51Թ

Chuki na taarifa potofu vyatawala zama hizi za COVID-19 -Guterres

Get monthly
e-newsletter

Chuki na taarifa potofu vyatawala zama hizi za COVID-19 -Guterres

UN News
15 April 2020
By: 
Shirika la afya ulimwenguni, WHO linashirikiana na Facebook kukabiliana na kuenea kwa taarifa potofu kuhusu chanjo katika mitandao ya kijamii
UN Photo/Manuel Elias
Shirika la afya ulimwenguni, WHO linashirikiana na Facebook kukabiliana na kuenea kwa taarifa potofu kuhusu chanjo katika mitandao ya kijamii

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema wakati dunia ikipambana na janga la mlipuko waCOVIDI-19, changamoto kubwa kabisa kuwahi kuikabili dunia tangu vita vya pili vya dunia, kunashuhudiwa pia mlipuko mwingine wa hatari, ambao ni mlipuko wa taarifa potofu

Kupitia ujumbe wake alioutoa leo kupitia mtandao Guterres amesema“Duniani kote watu wanaogopa, wanataka kujua nini cha kufanya na wapi pa kukimbilia kupata ushauri.Huu ni wakati wa sayansi na mshikamano.Lakini bado mlipuko wa taarifa potofu unasambaa duniani kote.”

Ameongeza kuwa ushauri wa afya wenye madhara na nukuu za hatari kama mafuta ya nyoka vinazidi kuongezeka.

Taarifa za uongo imekuwa ndio wimbo

Katibu mkuu ameonya kwamba“Uongo ndio unaotawala hewani, nadharia potofu zimeghubika na kuathiri mtandao huku Chuki ikishika kasi, unyanyapaa na kuwanyanyasa watu na vikundi nako kunaongezeka.”

Amehimiza kwamba huu ni wakati ambapo dunia inapaswa kuungana dhidi ya ugonjwa huu wa taarifa potofu pia na kusema“Chanjo yake ni uaminifu, kwanza uaminifu katika sayansi.

Pia amewapongeza waandishi wa Habari na wengine ambao wanakagua ukweli wa mlima wa taarifa potofu na machapisho kwenye mitandao ya kijamii.

Wamiliki wanajibika pia

Bwana Guterres ameyageukiwa makampuni ya mitandao ya kijamii na kusema“yanapaswa kufanya juhudi zaidi kukata mizizi ya chuki na dhana potofu kuhusu COVID-19.Pili uaminifu katika taasisi zilizowekwa katika kuchukua hatua, kuwajibika, utawala na uongozi wenye msingi wa ushahidi.”

Na ametaka pia kuwe na imanimiongoni mwa watu akisemakuheshimiana na kudumisha haki za binadamu lazima kuwe ni dira yetu katika kukabilianana mgogoro huu.

"Kwa Pamoja hebu tuukane uongo na upuuzi uliotawala huko nje.”

Mkakati kukabili taarifa potofu

Leo hii Katibu mkuuametangaza mkakati mpya wa mawasiliano wa Umoja wa Mataifa ambao amesema utajaza mtandao kwa taarifa sahihi na sayansi huku ukikabiliana na ongezoko la taarifa potofu,ambazo ni sumu inayoweka maisha katika hatari zaidi.

“Kwa sababu ya Pamoja, kutumia ufahamu na ukweli tunaweza kuishinda COVID-19 na kujenga dunia yenye usawa, haki na mnepo.” Amehitimisha Bwana. Guterres.