51Թ

Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia ongezeni vita dhidi ya COVID-19 -WHO

Get monthly
e-newsletter

Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia ongezeni vita dhidi ya COVID-19 -WHO

UN News
19 March 2020
By: 
Jumla ya visa vya corona Kusini Mashariki mwa Asia (Hadi kufikia 17 Machi 2020)
WHO
Jumla ya visa vya corona Kusini Mashariki mwa Asia (Hadi kufikia 17 Machi 2020)

Wakati nchini za Kusini Mashariki mwa asia zikiripoti visa zaidi ya 480 wa virusi vya Corona COVID-19 na vifo 8, shirika la afya ulimwenguni WHO leo limetoa wito kwa nchi hizo kuchukua hatua sasa na kuongeza juhudi haraka kukabiliana na ugonjwa huo.

Hadi sasa Thailand ndio inayoongoza katika ukanda huo kwa virusi vya/coronavirusikiwa na visa 177 na kifo kimoja , ikifuatiwa na Indonesia Indonesia yenye visa 134 na vifo 5, kisha India ikiwa na visa 125 na vifo 3, Maldives visa 13 , Bangladesh visa 8, Nepal kisa kimoja na Bhutan kisa kimoja.

Dkt.Poonam Khetrapal Singh, mkurugenzi wakanda hiyo ameonya kwambahali inabadilika haraka sana.

Maambukizi mapya ya virusi hivyo yamekuwa yakiripotiwa na kuthibitishwa.Wakati hii ni ishara ya tahadhari pia ni dhihirisho la haja ya kuchukua hatua Madhubuti Zaidi na juhudi za jamii nzima ili kuzuia kusambaa zaidi kwa COVID-19. Kwa hakika tunahitaji kuongeza juhudi na tena haraka.”

Nchi hizo 11 katika kanda ya WHO ya Kusini Mashariki mwa Asia ni maskani ya zaidi ya robo ya watu wote duniani.

Miongoni mwa nchi hizo 11 nchi 8 zimethibitisha kukabiliwa na mlipuko wa virusiambazo niThailand, Indonesia, India, Sri Lanka, Maldives, Bangladesh, Nepal na Bhutan.

Kwa mujibu wa Dkt. Singh idadi ya visa inaonyesha kwamba baadhi ya nchi hizo zinaelekea kwenye maambukizi makubwa ya kijamii ya ugonjwa huo hatari.Amesema endapo hilo litatokea basiitabidi tung’ang’ane kupunguza maambukizi na kukomesha mlipuko.

inabidi tujipande kukabiliana na hali inayobadilika kwa lengo la kukomesha maambukizi ya COVID-19 mapema ili kupunguza athari za virusi hivyoambavyo sasa vimezikumba nchi 150katika muda mfupi na kusababisha kupotea kwa idadi kubwa ya watu, hasara za kijamii, nchi na uchumi. Tunahitaji haraka hatua imara za hasa wakati huu. Tunahitaji kuchukua hatua sasa.”

Dkt. Singh ameelezea umuhimu wa juhudi za kuendelea na kubaini virusi, upimaji, matibabu na kuwatenga wagonjwa ikiwa ni pamoja na kuwafuatilia wote waliokutana na wagonjwa.

Watu pia wametakiwa kufuata ushauri wa WHO katika kupunguza maambukizi kupitia njia mbalimbali kama vile kunawa mikono ipasavyo, kuziba midomo wakati wa kukohoa na kupiga chafya na kujiepusha na mikusanyiko ya watu.