51Թ

Kutana na “mrejesha-ndege” wa Afrika anayerejesha pori katika visiwa vya Bahari Hindi

Get monthly
e-newsletter

Kutana na “mrejesha-ndege” wa Afrika anayerejesha pori katika visiwa vya Bahari Hindi

Dkt. Nirmal Shah, mhifadhi bingwa kutoka Ushelisheli, anasaidia kuwaokoa ndege adimu
Africa Renewal
Afrika Upya: 
19 December 2022
Glenn Jackway
Endemic Seychelles Magpie Robin
If you can't read now, just listen to the audio version: 

COP15 ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Uanuwai wa Kibiolojia, unaoendelea kwa sasa huko Montreal, Canada, inatafakari njia na mbinu za kuzuia kupungua kwa bayoanuwai huku maelfu ya spishi zikiwa hatarini duniani kote. Chini ya hali hii, AfrikaUpya ilizungumza na Dkt. Nirmal Shah, mhifadhi bingwa kutoka Ushelisheli ambaye anaokoa baadhi ya ndege adimu sana barani Afrika na kurejesha bayoanuwai iliyoharibika kwenye visiwa vya Bahari Hindi:

Na mwandishi wa Habari wa AfrikaUpya

Mnamo 1998, Birdlife International na Jumuiya ya Kifalme ya Ulinzi wa Ndege (RSPB) waliwasiliana na Dkt. Nirmal Shah kusaidia kuanzisha shirika lisilo la kiserikali ambalo lingeweza kuwa mshirika wao huko Ushelisheli.

Wakati huo, mbali na Madagaska, Ushelisheli ilikuwa na idadi kubwa zaidi ya ndege waliokuwa katika hatari ya kuangamia na ambao walihitaji kuokolewa kutokana na kuangamia, kuliko nchi nyingine yoyote ya Kiafrika.

Kulikuwa na ndege 19 pekee wa aina ya Seychelles Magpie Robin waliosalia kwenye Kisiwa cha Fregate, na ndege huyo alikuwa katika hatari ya kuangamia, hasa baada ya panya kuvamia kisiwa hicho

"Kulikuwa na ndege 19 pekee wa aina ya Seychelles Magpie Robin waliosalia kwenye Kisiwa cha Fregate, na ndege huyo alikuwa katika hatari ya kuangamia, hasa baada ya panya kuvamia kisiwa hicho," Dkt. Shah anakumbuka.

RSPB ilikuwa imetenga fedha kwa ajili ya uokoaji wa spishi hiyo lakini haikuweza kuidhibiti kupitia mtandao kutoka makao yake makuu nchini Uingereza. Jumuiya hiyo ilihitaji shirika la ndani ya Usheliisheli lililojitolea kusimamia mpango huo wa uhifadhi. Hii ilisababisha kuundwa kwa BirdLife Seychelles, inayoongozwa na Dkt. Shah.

Haikuwa kazi rahisi. "Niligundua kuwa kujaribu kuokoa Magpie Robin katika upekee hakungefaulu. Tulihitaji kuvirejesha visiwa vyote katika hali ya pori,” Dkt. Shah anasema.

Akiwa anahisi kusumbuliwa ila asiyetamauka, alizungumza na Global Environment Facility (GEF) kuhusu ufadhili. GEF ni ushirikiano wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, benki za maendeleo za kimataifa na mashirika ya kitaifa, yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali.

Dkt. Shah alifurahi kwa kuwa GEF ilitoa ruzuku kwa ajili ya mpango wa kuokoa spishi za ndege.

Miezi michache baada ya uzinduzi wake, shirika la BirdLife Seychelles lilipewa jukumu la kuhamasisha usaidizi wa mashinani, kitaifa na kimataifa ili kusaidia kuokoa ndege wengine waliokuwa hatarini. Miongoni mwa ndege waliotishiwa ni Bundi wa Seychelles Scops, Paradise Flycatcher, White eye na Warbler, ambao wote walikuwa wameorodheshwa na Muungano wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira (IUCN) kuwa hatarini kuangamia.

Niligundua kuwa kujaribu kuokoa Magpie Robin katika upekee hakungefaulu. Tulihitaji kuvirejesha visiwa vyote katika hali ya pori

"Mradi huo uliangalia sababu za kupungua na hatua, ikiwa ni pamoja na utafiti wa kina ambao ulichangia upatikanaji wa maarifa muhimu ajabu kuhusu flycatcher na bundi aina ya scops.

