51Թ

Tumejizatiti kuepusha maambukizi ya COVID-19 -CCBRT

Get monthly
e-newsletter

Tumejizatiti kuepusha maambukizi ya COVID-19 -CCBRT

UN News
25 June 2020
By: 
Frederick Msegela, Meneja wa CCBRT nchini Tanzania wakati wa mahojiano na UNIC Dar es salaam nchini humo.
UN Tanzania
Frederick Msegela, Meneja wa CCBRT nchini Tanzania wakati wa mahojiano na UNIC Dar es salaam nchini humo.

Nchini Tanzania hospitali ya CCBRT imechukua hatua za uhakika kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu, wakiwemo wafanyakazi wake wanajikinga ipasavyo dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19.

Frederick Msegela, ,Meneja wa usuluhishi na uhamasishaji kuhusu ujumuishaji wa watu wenye ulemavu CCBRT akizungumza na kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC Dar es salaam nchini humo amesema hatua yao hiyo inazingatia kuwa takribani asilimia 6 ya wafanyakazi wake wana ulemavu na kwamba,

“Inapokuja kwa asiyeona, katika mazingira ya kazi kama haya ni lazima kumuelekeza ni wapi pa kunawa mikono na ile dawa inapatikana. Lakini pia kama kuna taarifa ambazo zinatolewa kwa njia ya maandishi, ni lazima kwake ziwe katika mfumo rafiki, yaani maandishi ya nukta nundu ili mtu asiyeona aweze kusoma, la sivyobasi ziwe katika mfumo wa sauti kama ambavyo inafanyika kwenye redio ili kumuelimisha mtu asiyeona ili aweze kupata hizo taarifa.”

Hata hivyo kutokana na mazingira ya kuwa na ulemavu kuongeza changamoto zaidi kwa watu wa kundi hilo katika kujikinga na virusi vya Corona, Bwana Msegela ana ombi kwa serikali ya Tanzania akisema kuwa,

“Kwenye majanga kama haya kuwa na mikakati ya makusudi inayolenga kusaidia watu wenye ulemavu. Inawezekana kuna mikakati ya kusaidia jamii kwa ujumla wake, lakini inapokuja kwa watu wenye ulemavu lazima kuwe na mikakati rafiki kwao, kinyume na hivyo, kundi hili litabakia kuwa wahanga na watakuwa katika mazingira magumu sana na kupata hivi virusi.”

Kwa sasa nchini Tanzania hakujaripotiwa tena maambukizi mapya ya COVID-19 ambapo vyuo vimefunguliwa pamoja na baadhi ya wanafunzi wamerejea shule, huku hali ya kawaida inarejea rasmi tarehe 29 mwezi huu wa Juni.