51Թ

FAO endeleeni kutuimarisha - Wanawake Kakonko

Get monthly
e-newsletter

FAO endeleeni kutuimarisha - Wanawake Kakonko

UN News
29 May 2020
By: 
Wanawake wakulima wilayani Kakonko nchini Tanzania waliopokea mafunzo kuhusu mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
UN News/ Assumpta Massoi
Wanawake wakulima wilayani Kakonko nchini Tanzania waliopokea mafunzo kuhusu mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania wamesaidia wakulima hususan wilayaniKakonko mkoani Kigoma kupata mbinu bora za kilimo na kuondokana na kilimo cha mazoea na hatimaye waongeze mazao ili siyo tu kukabiliana na umaskini bali pia kutokomeza njaa.

Katika kata ya Katanga, wilaya yaKakonko, mkoani Kigoma, wanawake wa kikundi cha Umoja ni nguvu, wanapalilia shamba lao nyakati za asubuhi wakiwa na ari kubwa.

Wengine wanamwaga mbolea kwenye shamba hili la mahindi na maharagwe.

Shamba hili darasa ni matokeo ya mafunzo yaliyotolewa nakwa kushirikiana na serikali ya Tanzania. Salvasia Silivesta Barumbwa ni kiongozi wa kikundi hiki chenye wanachama 39.

(Sauti yaSalvasia Silivesta Barumbwa)

Je kanuni za kilimo bora zinafuatwa? Masumbuko William Masolwa ni Afisa kilimo,kata ya Katanga..

(Sauti ya Masumbuko William Masolwa)

Paskazia Kazibwa ni mkulima mwezeshaji wa kikundi na nilimuuliza nini kinawatia hamasa?

(Sauti ya Paskazia Kazibwa)

Na ujumbe wake kwa wanawake wengine ni upi?

(Sauti ya Paskazia Kazibwa)

Mradi umefikisha matokeo chanya hata kwa watoto wao, Paskazia ni shuhuda..

(Sauti ya Paskazia Kazibwa)

Tayari mahindi na maharagwe yameshavunwa na wakulima wanajiandaa kwa msimu ujao.