51Թ

Buriani Balozi Mahiga mchango wako tutauenzi daima -Wanadiplomasia

Get monthly
e-newsletter

Buriani Balozi Mahiga mchango wako tutauenzi daima -Wanadiplomasia

UN News
5 May 2020
By: 
Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa UN nchini Somalia, Balozi Augustine Mahiga, (kushoto) akihutubia Baraza la Usalama kuhusu Somalia. (11 Mei 2011)
UN/Eskinder Debebe
Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa UN nchini Somalia, Balozi Augustine Mahiga, (kushoto) akihutubia Baraza la Usalama kuhusu Somalia. (11 Mei 2011)

Mwendazake Balozi Augustine Mahiga aliyeaga dunia mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Tanzania , ambaye alikuwa na mchango mkubwa kwa nchi yake na Umoja wa Mataifa alikuwa pia mchapakazi hodari na aliishi na kufanya kazi viruzi na watu mbalimbali.

Baada ya taarifa za msiba wake ambao bila shaka umeacha pengo lisilozibika Tanzania, jumuiya ya kimataifa imetuma salamu za rambirambi huku nchi wanachama wakisema mchango wake utamkumbukwa daima. Hapa makao Makuu ya Umoja wa Mataifa anayepokea salamu hizo ni Mwakilishi wa sasa wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Kennedy Gastorn.

"Msiba wa Mheshimiwa Balozi Dkt. Mahiga ni pigo kubwa sana kwa dunia nzima kwa jumla. Alikuwa ni mwanadiplomasia nguli na asiye na mashaka tumepokea salamu tele za rambirambi kutoka kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na mabalozi wengi wanaowakilisha nchi zao hapa Umoja wa Mataifa pamoja na wanadiplomasia wengi waliofanya kazi na marehemu wanamkumbuka sana uzoefu wake wakidiplomasia. Alikuwa pia ni mzalendo wa kweli mfano alipokuwa hapa kama mwakilishi wa wahudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa alifanya mambo mengi pamoja na kuimarisha idara ya kiswahili katika Umoja wa Mataifa. Pia alishiriki sana katika ushiriki wa Tanzania katika ulinzi wa amani duniani. Wakati Tanzania ilipokuwa bwembe sio kuhudumu katika baraza la usalama wa Umoja wa Mataifa. Alikuwa na ushawishi mkubwa katika maazimio mengi ikiwemo utatuzi a migogoro ya kisiasa hasa katika nchi za maziwa makuu pamoja na ujenzi wa amani,kiujumla,hapa Umoja wa Mataifa Marehemu alikuwa anaheshimika sana kutokana na uredi wake katika kazi zake akiwa pia mwakilishi maalum wakati huo mkuu wa Umoja wa Mataifa katika misheni ya Ulinzi wa amani nchini Somalia. Kama Rais wa Jamuhuri ya mgano wa Tanzania Mhesimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alivyomwelezea, Balozi Dkt.Mahiga alikuwa ni mtu wa watu,mpole na mnyenyekevu sana.Hapa Umoja wa Mataifa tunamlilia sana na tunaungana na watanzania walioko nchin za nje kutoa pole zetu kwa familia ya marehemu kwa rais wa muungano wa Tanzania mheshimiwa John Pombe Magufuli spika wa bunge mheshimiwa Job Ndugai,wabunge wamungano wa jamuhuri ya Tanzania,wizara ya sheria na wananchi wote kwa jumla.Tutamuenzi daima Bwana apokee marehemu Balozi katika ufalme wake Amina"