51Թ

UN-Habitat kupata dola laki 7 kutoka Japan kusaidia wanaorejea Darfur Kusini, Sudan.

Get monthly
e-newsletter

UN-Habitat kupata dola laki 7 kutoka Japan kusaidia wanaorejea Darfur Kusini, Sudan.

UN News
By: 
Wakimbizi wa ndani jimbo la Darfur Sudan wanakabiliwa na changamoto nyingi na ugumu wa kupata maji safi. Pichani ni msichana na kaka yake wakiwa katika kituo cha maji safi cha Abu-Shok kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani illi kuteka maji. Picha: Mahady
Picha: UNAMID/Mohamad Mahady. Wakimbizi wa ndani jimbo la Darfur Sudan wanakabiliwa na changamoto nyingi na ugumu wa kupata maji safi. Pichani ni msichana na kaka yake wakiwa katika kituo cha maji safi cha Abu-Shok kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani illi
Picha: UNAMID/Mohamad Mahady. Wakimbizi wa ndani jimbo la Darfur Sudan wanakabiliwa na changamoto nyingi na ugumu wa kupata maji safi. Pichani ni msichana na kaka yake wakiwa katika kituo cha maji safi cha Abu-Shok kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani illi kuteka maji

Shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-HABITAT mjini Khartoum nchini Sudanlimetangaza kuwaJapan imeahidi mchango wa dola laki 7 kwa ajili ya mradi wa kusaidia wakimbizi wa ndani wanaorejea katika eneo la Alsalam, Darfur kusini nchini humo kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia mwezi Machi mwaka huu hadi Machi mwakani.

Mradi huu utawanufaisha watu 17,100 waliorejea na pia jamii za wenyeji katika kijiji vya Dagariss kilichoko kilomita 22 kusini magharibi mwa Nyala ambao ni mji mkuu wa Darful Kusini.

Kijiji cha Dagariss ni moja ya jamii ambazo zimeshuhudia idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani wanaorejea Darful. Hata hivyo wanakabiliwa na hali mbaya na uhaba wa huduma muhimu, usalama na wako katika uhitaji mkubwa.

Kupitia msaada huo wa Japan, mradi unalenga kusaidia urejeaji endelevu wa wakimbizi wa ndani na kuhakikisha usalama kwa pande zote yaani wanaorejea na wenyeji hasa katik suala la haki ya ardhi.

Mradi huu unafuatia maamuzi ya Baraza la Usalama yaliyofikiwa Julai 2018 hususani ibara ya 46 inayozungumzia umuhimu wa kukabiliana na masuala ya ardhi kwa ajili ya suluhu ya kudumu katika eneo la Darfur na kuweka mazingira safi ya kuruhusu wakimbizi wa ndani kurejea.

Mwaka uliopita, 2018, Japan iliipatia UN-Habitat kiasi cha dola laki 9 kuwasaidia wakimbizi wa Sudan Kusini na jamii za wenyeji katika eneo la Aljabalain nchini Sudan.