Ken Walibora Waliula alizaliwa mwaka 1964 katika kaunti ya Bungoma nchini Kenya, huku akifahamika na wengi kama mpenzi wa lugha ya Kiswahili na mtetezi mkubwa.
Mwenda zake Walibora alikuwa ni mwandishi wa riwaya, mashairi, mhadhiri na alivaa kofia nyingi.Mnamo Aprili 10, 2020, profesa Walibora alifariki dunia kufuatia ajali ya barabarani.
Mapema mwaka jana alizungumza na Grace Kaneiya wa idhaa hii ambapo katikamazungumzo ya kwa kina alinidokezea kuhusu kazi zake za sanaa na malengo yake kupitia kazi hizo.