Tunaelekea nchini Uganda, kumulika mizozo ya kifamilia wakati huu wa mlipuko waCOVID-19na madhara yake. Mizozo ambayo inadaiwa kusababishwa na wanafamilia kukaa pamoja majumbani kwa muda mrefu kutokana na vizuizi vya kutembea vilivyowekwa na serikali ikiwa ni moja ya hatua za kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.
Umoja wa Mataifa umekuwa ukizungumzia visa na mikasa inayoripotiwa majumbani hivi sasa wakati familia zikisalia majumbani kuepuka kusambaa kwa virusi vya Corona. Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres alishapaza sauti akinukuu ripoti za wanawake na wasichana kuripoti katika vyombo vya usalama wakiomba msaada kutokana na ukatili wa kimwili na kifikra majumbani.
Ni katika kuthibitisha hayo, mwandishi wetu wa Uganda, John Kibego ametembelea wilaya ya Hoima ambako amezungumza na wakazi ambao wameelezea siyo tu ukatili wa majumbani bali pia mshtuko wa wanandoa kujikuta wanakaa kwa pamoja muda mrefu kuliko ilivyozoeleka na kuleta msuguano.
Badala ya raha ikageuka karaha, kulikoni?