"Pia ilianzisha ushirikiano wetu na wamiliki wa visiwa vya kibinafsi kwa kurejesha visiwa vyao na visiwa vya matumbawe kupokea, kukuza na kuzidisha spishi hizi," Dk. Shah anakumbuka.

Yalikuwa ni mafanikio makubwa. Idadi ya ndege aina ya Seychelles Magpie Robin iliongezeka, na kuwezesha uhamisho wao hadi visiwa vingine vitatu vilivyorejeshwa.

Kufuatia ukuaji wa idadi ya ndege aina ya robin na urejesho wa bayoanuwai, GEF iliendeleza ruzuku ya pili ili kuongeza idadi ya spishi hiyo. Ruzuku hiyo ililenga kisiwa cha Denis, mojawapo ya visiwa vidogovidogo115 vinavyounda msururu wa visiwa vya Ushelisheli.

Msaada zaidi, chini ya mradi wa Darwin na Chuo Kikuu cha Kent, ulianzisha upandaji miti na urejesho wa pori katika Kisiwa cha Denis.

Makundi ya wastani ya Magpie Robins ya Ushelisheli, Warblers na Fody yalihamishwa hadi visiwa kadhaa na kampeni ya uhamasishaji wa kijamii ilifanyika kwenye kisiwa cha La Digue, ambacho kilitokea kuwa mahali pekee duniani ambapo Flycatcher wa Ushelisheli walipatikana.

Hatimaye, kikundi hicho kilianza mpango wa kuhamisha Flycatcher hadi Kisiwa cha Denis, ambayo yalikuwa mafanikio makubwa ya uhifadhi.

"Flycatcher wananawiri," anasema Dkt. Shah. "Leo hii, Orodha Nyekundu ya IUCN inawaainisha kama spishi inayostahili kuhifadhiwa kwa makini ila isiyo katika hatari ya kuangamia tena," ambayo ni mafanikio makubwa," anasema. "Tunatarajia kwamba idadi ya Magpie Robin wa Ushelisheli itaimarika pia, kwani idadi yao imeongezeka zaidi ya mara nne kwenye visiwa vitano tangu tuanze kazi yetu.

"Seychelles Warbler, ambayo wakati mmoja ilitabiiriwa kutoweka, pia imeondolewa kutoka kwa jamii iliyo hatarini ya Orodha Nyekundu ya IUCN," Dk. Shah anasema.

Anafafanua kazi ya kuokoka kwa spishi hizi na kurejesha asili katika visiwa vya Cousin, Denis, La Digue, Fregate, Praslin na vingine kuwa "isiyo na kifani ulimwenguni kwa spishi zilizo hatarini kuangamia haswa kwa sababu ya hatua inayolengwa ya uhifadhi."

Ademola Ajagbe, meneja wa kikanda wa The Nature Conservancy, anayataja mafanikio yaliyopatikana nchini Ushelisheli kama "jambo la ajabu katika kuwarejesha ndege walio hatarini duniani kutoka kwenye ukingo wa kuangamia kuwa dhihirisho wazi kwamba kukiwa na hali zinazofaa urejesho wa asilia unawezekana"

Mkurugenzi Mshiriki katika ICUN, James Hardcastle anamsifu Dkt. Shah kama mmoja wa wataalamu wakuu wa muungano huo na mwanachaama mkuu wa Tume ya Dunia ya IUCN ya Maeneo Tengefu na Mtandao wa Uokozi wa Spishi, "kwa ushindi wake wa ajabu katika kurejesha pori upya katika visiwa na kurejesha bayoanuwaii.

"Kazi yake ya kufufua na kurejesha spishi za ndege ni ya kiufundi na changamano," Bw. Hardcastle anasema. “Dkt. Shah aliongoza shughuli hiyo kwa ustadi—kutoka katika kuendeleza mawazo, kuhimiza heri njema kisiasa na kupata utaratibu hadi kutafuta utaalamu wa kimataifa na kuanzisha programu inayoweza kutekelezeka katika visiwa hivyo na kwingineko.”

Kulingana na Bw. Hardcastle, “mafunzo yaliyopatikana katika Kisiwa cha Cousin na visiwa vingine vya Ushelisheli kwa miaka 60 iliyopita yamevichochea visiwa na wahifadhi wa mazingira ulimwenguni kote. Pia yamefahamisha sera ya IUCN kuhusu kila kitu kuanzia urejesho wa spishi na kazi bora ya usimamizi kwa urejesho na ufufuzi wa visiwa.”