51Թ

UN yazindua mikakati wa kupambana na taarifa potofu dhidi ya COVID-19

Get monthly
e-newsletter

UN yazindua mikakati wa kupambana na taarifa potofu dhidi ya COVID-19

Afrika Upya: 
21 May 2020
Verified will provide information around three themes:  science — to save lives; solidarity — to promote local and global cooperation; and solutions — to advocate for support to impacted populations
WFP/Sonia Assoue
Kuongeza uelewa na kulinda Wananchi wa Chad dhidi ya COVID-19, serikali ya Chad na Umoja wa Mataifa hutegemea watunza habari wa jadi: waandishi wa habari katika miji na wafanyikazi wa jamii na wa mashambani.

Umoja wa mataifa leo umezindua mpango wa kukabiliana na ongezeko kubwala utoaji wa taarifa potofu kuhusu Ugonjwa wa virusi vya corona auCOVID-19kwa kuongeza kasi na ufikishwaji wa taarifa sahihi.

Akitangaza mpango huo wa uhakika auKatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema"Hatupaswi kuwafumbia macho wale wanaotuongoza katika taarifa potofu, hofu na chuki. Upotoshaji unaenezwa kwa mitandao, programu tumishi za jumbe mbalimbali baina ya watu.Waandaaji wa jumbe hizo potofu hutumia njia rasmi kutengeneza na kusambaza taarifa. Ili kukabiliana na hali hii,wataalamu wa afya na asasi kama Umoja wa Mataifa tunapaswa kuwafikia watu kwa taarifa sahihi zenye kuaminika.”

Sayansi , mshikamano na msaada

Katibu Mkuu amesema katika mkakati huo mpya Idara ya Mawasiliano ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa- DGC itatoa taarifa katika dhima kuu tatu:Sayansiili kuokoa uhai, Mshikamano ili kuhamasisha ushirikiano wa ndani na kimataifa na Suluhu ili kuisaidia jamii iliyofikiwa.

Pia itahamasisha kupata kiwango cha unafuu ili kukabili majanga ya tabianchi na kupata suluhu ya umasikini, njaana kutokuwa na usawa.

Mpango huu unahamasisha dunia kujiunga na kuwa sehemu ya kujitoleakutoa taarifana kutoa maudhui ili kuzifanya jamii na familia kuuunganika na kuwa salama.

Wanaojitolea hao wataeelezewa kuwa kama watoaji taarifa wa kwanza wa kidigitali, na watoaji taarifa hao wa kujitolea watapokea taarifa zilizothibitishwa kila siku na zilizo wekwa katika mfumo wa kueleweka ili kuwa suluhu ya kukabiliana na taarifa potofu na kujaza zile zisizo jitosheleza.

Idara ya Mawasiliano ya kimataofa ya Umoja wa Mataifa itashirikiana na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa na mataifa mengine,wahamasishaji, asasi za kiraia, mashirika ya habari na biashara ili kusambaza taarifa za kuaminika, maudhui sahihi na kushirikishamitandao ya kijamii kung'oa chuki namadai yenye madhara.

Guterres ameongeza kuwa“Katika nchi nyingi habari potofu zinazoenea kwenye njia za kidijitali zinazuia mwitikio wa jitihada za kuelimisha jamii kuhusu afya ya na kusababisha machafuko. Kuna hali inayofanyika kutumia vibaya ugonjwa huu kuwalenga vikundi vya pembezoni, ambavyo vinaweza kuwa na madhara zaidi skatika jamii hasa wakati huu ambapo uchumi unazidi kudorora kwenye nchi nyingi hali ambayo ikiachwa inaweza kuwa changamoto kubwa.

Taarifa potofu zina athiri jitihada na kuchagiza uhasama

Mkakati huo utaongozwa na idara ya mawasiliano ya kimataofa ya Umoja huo DGC na kushirikiana na moja ya asasi zinazoongoza katika uhamasishaji wa kijamii ya Purpose kwa ufadhili wa taasisi ya IKEA na Luminate.

Melissa Fleming, Mkuu wa DGC amesema, Mpango huo “ھ”au uhakika pia utafanya kazi kushughulikia hali hii na maudhui yenye matumaini ambayo husherehekea vitendo vya kibinadamu, utaangazia michango muhimu ya wahamiaji, na kufanya kampeni hiyo kwa ushirikiano wa kimataifa.

Kwa upande wake Patricia Atkison, Afisa Mkuu wa Mipango katika taasisi ya IKEA, amesema:“Janga la COVID-19 ni janga la kiafya ambalo halikutarajiwa duniani. Taasisi ya IKEA inajivunia kuunga mkono kampeni ya 'Uhakika' ama 'Verified' na hatua inayolenga kuhakikisha kila mtu anapata taarifa za kisayansi zinazoaminika na ushauri wanaohitaji kuweka familia zao na wapendwa wao salama.”

Naye Nishat Lalwani, Mkurugenzi Mtendaji wa Luminate, ameongeza kuwa“COVID-19inakumbusha kwamba ufikishaji wa habari sahihi, zinazoaminika unaweza kuleta tofauti kati ya hofu na ujasiri, mgawanyiko na umoja, na hata maisha na kifo. Tunajivunia kuunga mkono kampeni hii ya Uhakika na kazi yake ya kukabiliana na ugonjwa wa virusi vya Corona ‘kwa kueneza habari za kuaminika, zenye msingi wa kisayansi kulinda watu na jamii ulimwenguni kote.”

More from this author