51Թ

Mtoto kiziwi alazimika kuosha magari jijini Kinshasa ili alee familia yake

Get monthly
e-newsletter

Mtoto kiziwi alazimika kuosha magari jijini Kinshasa ili alee familia yake

UN News
29 May 2020
By: 
Mtoto Steve Okito mwenye umri wa miaka 14, ni kiziwi na anatoa ushuhuda jinsi janga la Corona lilivyoathiri masomo yake na familia yake.
UNICEF VIDEO
Mtoto Steve Okito mwenye umri wa miaka 14, ni kiziwi na anatoa ushuhuda jinsi janga la Corona lilivyoathiri masomo yake na familia yake.

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, athari za janga la virusi vya Corona auCOVID-19zimekuwa mbayá zaidi kwa watoto wenye ulemavu, ambapo mtoto mmoja mkazi wa mji mkuu Kinshasa, ambaye nikiziwi, amelazimika kusaka mbinu za kuweza kupata kipato ili kusaidia familia yake.

Mtoto huyo, Steve Okito mwenye umri wa miaka 14, anaishi jijini kinshasa na mama yake na wadogo zake watatu wa kiume. Yeye ni mwanafunzi wa darasa la 7, lakini sasa hawezi tena kwenda shule.

Katika mfululizo wa video za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto,zinazolenga kupaza sauti za vijana, Steve anaonekana akizungumza kwa lugha ya alama na anasema kuwa“shule zimefungwa kwa sababu ya janga la virusi vya Corona. Siwezi tena kuwaona marafiki zangu.”

Mtoto huyu anatoka familia maskini, na mama yake amepooza kwa hiyo analazimika kusaka kazi na kile afanyacho ni kusafisha magari jijini Kinshasa ili apate ujira.

Steve anasema kuwa,“sasa hivi naosha magari kwa sababu shule imefungwa. Kila kitu kimefungwa na ninalazimika kupata fedha ili nisaidie familia yangu. Fedha nampatia mama yangu. Hapa kwa mfano nimeosha hili gari na nimepata faranga 3000 sawa na dola 2. Lakini inategemea na mmiliki, wakati mwingine naweza kupata malipo ya juu zaidi.”

Ujio wa janga la Corona umefanya maisha ya Steve kuwa magumu zaidi kwa sababu hali ni ngumu zaidi kwa yeye kupata fedha akisema kuwa,“kabla ya Corona, magari ya kuosha yalikuwa ni mengi, lakini sasa kila kitu kimefungwa, hakuna mtu anayewasha gari kwenda kutembelea rafiki au kuzunguka tu.”

Matarajio ya Steve ni kuwa shule zitafunguliwa ili aweze kuwaona tena rafiki zake,shule zimefungwa kwa sababu yaCOVID-19.

Hata hivyo Wizara ya afya ya DRC, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na wadau wanaendelea kushirikiana ili kuwepo kwa wafanyakazi wa kuwapatia watoto kama Steve msaada wa kisaikolojia ili waweze kuhimili madhara ya muda mfupi na muda mrefu ya janga la COVID-19.