51Թ

Afya ya binadamu inategemea afya ya sayari tunayoishi -Guterres

Get monthly
e-newsletter

Afya ya binadamu inategemea afya ya sayari tunayoishi -Guterres

UN News
19 June 2020
By: 
Msichana akipika katika moja ya vijiji nchini Ethiopia ambalo ardhi imeathirika vibaya na ukame unaoendelea
UNICEF/Tanya Bindra
Msichana akipika katika moja ya vijiji nchini Ethiopia ambalo ardhi imeathirika vibaya na ukame unaoendelea

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kukabiliana na ongezeko la jangwa na ukame duniani Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameisihi dunia kulinda ardhi ya sayari tunayoishi kwani afya ya binadamu inategemea afya ya sayari hiyo.

Kupitia ujumbe wake wa siku hii Guterres amesema leo hii dunia inateketea, mmomonyoko wa ardhi unawaathiri watu bilioni 3.2 na asilimia 70 ya ardhi ya dunianiimebadilishwa na shughuli zakibinadamu.

Katibu Mkuu amesema hali hii inaweza kubadilishwa na kuletasuluhisho ya changamotonyingi zinazoikabili dunia kuanziauhamiaji wa kulazimishwa,njaa hadi mabadiliko ya tabia nchi.

Katika eneo la Afrika la Sahel,amesema ukandamkubwa wa Kijani-Kibichi unabadilisha maisha na njia zawatukuishi kutoka SenegalhadiDjibouti na kuongeza kuwa "Kwa kurejesha katika ubora ekari milioni 100 za ardhi iliyoharibiwa, uhakika wa chakula unadumishwa, kaya zinahifadhiwa na ajira zimetengenezwa.Juhudi kama hizo zinarudisha bayoanuai, hupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi na kufanya jamii kuwa na mnepo zaidi.Kwa ujumla, faida zinazidi gharama mara kumi."

Pia katikakuadhimisha siku hii yakukabiliJangwa na Ukame,ametoawito wakuwa na mkataba mpya kwa ajili yamasuala yaasili

"Kupitia hatua ya kimataifa na mshikamano, tunaweza kuongeza urejeshwaji wa ardhi na suluhisholaasili kwa hatuaza kukabili mabadiliko ya tabianchina faida kwa vizazi vijavyo.Kwa kufanya hivyo, tunaweza kutekelezamalengo yamaendeleoendelevu nakuhakikishahakuna mtu atakayeachwa nyuma.”.

Siku ya kimataifa ya kukabiliana na ongezeko la jangwa na ukame huadhimishwa kila mwaka Juni 17.