51Թ

Mkutano wa G-20 UN yasisitiza mshikamano kukabili COVID-19

Get monthly
e-newsletter

Mkutano wa G-20 UN yasisitiza mshikamano kukabili COVID-19

UN News
27 March 2020
By: 
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa miongoni mwa washiriki wa mkutano wa G-20 kwa njia ya video
UN Photo/Evan Schneider
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa miongoni mwa washiriki wa mkutano wa G-20 kwa njia ya video

Katika mkutano huo ambao ulijikita na COVID-19 Guterres ametoa wito akisistiza kwamba“Hatua za pamoja za kimataifa zinahitajika ili kuweza kushinda vita dhidi ya virusi vya Corona na pia mshikamano na wale wasiojiweza ni muhimu.”

Kwenye mkutano wa mataifa 20 yaliyoendelea kiuchumi duniani au G-20 uliofanyika leo kwa njia ya video Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza mshikamano na hatua za pamoja katika vita dhidi ya virusi vya Corona, COVID-19.

Guterres ameuambia mkutano huo ulioandaliwa na Saudi Arabia ambaye ndiye rais wa sasa wa mzunguko wa G-20, kwamba janga hili la Corona linatishia binadamu wote.

Hadi kufikia leo watu walioambukiza virusi vya Corona duniani kote ni zaidi ya 480,000 na vifo Zaidi ya 21,000.

Mlipuko huo kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa umesababisha kuchukuliwa kwa hatua kali ambazo zimewaathiri Zaidi ya watu bilioni 3 kote duniani.

Guterres amesema “Tuko katika vita na virusi na kwa sasa hatuvishindi. Vita hivi vinahitaji mipango ya vita kukabiliana navyo”

Katibu Mkuu Antonio Guterres akishiriki kwa njia ya video mkutano wa G-20
Katibu Mkuu Antonio Guterres akishiriki kwa njia ya video mkutano wa G-20
UN Photo/Evan Schneider

Kinachojitajika kwa sasa

Kwa mujibu wa bwana Guterres “mshikamano ni muhimu sana“ ndani ya G-20 na nchi zinazoendelea hususan zilizoathirikana vita. Ili kukomesha haraka maambukizi ya COVID-19 mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kuna haja ya mkakati wa G-20 wa kuratibu hatua hizo ambao utaongozwa na shirika la afya duniani.

Ameongeza kuwa “Nchi zote lazima ziweze kuchanganya upimaji, kufuatilia visa, kufanya karantini na matibabu la pia vikwazo kwa watu kukusanyika ili kupunguza kusambaa kwa maambukizi ya virusi. Na lazima kuwe na mipango ya watu kutoka kuweza kuhakikisha maambukizi yanadhibitiwa hadi pale chanjo itakapopatikana. Na lazima tusake msaada wa lazima kuziongezea uwezo nchi zinazoendelea kupambana na ugonjwa huu.”

Uwekezaji wahitajika

Kuhusu athari za kijamii na kiuchumi za janga hilo la Corona , Guterres ametoa wito wa kuchukua hatua za pamoja ili kupunguza athari.“endapo kuhakikisha kuendelea kwa mfumo wa fedha duniani , mkazo lazima uweke Zaidi ya yote kwenye mtazamo wa kibinadamu. Tunahitaji kujikita na watu kuhakikisha wanaweza kuendesha nyumba zao na kamampuni ya biashara kuweza kulinda ajira.”

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu hili litahitaji hatua kubwa za kimataifa na kwa mantiki hiyo amecagiza na kukaribisha msaada wa kijamii na kiuchumi kwa nchi zilizoendelea kwa kupeleka moja kwa moja .“Lakini mpango wa kujikwamua kusaidia nchi zinazoendelea kwa lengo hilohilo nao pia unahitaji uwekezaji mkubwa. Na kwa hilo anafikiria ni muhimu kutenga fungu Zaidi kwa shirika la fedha duniani IMF na taasisi za fedha za kimataifa .”

Mkuu huyo wa Umoja wa Msataifa ametoa wito wa kuondoa vikwazo ambavyo vinaweza kuathiri uwezo wan chi kupambana na mlipuko huo wa Corona.

Na mwisho amesema “ni lazima kufanyakazi pamoja sasa kuandaa mazingira kwa ajili ya kujikwamua mbayo ambayo yatajenga uchumi jumuishi , endelevu na wenye usawa”,kwa kuzingatia malengo ya amendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa ifikapo 2030.