Radio Miraya inayoendeshwa na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMIS imekuwa chombo muhimu cha kuhakikisha wanafunzi wanaendelea kupata elimu kupitia vipindi vya redio wakati huu shule zikiwa zimefungwa kutokana na janga laCOVID-19nchini.
Katika studio za Redio hiyo zilizoko mjini Juba waalimu wa masomo mbalimbali wakijiandaa kupeperusha vipindi ambavyo ndio njia pekee kwa sasa ya kuhakikisha maelfu ya watoto wanaosalia majumbani kujikinga na corona wanaendelea kusoma
Urushwaji wa vipindi hivyo umeandaliwa kwa ushirikiano wa wizara ya elimu ya Sudan Kusini na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watotona kisha kurushwa bure na Redio hiyo ya. Mkuu wa UNMISS ni David Shearer.
“Hii ni fursa moja ambayo watoto wanaendelea kuwa na hamasa ya kusoma, injumuisha familia pia kwa sababu kila mtu atasikiliza kipindi hivyo ingawa shue zimefungwa , watoto wanaweza kuendelea kusoma na kuendelea na utaratibu wa shule na hamasa ya masomo.
Waziri wa elimu wa nchi hiyo Awut Deng Aculi anasema wametumia redio kwa kuwa inafika mbali na wengi wanaweza kumudu kwani
"Mfumo wa elimu umeathirika sana, tunaamini kwamba baada ya kufunga shule ilikuwa muhimu kuendelea na masomo na hii imekuwa fursa kwa watoto kuendelea kusoma wakiwa nyumbani”
Kwa mwalimu wa shule ya msingi Alfred Anasi Dominic kutumia Redio ni fursa ya kipekee kwa wanafunzi wake
"Nimefurahi sana kwamba tunarusha vipindi kupitia Radio Miraya kwa sababu inafikia wasikilizaji wengi nchini mwetu. Kila jimbo unakokwenda Radio Miraya inatangaza. Naamini kwamba , wasikilizaji wetu , watu wetu watafaidika sana na vipindi hivi"
Vipindi hivyo vya masomo vinarushwa mara mbili kwa siku kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa na mbali ya kurusha vipindi vya shule radio Miraya imejiolea kurusha matangazo ya kuelimisha jamii kutwa nzima kuhusu kujikinga na virusi vya corona.