51Թ

COVID-19 na mabadiliko ya tabianchi vyahitaji ujasiri na utashi kuvishinda -UN

Get monthly
e-newsletter

COVID-19 na mabadiliko ya tabianchi vyahitaji ujasiri na utashi kuvishinda -UN

UN News
29 April 2020
By: 
Niger inakumbana na upungufu wa chakula na viwango vya mapato ya chini
WFP/Simon Pierre Diouf
Niger inakumbana na upungufu wa chakula na viwango vya mapato ya chini

Ili kukabiliana na janga la virusi vya corona auna tishio linguine linalonyemelea la mabadiliko ya tabianchi njia pekee ya kukabiliana nayo ni“ujasiri, maono na uongozi wa ushirikiano, ukijikita katika mshikamano wa kimataifaamesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakati wa majadiliano ya kimataifa hii leo yaliyojikita katika mabadiliko ya tabianchi.

Ili kukabiliana na janga la virusi vya corona au COVID-19 na tishio linguine linalonyemelea la mabadiliko ya tabianchi njia pekee ya kukabiliana nayo ni“ujasiri, maono na uongozi wa ushirikiano, ukijikita katika mshikamano wa kimataifaamesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakati wa majadiliano ya kimataifa hii leo yaliyojikita katika mabadiliko ya tabianchi.

Na wakati kukiwa na tishio kubwa la maisha ya watu , biashara kulemaa na uchumi kuharibika.Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameonya katika jmajadiliano hayo kwa njia ya mtandao yanayofanyika mjini Petersberg Berlin Ujerumani kwamba Malengo ya Maeendeleo endelevu SDGs pia yako katika tishio kubwa.

“Gharama kubwa ni kutofnya chochote” amesema Katibu Mkuu akitetea haja ya haraka ya kuimarisha na kupunguza gesi chafuzi ya viwandani kuweza kudhibiti ongezeko la joto duniani lisizidi nyuzi joto 1.5C kiwango ambacho ni cha juu kuliko ilivyokuwa kabla ya maendeleo ya viwanda kuweza kupmbana na mabadiliko ya tabianchi.”

Utashi wa kisiasa wahitajika

Akifurahishwa na teknolojia na maoni ya umma hususani ya vijana , amebaini kwamba miji mingi na biashara nyingi zinachukua hatua. Hata hivyo amesema“Lakini bado tunakosa utashi wa kisiasa ambao ni wa lazima , kuwa na hamasa na matamanio ya kukabili, kudhibiti na kufadhili.”

Katika kukabiliana na mabadiliko hayo Guterres amesema nchi zote ni lazima ziahidi katika kupunguza hewa ukaa ifikapo mwaka 2050. Na nchi zinazoendelea ambazo hazihusiki san ana mabadiliko ya tabianchi lakini ndizo zinazoathirika zaidi na athari zake amesema zinahitaji kujengewa mnepo na msaada .

Na hili amesema linahitaji ufadhili wa kutosha wa fedha kuanzia ahadi ya dol bilioni 100 kila mwaka kwa ajili ya kudhibiti na juhudi za mnepo wdhidi ya mabadiliko hayo ameongeza Bwana Guterres.

Kuna fursa ni kubwa

Katika mipango ya kujikwamua kutokana na janga la corona Katibu Mkuu amesema kuna fursa kubwa ya kuchaiza ulimwengu kufuata njia ambayo itakabiliana na mabadiliko ya tabianchi , kulinda mazingira, kubadili mwenendo wa kutoweka kwa bayoanuai na kuhakikisha afya ya muda mrefu na usalama wa binadamu.

"Kwa kufanya mabadiliko ya kuhamia kwenye kiwango kidogo cha hewa ukaa, kuongezeka kwa mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, tunaweza kuunda dunia safi, inayojali mazingira, salama, yenye haki na mafanikio Zaidi kwa wote.”Amesisitiza.

Kwa mantiki hiyo amependekeza hatua sit ana tofauti za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ambazo nchi zinaweza kuzichukua kujikwamua.

Hatua chanya za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

1. Kuunda ajira mpya na biashara kupitia mfumo unaojali mazingira nawa haki wakati wa kuharakisha upunguzaji wa hewa chafuzi katika nyanja zote za uchumi.

2. Kutumia pesa za walipa kodi kuunda ajira zinazojali mazingira na ukuaji wa pamoja wakati wa kuokoa biashara.

3. Kubadilisha uchumi kutoka kijivu hadi kijani, ukitumia ufadhili wa umma ambao hufanya jamii kuwa zenye mnepo zaidi.

4. Wekeza fedha za umma katika siku zijazo, kwa miradi inayosaidia mazingira na hali ya hewa.

5. Fikiria hatari na fursa kwa uchumi wako mwenyewe, wakati mfumo wa kifedha ya ulimwengu inafanya kazi ili kuunda sera na miundombinu.

6. Kufanya kazi pamoja kama jamii ya kimataifa kupambana na COVID-19 na mabadiliko yatabianchi.

Kama ilivyo janga la corona Guterres amesema gesi chafuzi ya viwandani haieshimu mipaka , na kujitenga ni mtego ambao hakuna nchi inayoweza kufanikiwa peke yake.

“Tayari tuna mfumo wa pamoja wa kuchukua hatua ambao ni ajenda ya 2030 kwa ajili ya maendeleo endelevu na mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi.Amekumbusha mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa.

Amesisitiza kuwabila mchango wa wachafuzi wa kubwa wa hali ya hewa , juhudi zetu zote zitakuwa hatarini, hebu tutumie mbinu za kujikwamua na janga hili kuweka msingi kwa ajili ya usalama, afya, ujumuishi na dunia yenye mnepo zaidi kwa ajili ya watu wote.”