Lishe bora ni haki ya kila mtoto:UNICEF
Get monthly
e-newsletter
Lishe bora ni haki ya kila mtoto:UNICEF
Lishe bora na huduma zingine za msingi kama elimu na afya ni haki ya kila mtoto kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, lakini mara nyingi mamilioni ya watoto hukosa haki hiyo hususani lishe bora kutokana na sababu mbalimbali. UNICEF inasema hali hiyo inaweka afya za watoto hatarini na pia njiapanda mustakhbali wao.
Mkoani Ruvuma nchini Tanzania kuna watoto walioathirika na utapia mlo kwa kukosa lishe bora, lakini wengine hata kushindwa kuhuduria masomo kwa sababu hiyo. John Kabambala kutoka Radio washirika Tanzania Kids FM alitembelea shule ya msingi Gracious ya mjini Songea mkoani humo kupata maoni ya waalimu na wanafunzi kuhusu haki ya lishe bora kwa watoto na jukumu la wazazi kuhakikisha haki hiyo inatimia.
Mwalimu Estina Msigwa anasema kuna wazazi ambao wanajipendelea zaidi kuliko watoto wao kwa kula vyakula ambavyo ni vizuri kuliko vile wanavyowapatia watoto wao ingawa anaamini kuna wale ambao hawawalishi watoto wao vizuri kulingana na hali ya kipato. Mawazo yake yanaungwa mkono na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Jaredi Misinze anayesema, “ kuwanyima Watoto chakula kizuri ni kuwanyima watoto haki. Watoto wana haki zote za kupata chakula kizxuri ambacho wao wazazi wenyewe wanapenda kula”