51³Ô¹Ï

Viwango vya joto na baridi mwezi Januari vilizidi kipimo- WMO

Get monthly
e-newsletter

Viwango vya joto na baridi mwezi Januari vilizidi kipimo- WMO

UN News
By: 
Manzari ya ofisi za Umoja wa Mataifa Geneva (UNOG) hali mbaya ya theluji ikitarajiwa. o1 Februari 2019. Picha: Daniel Johnson/UNOG
Picha: Daniel Johnson/UNOG. Manzari ya ofisi za Umoja wa Mataifa Geneva (UNOG) hali mbaya ya theluji ikitarajiwa. o1 Februari 2019
Picha: Daniel Johnson/UNOG. Manzari ya ofisi za Umoja wa Mataifa Geneva (UNOG) hali mbaya ya theluji ikitarajiwa. o1 Februari 2019

Shirika la hali ya hewa duniani, WMO limetoa tathmini ya mwenendo wa hali ya hewa katika maeneo mbalimbali ulimwenguni kwa mwezi uliopita wa Januari, tathmini ambayo inaonyesha madhara ya myoto ya nyika, mafuriko na mvua.

Tathmini hiyo inasema hali ya hewa ilikuwa ni ya kupindukia ikitolea mfano eneo la Amerika ya Kaskazini ambako limepata baridi kali kupindukia huku maeneo ya Australia yakipata kiwango cha juu zaidi cha joto na mvua kubwa huko Amerika ya Kusini ilhali theluji kali ilianguka kwenye milimaÌý ya Alps na Himalaya.

Katibu Mkuu wa WMO Petteri Taalas amesema “hewa nzito yenye baridi kali kutoka ncha ya kaskazini mwa dunia ilivurumaÌý hadi maeneo ya Amerika Kaskazini ikiambatana na upepo mkali ambapo shirika la hali ya hewa la Marekani limesema viwang vya joto vilikuwa vya chini sana kuliko kawaida, mathalani nyuzi joto hasi 53.9 katika kipimo cha selsiyasi tarehe 30 mwezi huu wa Januari.â€

Amesema kuwa hali ya hewa ya baridi kali kwenye maeneo ya mashariki mwa Marekani yanapatia msisitizo mabadiliko ya tabianchi akiongeza kuwa kwa ujumla, “kimataifa, kumekuwepo na kuporomoka kwa kiwango kipya cha baridi na ni matokeo ya ongezeko la joto duniani. Ni vyema kutofautisha kati ya hali ya hewa ya muda mfupi na tabianchi ya muda mrefu.â€

Kwa upande wa Afrika hususan maeneo ya kusini, WMO imesema kimbunga Desmond kilitua Msumbiji tarehe 22 mwezi uliopita wa Januari na kusababisha pepo Kali na mafuriko kwenye mji wa Beira pamoja na mvua huko Madagascar na Malawi.

WMO imesisitiza kuwa kinachoendelea sasa kwenye hali ya hewa si kitu kipya ijapokuwa tafiti zaidi zinafanyika kuweza kubaini ni kwa jinsi gani inaathiriwa na mabadiliko ya tabianchi.

Ìý