Wakimbizi wa Sudan Kusini waliokuwa Sudan waanza kurejea nyumbani:UNMISS
Get monthly
e-newsletter
Wakimbizi wa Sudan Kusini waliokuwa Sudan waanza kurejea nyumbani:UNMISS
Mkataba wa amani uliotiwa saini hivi karibuni Sudan Kusini wawa hamasa kubwa kwa mamia ya wakimbizi wa nchi hiyo walioko Sudan kutaka kurejea nyumbani , baada ya kuishi ukimbizini kwa miaka mingi.
Mamia ya wakimbizi wa Sudan Kuisni waliokuwa wakiishi Sudan kwa miaka mingi sasa wameanza kurejea nyumbani kwa hiyari.
Kwa mujibu wa tarifa ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS iliyotolewa leo, takriban wakimbizi 500 wa Sudan Kuisni wamewasili Bentiu baada ya kuishi ukimbizini kwa miaka kadhaa.
UNMISS inasema hatua hiyo inafuatia kutiwa saini kwa mkataba mpya wa amani miezi mitano iliyopita hatua iliyowahamasisha wakimbizi hao kurejea nyumbani kwa hiyari.
Akizungumzia kuwasili kwao kamishina wa kaunti ya Tubkonabwana Kur Yai amesema mabasi matano yalikuwa yamejaza wakimbizi hao ambao ni wanawake na watoto yamewasili Bentiu usiku wa kuamkia leo na mengine mengi yanatarajiwa kuwasili.
Ameongeza kuwa kufutia kuwasili kwa wakimbizi hao serikali inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba ujumuishwaji wa wakimbizi hao kwenye jamii unakuwa shwari na unaostahili.