Mada kwa kina: Kala Jeremiah na matumizi ya nyimbo zake kutetea haki za watoto na vijana
Get monthly
e-newsletter
Mada kwa kina: Kala Jeremiah na matumizi ya nyimbo zake kutetea haki za watoto na vijana
Nchini Tanzania wasanii wanatumia mbinu mbalimbali kusaidia jamii inayowazunguka kwa kutambua kuwa msanii ni kioo cha jamii na hivyo akionacho ndicho ambacho anakiwasilisha kwa jamii yake kwa lengo la kuelimisha au kuburudisha jamii hiyo husika.
Wasanii kwa kutumia vipaji vyao iwe ni kuimba au kuchora wanalenga kunasua jamii yao kutoka katika lindi la umaskini, magonjwa au hata ukandamizaji. Miongoni mwa wasanii hao ni Kala Jeremiah ambaye ni mtetezi wa haki za vijana na watoto.
Hivi karibuni alikuwa mkoani Mara nchini Tanzania kwa lengo la kushiriki maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kutokomeza ukeketaji wa watoto wa kike na wanawake.
Ìý
Warren Bright, mkuu Afisa wa Mawasilioano wa shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu, UNFPA nchini Tanzania alizungumza na mwanamuziki huyo nguli wa muziki wa kufokafoka ili kufahamu kulikoni anatumia kipaji chake kutetea haki za watoto na vijana na zaidi ya yote ushauri wake kwa wanamuziki nchini humo.