51Թ

Somalia inahitaji msaada wa kibinadamu wakati watu milioni 4.1 wakikabiliwa na kutokuwa na uhakika wa chakula

Get monthly
e-newsletter

Somalia inahitaji msaada wa kibinadamu wakati watu milioni 4.1 wakikabiliwa na kutokuwa na uhakika wa chakula

UN News
6 February 2020
By: 
Mama akinunua samaki wa mkebe kwa vocha cha WFP Burao, Kaskazini mwa Somalia.
WFP/C. McDonough
Mama akinunua samaki wa mkebe kwa vocha cha WFP Burao, Kaskazini mwa Somalia.

Umoja wa Mataifa na mamlaka nchini Somali wametoa ombi la dharura kwa ajili ya msaada wa kibinadamu kukabiliana nahali yakutokuwa na uhakikawa chakula unaokabili mamilioni ya watu nchini humo.

Kwa mujibu wa tathmini chini ya usimamizi wa shirika la chakula na kilimo duniani, takriban watu miilioni 1.3 nchini Somalia wanakabiliwa na uhaba wa chakula na wanahitaji msaada wa dharura wa kibinadamu wakati huu ambao watoto 690,000 walio chini ya umri wa miaka mitano huenda wakaugua utapiamlo uliokithiri kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Mratibu wa misaada ya kibinadamu nhini Somalia,Adam Abdelmoula, amesema licha ya mvua za mwezi Januari na Februari zilizoimarisha uhakika wa chakula lakini.

(Sauti ya Adam)

“Takriban watu milioni 4.1 nchini Somalia wataendelea kukabiliwana kutokuwa nauhakika wa chakula kufikia katikati mwa mwaka 2020 ikiwemo watu milioni 1.3 walio na mahitaji ya dharura. Zaidi ya watoto 962,000 wanakabiliwa na utapiamlo uliokithiri, ikiwemo watoto 162,000 ambao huenda wakapataunyafuzimwaka huu iwapo mahitaji yao hayatashughulikiwa.”

Kwa upande wake naibu waziri wa kilimo na umwagiliaji, Hamoud Ali Hassan, amesema changamoto ya kibinadamu inayokabili nchi yake ni zaidi ya hali ya hewa akisema,

(Sauti ya Ali)

“Changamoto nchini Somali si tu kwa sababu ya ukosefu wa mvua. Ni kwa sababu ya ukosefu wa miundombinu, ambayo inaathiri usafiri wa watu kutoka jimbo moja hadijingine.Ukosefu wa usalama ni moja ya sababu.”

FAO imesema Somalia inakabiliwa na changamoto mseto ikiwemo pia uvamizi wa nzige ambao huenda ukaathiri mazao na malisho ya mifugo.

Shirika hilo limeongezakwamba juhudi za pamoja zinahitajika kukabilia na hali ya sasa.