51Թ

DRC ni kimbilio kwa maelfu ya watu wanaokimbia machafuko Sudan Kusini

Get monthly
e-newsletter

DRC ni kimbilio kwa maelfu ya watu wanaokimbia machafuko Sudan Kusini

UN News
By: 
Bongyereirwe Wakimbizi wa Sudan Kusini waliopo nchini Uganda. Picha: WFP/Henry
Picha: WFP/Henry. Bongyereirwe Wakimbizi wa Sudan Kusini waliopo nchini Uganda
Picha: WFP/Henry. Bongyereirwe Wakimbizi wa Sudan Kusini waliopo nchini Uganda

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema limeshuhudia ongezeko la wakimbizi kutoka nchiniSudan Kusini wanaowasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,DRC.

Akizungumza na waandishi habari mjini Geneva, Uswisi hiileo msemaji wa UNHCR Babar Baloch amesema maelfu ya watu walio na wasiwasi wa usalama waowamevuka mpaka kufuatia mapigano yanayolenga raia.

“Inakadiriwa kuwa wakimbizi 5000 wamewasili katika vijiji vya mpakani karibu na mji wa Ingbokolo, kaskazini mashariki mwa jimbo la Ituri kwa mujibu wa machifu walioko mashinani. Kuna ripoti kuwa watu wengine 8,000 wamefurushwa makwao, vitongoji vya mji wa Yei.”

Kwa mujibu wa UNHCR, watu wanakimbiamapiganoyaliyozuka Januari 19 mwaka huu kati ya jeshi la serikali na kundi lililojihami la National Salvation Front katika jimbo la Equatoria kati linalopakana na DRC na Uganda.

“Nchini DRC wale wanaokimbia machafuko Sudan Kusiniwaliwasili kwa miguu mwishoni mwa wiki, wengi ni wanawake, watoto na wazee. Waliwasili wakiwa wamechoka, wana njaa na kiu. Miongoni mwao kuna wanaoumwa malaria na magonjwa mengine.”

UNHCR imeongeza kuwa idadi kubwa yawanaowasili wamekumbwa na kiwewe baada ya kushihidia ukatili ikiwemo watu waliojihami wakiua, kubaka na kupora vijiji.