kidini, viongozi wa vijana, pamoja na viongozi wa makundi ya wanaume na wanawake.
- Mabingwa Madaktari wa Watoto wa Kidini wametoa utetezi kwa serikali na wanajamii ili watoto na vijana wote wasaidiwe kupata huduma na matibabu ya VVU.
Makala hayo yanaonyesha athari za mageuzi za mitazamo ya kidini, ikiangazia mikakati bunifu, programu, na hatua ambazo zimeokoa maisha na kukuza ustawi wa vijana.
Kwa kuleta pamoja uwezo wa dini na hatua unaotegemea ithibati, mashirika haya yameunda nguvu inayozidi matibabu ya hospitalini.
Wamekuza hisia za kuhusishwa, upendo, na usaidizi, na kuunda nafasi salama ambapo watoto na vijana walioathiriwa na VVU wanaweza kupata faraja, mwongozo, na uwezeshaji.
Mwitikio wa kimataifa wa kukomesha UKIMWI kwa watoto unazidi kuwa duni
Kila saa moja watoto kumi na mmoja hufa kutokana na UKIMWI. Watoto milioni 1.7 wanaishi na VVU huku robo tatu (76%) ya watu wazima wanaoishi na VVU wanapata matibabu ilhali ni nusu (52%) tu ya watoto wanaopata.
Watoto wanaoishi na VVU wako hatarini zaidi kuliko watu wazima: huku ikiwa watoto ni 4% ya watu wanaoishi na VVU, wanawakilisha 15% ya vifo vinavyotokana na UKIMWI.
Katika Dibaji yao ya Makala hayo Winnie Byanyima, Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS na John Nkengasong, Mratibu wa Ukimwi Duniani kutoka Marekani na Mwakilishi Maalum wa Diplomasia ya Afya Duniani wanasema: "Ni aibu kwamba ulimwengu unalegea katika hatua za kukomesha UKIMWI kwa watoto" na wanaeleza ukosefu wa usawa kati ya watu wazima na watoto kuwa " ni wa kuvunja moyo."
Hata hivyo, pia wametoa wito wa pamoja: "Tunaweza kukomesha UKIMWI kwa watoto. Lazima tukomeshe UKIMWI kwa watoto. Pamoja tutakmesha UKIMWI kwa watoto. Makala haya yenye kuelimisha, kutia moyo, yatatumika kuokoa na kubadilisha maisha ya watoto.â€