Sanaa mbali ya ajira ni daraja la amani:UN
Get monthly
e-newsletter
Sanaa mbali ya ajira ni daraja la amani:UN
Mbali ya kuburudisha , kuelimisha na kuleta kipato kwa maelfu ya watu wanaoikumbatia, sanaa pia ni chachu ya kuchagiza amani kwakuwa inawaleta watu pamoja, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Sanaa ni moja ya mbinu zinazotumiwa na Umoja wa Mataifa kueneza amani na kuondoa migogoro kote duniani. Aidha Sanaa inatumika pia kama ajira. N amiongoni mwa wanaoitumia Sanaa kujipatia kipato ni Bi Rose Luangisa ambaye ni mtayarishaji wa maonesho ya vitu vya asili kutoka barani Afrika na mwaka huu wa 2019 ameshiriki katika maonesho ya Sanaa ya Umoja wa Mataifa yaliyopewa jina ‘Sanaa kwa ajili ya amani’ yakifanyika katika makao makuu ya umoja huo jijini New York Marekani. Baada ya maonesho hayo Bi Luangisa ameketi na UN News Kiswahili kuzungumzia suala hilo. Akizungumza nami ameanza kwa kuelezea watu wanavyofaidika na shughuli za Sanaa.