51Թ

Jamani jiungeni nasi kwenye mradi wa kuondoa umaskini CAR- Mnufaika

Get monthly
e-newsletter

Jamani jiungeni nasi kwenye mradi wa kuondoa umaskini CAR- Mnufaika

UN News
By: 
Mradi wa kupunguza ghasia kwenye jamii, CVR ukiwa na wanufaika 2000 huko mjini Bambari, jimbo la Ouaka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR.  Picha: UN/MINUSCA - Hervé Serefio
Picha: UN/MINUSCA - Hervé Serefio. Mradi wa kupunguza ghasia kwenye jamii, CVR ukiwa na wanufaika 2000 huko mjini Bambari, jimbo la Ouaka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR
Picha: UN/MINUSCA - Hervé Serefio. Mradi wa kupunguza ghasia kwenye jamii, CVR ukiwa na wanufaika 2000 huko mjini Bambari, jimbo la Ouaka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu, CAR, kwa kushirikiana na wadau wameanzisha mradi wa kuwajengea uwezo wapiganaji waliosalimisha silaha zao na kuwa raia wema.

Mradi huo wa shughuli za kilimo na ufugaji unatekelezwa kando kando mwa mto Ouaka ulioko mji wa Bambari, jimboni Ouaka.

Msimamizi wa mradi huo kwenye kituo hicho cha kilimo na ufugaji, Faustin Doulouamba anasema ufadhili unatoka MINUSCA na shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM ambapo washiriki wanalima bustani na lengo ni kutokomeza umaskini na zaidi ya yote..

“Mradi huu unalenga kusaidia kurejelea tena kwenye jamii watu waliokuwa wakijiunga na vikundi vya kujihami ambao hawawezi kusaidiwa na mpango wa kitaifa wa kusalimisha silaha na kujinga tena kwenye jamii, DDR pia na vijana wanaoishi kwenye mazingira hatarishi.”

Miongoni mwa wanufaika ni Flaure Ngouane naye anapaza sauti akisema..

"Mradi huu ambao umeanzishwa na MINUSCA na IOM kwa faida yetu utatuwezesha kuondokana na umaskini lakini pia utatuwezesha kujitegemea kiuchumi. Natoa wito kwa wale wote wanaovutiwa na mradi huu waje waungane nasi. "

Tangu mwezi Agosti 2017, MINUSCA imekuwa ikitekeleza miradi ya kuwajengea uwezo wapiganaji waliojisalimisha katika taifa hilo ambalo limekuwa na ghasia za wenyewe kwa wenyewe tangu mwaka 2012.