51Թ

Katiba ya Umoja wa Mataifa leo imetimiza miaka 75

Get monthly
e-newsletter

Katiba ya Umoja wa Mataifa leo imetimiza miaka 75

UN News
29 June 2020
By: 
Peter Thomson Rais wa kikao cha 71 cha Baraza Kuu akiwa ameshikilia katiba ya Umoja wa Mataifa
UN Photo/Amanda Voisard
Peter Thomson Rais wa kikao cha 71 cha Baraza Kuu akiwa ameshikilia katiba ya Umoja wa Mataifa

Katiba ya Umoja wa Mataifa ambayo ilipitishwa na kutiwa Saini 26 Juni 1945 mjini San Francisco nchini Marekani na mataifa 50, leo inasherehekea miaka 75.

Kativba hiyo ilitiwa saini Juni 26 mwaka 1945 wakati wa kukunja jamvi la mkutano wa kimataifa kwa ajili ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa na ikaanza kutumika rasmi 24 Oktoba mwaka 1945, huku mkataba wa mahakama ya kimataifa ya haki ICJ moja ya nguzo sita kuu za Umoja wa Mataifa ikiwa sehemu ya katiba hiyo. Na tarehe hiyo 24 Oktoba 1945 ndio siku Umoja wa Mataifa ulipoanza rasmi.

Mwongozo wetu ni katika ya UN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wako kwenye maadhimisho hayo yaliyofanyika kwa njia ya mtandao amesema maadhimisho hayo ya miaka 75 ya katiba ya Umoja wa Mataifa yanafanyika katika wakati mgumu ambapo dunia nzima inapambana na athari za janga la corona au COVID-19 lakini pia“Watu kila mahali wanapigania haki na kupaza suati zao dhidi ya ubaguzi wa rangi. Kutambua tatizo huo ni mwanzo lakini tunahitaji kuja pamoja kuyatatua matatizo hayo. Kukabiliana na changamoto zetu za pamoja na kuyumba kwa dunia yetu tuna mwongozo ambao si mwingine bali katika ya Umoja wa Mataifa.”

Ameongeza kuwa ingawa katiba ya Umoja wa Mataifa ilitiwa Saini miaka 75 iliyopita misingi yake bado inasimamia ukweli uleule hadi leo ambao ni“Imani katika missing ya haki za binadamu, haki sawa kwa wanaume na wanawake, katika utu na kuthamini watu, sharia za kimataifa na kutatua mizozo kwa njia ya amani, na mazingira bora ya maisha kukiwa na uhuru mkubwa, maadali haya yasiyopitwa na wakati ynatatuongoza katika mustakabali mpya.”

Katika kumbukumbu hiyo ya miaka 75 , Umoja wa Mataifa umezindua mjadala wa matarajio ya watu kote duniani katika ujenzi wa mustakabali bora kwa wote.

“Mustakabali ambao utasitisha uharibifu wa mazingira na kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi,ambao tutakataa ubaguzi na kusherehekea tofauti zetu za kibinadamu, mustakabali ambao vijana watashika usukani , mitaani, mashuleni na katika jamii.”

Guterres ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa ulianzishwa kabla ya dharura ya vitisho vipya kama vile uhalifu na kauali za chuki mtandaoni.“Lakini katiba yetu inatuonyesha njia ambayo itaturuhusu kukabiliana na changamoto hizi.”

Pia ametoa wito wa kufanya ujenzi wa amani, utimizaji wa haki za binadamu na haki kwa wote kuwa sio ndoto tena kwa kushikama kwa pamoja.

Heko kwa waliotia Saini katiba ya UN

Naye Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Tijani Muhammad-Bande anayeongoza chombo kinachojumuisha wanachama wote katika maadhimisho hayo amewapongeza wote walioshika kalamu na kutia saini katiba hiyo ya Umoja wa Mataifa miaka 75 iliyopita, ambao walithubutu kutafakari dunia bora iliyotawaliwa na amani na usawa.

Ameongeza kuwa “tunapata nguvu kutoka kwa waliotutangulia wakati huu tukikabiliwa na hali ya taharuki.”

Kwa Rais huyo wa Baraza Kuu, kutiwa Saini kwa katika ya umoja wa Mataifa miaka 75 iliyopita kumewezesha“Kuundwa kwa shirika la kimataifa lenye misingi ya usawa na uhalali ambapo maisha ya dunia mpya yanatokana na misingi ya kanuni. Umoja wa Mataifa ulianzishwa ili kuokoa vizazi vijavyo kutokana na zahma za vita.”

Amekumbusha kwambaRobo tatu ya karne iliyoopita wasio na Imani walihoji dhamira ya wanachama wa Umoja wa Mataifa, lakini shuku na shaka hazikufua dafu wakati huo na hazitoweza sasa. Kwani sisi watu daina tutasalia kuwa Umoja wa Mataifa tukiongozwa na misingi ya katiba yetu.”