51Թ

Mahitaji ya kuwatafutia wakimbizi nchi ya tatu yalifikiwa kwa chini ya asimilia 5 tu duniani kote.

Get monthly
e-newsletter

Mahitaji ya kuwatafutia wakimbizi nchi ya tatu yalifikiwa kwa chini ya asimilia 5 tu duniani kote.

UN News
By: 
Prise Josphine na Jemima Nsenga ni wakimbizi waliohamia nchi ya tatu Marekani, waliposhiriki hafla ya kukaribisha kupitishwa kwa mkata wa wakimbizi kwenye Umoja wa Mataifa. Picha: UN News/Grece Kaneiya
Picha: UN News/Grece Kaneiya. Prise Josphine na Jemima Nsenga ni wakimbizi waliohamia nchi ya tatu Marekani, waliposhiriki hafla ya kukaribisha kupitishwa kwa mkata wa wakimbizi kwenye Umoja wa Mataifa.
Picha: UN News/Grece Kaneiya. Prise Josphine na Jemima Nsenga ni wakimbizi waliohamia nchi ya tatu Marekani, waliposhiriki hafla ya kukaribisha kupitishwa kwa mkata wa wakimbizi kwenye Umoja wa Mataifa.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema mwaka jana 2018 mahitaji ya kuwapatia wakimbizi nchi ya tatu ya hifadhi yalikuwa ni chini ya asilimia 5 licha ya kwamba mwaka huo ulivunja rekodi ya idadi ya kubwa ya wakimbizi waliosaka hifadhi ya nchi ya tatu.

Takwimu za UNHCR zilizotolewa leo huko mjini Geneva, Uswiszinafafanua kuwa takribani wakimbizi milioni 1.2 waliohitajikuhamishiwa nchi nyingine kwa mwaka 2018, ni wakimbizi 55,692 pekee ambao walipatiwa makazi mapya.

Idadi kubwa zaidi ya wakimbizi hao waliosaka hifadhi nchi ya tatu kwa msaada wa UNHCR niwalitoka nchi zenye wakimbizi wengi zaidi ikiwemo Lebanon wakimbizi9,800, Uturuki wakimbizi9,000, Jordan wakimbizi5,100na Uganda wakimbizi4,000.

Akifafanua zaidi, Shabia Mantoo ambaye ni msemaji wa UNHCR mjini Geneva, Uswisi amesema,"Asilimia 68 ya majina yaliyowasilishwa mwaka jana walikuwa manusura wa vurugu na mateso, wale wanaohitaji kulindwa kisheria na wanawake na wasichana waliko hatarini. Zaidi ya nusu yaani asilimia 52 ya maombi ya kutafutiwa nchi ya tatu walikuwa watoto”

Kwa mujibu wa UNHCR, katika mwaka huu wa 2019, inakadiriwa kuwa wakimbizi milioni 1.4 ambao wanaishi katika nchi 65 duniani kote watahitaji kuhamishiwa katika nchi ya tatu.

Bi. Mantoo amesema wakimbizi wengi ambao wanatakiwa kuhamishwa ni pamoja na wakimbizi wa Syria ambao kwa sasa wanahifadhiwa katika nchi mbalimbali za mashariki ya kati na Uturuki kwa hiyo,“Mkataba wa kimataifa kuhusu wakimbi unatoa wito kwa mataifa mbalimbali kutoa nafasi zaidi za kuwapokea wakimbizi kwa kupanua programu zilizoko hivi sasa au kwa kuanzisha programu mpya”