Utesaji ni ukatili mbaya sana wa haki za binadamu amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio guterres hii le ikiwa ni siku ya kimataifa ya kuwaunga mkono waathirika wa utesaji.
Ameongeza kuwa “Ingawa sharia za kimataifa zinapiga matufuku utesaji katika mazingira yoyote yale , bila kujali hilo ukatili huo unaendelea kutekelezwa katika nchi nyingi na hata katika nchi ambazo utesaji ni kosa la jinai.”
Utesaji unalenga kumdhalilisha muathirika wa uhalifu huo na kumpora mtu utu wake.
Hakuna kinachouhalalisha
Wasiwasi kuhusu kulinda usalama wa taifa na mipaka vinaendelea kutumika kuruhusu utesaji na mifumo mingine ya ukatili, udhalilishaji na unyanyasaji.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu athari zake huenda mbali zaidi ya kitendo cha kumtenga mtu binafsi bali hurithishwa kwa vizazi na vizazi na hivyo kusababisha mzunguko wa machafuko.
Na tangu mwanzo Umoja wa Mataifa umekuwa ukilaani uhalifu huo kama moja ya ukatili mbaya kutukelezwa na binadamu dhidi ya binadamu mwenzake. Hivyo amesisitiza “Katika siku hii ya kimataifa ya kuwaunga mkono waathirika wa utesaji , watetezi wa haki za binadamu na manusura wa utesaji kote duniani chukueni fursa hii kupaza sauti dhidi ya utesaji kitendo kibaya zaidi ya kumnyima binadamu utu na pia wakumbukeni na kuwaunga mkono waathirika.”
Hauna misingi ya kisheria
Utesaji umepigwa marufuku chini ya vyombo vyote vya kisheri na hauwezi kuhalalishwa katika mazingira yoyote yale. Kupingwa kwake kulianzisha baadhi ya kanuni katika sharia za kimataifa ikimaanisha kwamba kila nchi mwanachama anabanwa kisheria bila kujali kwamba nchi hiyo imeridhia mikataba ya kimataifa ambayo inapinga utesaji ama la kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Zaidi ya hayo Umoja wa Mataifa unasema mfumo wa utesaji au kusambaa kwa vitendo vya utesaji ni uhalifu dhidi ya ubinadamu chini ya sharia za kimataifa.
“Utesaji unaondoa utu wa kila mtu na kila kitu unachokigusa ikiwemo wa watesaji, mfumo na matifa unakotendeka. Watesaji haupaswi kuruhusiwa kamwe kukwepa sharia na uhalifu wao na mifumo ambayo inaruhusuutesajilazima isambaratishwe au kubadilishwa”amesema mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Kujikwamua na jinamizi hilo
Ili kuweza kuondoka kwenye athari za jinamizi hilo na kupona waathirika wa utesaji wanahitaji program malum na za haraka. “Waathirika, manusura na familia zao lazima wawezeshwe na kusaidia kusaka haki kwa ajili ya yaliyowasibu.”
Mfuko wa hiayari wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya waathirika wa utesaji hutoa fedha kuwasaidia waathirika na familia zao kwa kutoa mamia ya ufadhili kwa mashirika ya kijamii duniani kote kwa ajili ya huduma za matibabu, kisaikolojia, kisheria, kijamii na msaada mwingine.
Kwa mujibu wa Umoja wa Msataifa mfuko huo pia unachangia katika huduma ya kuwasaidia waathirika kurejea katika Maisha ya kawaida, kurejeshwa makwao, kuwawezesha na kuwapa fursa za matibabu karibu manusura 50,000 kila mwaka.
“Kwa upande huo naupongeza mfuko wa hiyari wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya waathirika wa utesaji na natoa wito wa kuutunisha zaidi” ameongeza Katibu Mkuu na kuhitimisha kwamba
Siku hii maalum inatoa fursa kwa kila mtukila mahali kwa Pamoja kuunga mkono maelfu ya watu kote duniani ambao wameteswa na ambao bado wanateswa leo hii.“Katika siku hii ya kimataifa hebu tuwaenzi waathirika wa utesaji na kujitoa kufanya kazi ya kufiki dunia ambayo utesaji hautokei.”