Watoto 11 wamearifiwa kuuawa katika shambulio lililofanywa kwenye soko lililofurika umati wa watu mjini Afrin Kaskazini mwa Suria
Watoto 11 wamearifiwa kuuawa katika shambulio lililofanywa kwenye soko lililofurika umati wa watu mjini Afrin Kaskazini mwa Suria.
Kupitia taarifa iliyotolewa leo na Ted Chaiban mkurugenzi wa kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto” Ni jambo la kusikitisha kwamba Watoto 11 kuripotiwa kuuawa na wengine wengii kujeruhiwa wakati bomu liliporipuka karibu na gari la mafutakwenye soko lililojaa watu mjini Afrin Aleppo vijijini nchini Syria”
Mkurugenzi huyo amesema“tunahofia kwamba idadi ya vifo itaongezeka na huenda ni kubwa zaidi. Miaka 10 katika mzozo wa Syria Watoto wanaendelea kulipa gharama kubwa kutokana na kiwango cha machafuko, uharibifu na vifo. Na machafuko haya yanaendelea kuzua machafuko mengine.”
Ameongeza kuwa machafuko sio kitu kipya Afrin kwani mapema mwaka 2018kutokana na mapigano kushika kasi karibu Watoto 56,000 walilazimika kukimbia eneo hilona kwenda katika sehemu zingine za Syria.
Vita vya Syria havina dalili yoyote ya kumalizika hivyo UNICEF imezikumbusha pande zote katika mzozo na wale walio na ushawishi dhidi ya pande hizo kwamba Watoto sio walengwa na kwamba mashambulizi katika maeneo yaliyofurika rai ani ukiukwaji wa sharia za kimataifa.