51Թ

COVID-19: Zanzibar yachukua hatua kupunguza mlundikano magerezani

Get monthly
e-newsletter

COVID-19: Zanzibar yachukua hatua kupunguza mlundikano magerezani

UN News
27 March 2020
By: 
Mtazamo wa maeneo ya forodhani visiwani Zanzibar.
UN News/Assumpta Massoi
Mtazamo wa maeneo ya forodhani visiwani Zanzibar.

Idadi ya wagonjwa wa virusi vya Corona, huko visiwani Zanzibar nchini Tanzania ikiwa imefikia wagonjwa wawili, hii leo serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetangaza hatua za kuhakikisha sekta ya mahakama inaunga mkono hatua za kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona, COVID-19 ikiwemo kusitisha kwa muda usikilizaji wa kesi za madai na jinai. Omar Abdalla wa Televisheni washirika ZenjFMkutoka Zanzibar ametuandalia taarifa hii.

Hatua hizo zimetangazwa hii leo huko Vuga, Unguja na Mrajis Mkuu wa Mahakama Mohamed Ali Mohamed wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Jaji Mkuu wa Zanzibar akisema,"usikilizaji wakesi zote unasitizwa kwa muda wa siku thelathini kwanzia leo hadi tarehe ishirini na nne mwezi ujao.Kwa zile kesi ambazo ziko kwenye hatua ya kuwasilishwa mahakamani kwa hatia dharura na mawakilikuweza kwendelea kusikiliza kesi hizo basi wenye kesi hizo watawakilisha kwa maandishi. Pili mahakama itahudumia kesi za dharura tu na washtakiwa wenye kesi nzito za mauaji na zinginezomaombi ya dharura ya dhamana yanaweza yakatolewa muombaji na wakili wake au kwa ombi la dhamana wadhamini ndio watakao ruhusiwa kuingia katika mahakama"

Na kuhusu kesi zenye dhamana na kuepusha mrundikano kwenye vyuo vya mafunzo, Bwana Mohamed amesema,"tatu kwa makosa ya dhamana majagi na mahakimu ataweza kutoa dhamana kwa kesi zote ndogo ndogo ambazo zinahimili dhamana hizona kuepusha mrundikano kwenye vyuo vya mafunzo ambao wameshindwa kuondoa dhamana zao kwa ajili ya ukosefu wa fedha dhamana hizo zitaachiliwa wazi zitakua huru kuweza kutoka vyoo vya mafunzo. Nne katika kipindi hichi watendaji wote wa mahakama wataendelea kuwepo kazini hata hivyo kumbi za mahakama hazitatumika majagi na mahukumu wenye hukumu zao bado wataendelea kutoa hukumu hizo kama kawaida na kuweza kuzitoa katika mahakama zetu. Swala la ndugu zetu walioko kwenye chuo cha mafunzo bado uratibu unaendelea kwenda kushughulikiwa kwa kuweza kuharisha mashauri yao yote kwa wale ambao wako rumande na wale ambao wana dhamana katika mahakama kuu.Usikilizaji wa kesi zote unasitizwa kwa muda wa siku thelathini kuanzia leo hadi tarehe ishirini na nne mwezi ujao.Kwa zile kesi ambazo ziko kwenye hatua ya kuwasilishwa mahakamani kwa hatia dharura na mawakilikuweza kuendelea kusikiliza kesi hizo basi wenye kesi hizo watawakilisha kwa maandishi."

Amesema ingawa Zanzibar bado haina mfumo wa kuendesha kesi kwa njia ya video, bado wanachukua hatua kuweza kuona jinsi gani wanapunguza mrundikano gerezani na rumande.

Hadi hivi sasa Zanzibar ambayo inaunda Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, ina mgonjwa mmoja tu wa virusi vya Corona ilihali Tanzania Bara wamethibitishwa wagonjwa 13 hadi leo Alhamisi.