51Թ

China yadhihirisha COVID-19 inaweza kudhibitiwa

Get monthly
e-newsletter

China yadhihirisha COVID-19 inaweza kudhibitiwa

UN News
19 March 2020
By: 
Vifaa tiba vilivyotolewa na shirika la mpango wa chakula duniani, WFP vikiwasili, Beijing.Vifaa tiba vilivyotolewa na shirika la mpango wa chakula duniani, WFP vikiwasili, Beijing.
Picha kwa hisani ya Yingshi Zhang
Vifaa tiba vilivyotolewa na shirika la mpango wa chakula duniani, WFP vikiwasili, Beijing.

Uzoefu wa China katika kudhibiti kusambaa kwa virusi vya Corona unaweza kutumika kama somo kwa nchi zingine ambazo sasa zinakabiliwa na mlipuko huo wa COVID-19 amesema afisa wa shirika la afya ulimwenguni WHO nchini China.

Akizungumza na UN News Dkt. Gauden Galea amesema wakati visa 153,000 vya matatizo ya mfumo wa kupumua yameripotiwa kote duniani hadi kufikia Jumapili iliyopita , nchini China maambukizi yanapungua na kuonyesha kwamba chanzo cha mlipuko huko kimedhibitiwa .“Ni mlipuko ambao umeshughulikiwa wakati uliposhika kasi ya kusambaa kuanzia kwenye mizizi yake. Hii ni bayana kutokana na takwimu ambazo tunazo pamoja na ufuatiliaji wetu ambapo tunaweza kuona kwenye jamii kwa ujumla.”

Ameongeza kwamba“Hivyo hili ni somo kubwa kwamba chanzo cha kawaida cha mlipuko huu hakipaswi kufikia kiwango cha juu sana ambacho kinatikisa na kulemea kabisa mifumo ya huduma za afya. Ni somo la kudhibi ambalo nchi nyingine zinaweza kujifunza kwa ajili ya mazingira yao.”

Ukurasa kuhusu virusivyacorona & taarifa mpya

Wasomaji wanaweza kupata taarifa na muongozo kuhusu mlipuko wa virusi vya corona (2019-nCov) kutoka Umoja wa Mataifa, Shirika la afya duniani na mashirika mengine ya UN hapa.

Kwa habari mkpya kila siku kutoka UN News, bofya hapa.

Kuelewa vyema homa ya kichomi

COVID-19 ni virusi vipya vya Corona vilivyobainika ambavyo hujulikana kusababisha matatizo ya mfumo wa hewa kama ilivyokuwa MERS na SARS.imekuwa ikifuatilia mlipuko huu tangu Desemba 31 mwaka jana ambapo iliarifiwa kwa mara ya kwanza kwamba ‘homa ya kichomi isiyojulikana chanzo chake imezuka na kubainika Wuhan mji mkubwa Zaidi katika jimbo la Hubei Katikati mwa China.”

Dkt. Galea amesema kulikuwa na maswali makuu matatu ya kuelewa lihusu hatua ya mwanzo ya mlipuko huo ambayo ni :jinsi gani vitusi hivyo vinaambukizwa, ni mlipuko mkubwa kiasi gani na hatua za kuudhibiti.

Dr.Gauden Galea, mwakilishi wa WHO nchini China
Dr.Gauden Galea, mwakilishi wa WHO nchini China

Amesema “Katika wiki tatu za kwanza tulijikita sana na kuangalia uchunguzi wa eneo husika , kwa kuwauliza maswali wachunguzi wa kitaifa , kusaka ufafanuzi wa kimataifa kutoka kwa mtandao wa wataalam, kuuandaa mawasiliano kwa ajili ya vyombo vya habari , na kuwasiliana na washirika kwenye Umoja wa Mataifa katika ofizi zao mjini Beijing.”

Dkto Galea na wafanyakazi wenzie pia walipata fursa ya kuzuru Wuhan na anasema wanaelewa kwamba wakati kulikuwa na changamoto wakati huo kuweka historia ya aina nyingine ingekuwa vigumu. Ameelezea gharama kubwa waliyolipa watu wa Wuhan kutokana na kila kitu kusimama kwa sababu ya corona wakati kwingine China na duniani wakijiandaa na mlipuko huo.

Amesema “hatua hizo zilfanyakazi na kuruhusu sehemu zingine china kuweza kudhibiti mlipuko kwa njia ambayo imesaidia. Muundo wa janga hilo na kiwango kidogo cha idadi ya visa kilichoshuhudiwa nje ya Hubei ni Ushahidi wa mafanikio na kufanyakazi kwa hatua hizi.Ni muhimu kutambua kwamba changamoto hizo sio tu za China na kwamba kuna nchi chache tu ambazo zinazochukua hatua za kasi sana za kudhibi ugonjwa huo.”

Kutoka dharura na kuwa janga la kimataifa

Kufuatia mikutano miwili ya kamati ya dharura ya WHO mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Dkt. Tedross Adhamon Ghebreyesus mnmo tarehe 30 Januari alitangaza mlipuko huo wa virusi vipya vya kurona kuwa dharura inayotia hofu kimataifa na ndio shirika hilo likachukua hatua Madhubuti za kusafirisha vifaa vya upimajina kujikinga kwa nchi mbalimbali duniani.

Na wiki iliyopita WHO ikatangaza kwamba sasa COVID-19 inaelezwa kuwa ni zahma ya kimataifa ambayo ni ya kwanza kusababishwa na virusi vya Corona.

” Unapotambua kwamba imetangazwa dharura ya afya ya kimataifa tangu Januari 30 na sasa tuko katikati ya mwezi Machi ni muhimu sana kuelewa kwamba nchi yoyote ambayo bado haijafikiwa basi huu ni wakati wa kuchukua hatua haraka ili kujiandaa nakuandaa umma kupitia mawasiliano muafaka. Amesema Dkt. Gaela.”