51Թ

Wasichana wasiogope sayansi kwa sababu inatuzingira kila mahali- Bi Wahome

Get monthly
e-newsletter

Wasichana wasiogope sayansi kwa sababu inatuzingira kila mahali- Bi Wahome

UN News
By: 
Bwibo Khayrath Mohamed Kombo, 15, ni mmoja wa wasichana walioshiriki kambi ya kuwawezesha wasichana kuwa wabobevu katika programu za Kompyuta iliyofanyika Addis Ababa mwaka 2018.  Picha:UN Women/Faith
Picha:UN Women/Faith. Bwibo Khayrath Mohamed Kombo, 15, ni mmoja wa wasichana walioshiriki kambi ya kuwawezesha wasichana kuwa wabobevu katika programu za Kompyuta iliyofanyika Addis Ababa mwaka 2018.
Picha:UN Women/Faith. Bwibo Khayrath Mohamed Kombo, 15, ni mmoja wa wasichana walioshiriki kambi ya kuwawezesha wasichana kuwa wabobevu katika programu za Kompyuta iliyofanyika Addis Ababa mwaka 2018.

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi, Shirika la Umoja wa mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN- Women na lile la elimu sayansi na utamaduni, UNESCO yamesema sauti za wanawake na wasichana na ujuzi katika sayansi, teknolojia na ubunifu ni muhimu katika kuleta suluhu katika Dunia ya sasa ambayo inashuhudia mabadiliko ikiwemo mabadiliko haribifu.

Halikadhalika mashirika hayo yamesema kuna haja ya kuziba pengo katika sekta ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hisibati, STEM na kuimarisha usawa wa kijinsia katika kazi husika.

Kauli hiyo imethibitishwa na Anastasia Wahome,mkuu wa kitengo cha sayansi na takwimukatika shirika la kikanda la kiserikali linalousika na usimamizi wa rasilimali kwa ajili ya maendeleo lililoko jijini Nairobi, Kenya akisema kuwabado wasichana hawajakumbatia masomo ya STEM kama inavyohitajika kwa kuwa wasichana wengi bado wana hofu ya kujifunza masomo hayo kutokana na kukosa watu wa mfano kwao.

Akaenda mbali zaidi na kutoa wito kwawasichana ambao wangependa kujikitia katika masomo ya sayansi wajitokeze.