Ujerumani na Ufaransa leo zimesisitiza uungaji mkono wa kisiasa na kifedha kwa shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO wakati huu ambapo janga la virusi vya Corona au COVID-19, limeendelea kutikisa ulimwengu.
Msimamo wa mataifa hayo mawili ya Ulaya umetolewa leo mjini Geneva, Uswsi na mawaziri wao wa afya, Jens Spahn wa Ujerumani na Olivier Veran wa Ufaransa.
Wawili hao walikuwepo nchini Uswisi kwa mazungumzo na maafisa wa ambapo baadaye walizungumza na waandishi wa habari, na Bwana Verana amesema kuw,a “Ufaransa ina imani na uwezo wa WHO wa kushughulikia changamoto za kiafya zinazoibuka na kufanya tathmini ya kazi hiyo ili kupata matokeo mazuri.”
Amesema kuwa Ufaransa inaimarisha mchango wake wa kifedha kwa WHO na kwamba “Rais Emmanuel Macron ametanganza nyongeza ya mchango wa dola zaidi ya milioni 50, kando ya gharama za uendeshaji ambazo Ufaransa huwa inachangia.”
Bwana Veran amesema kuwa zama hizi ambapo maabara nyingi duniani kote zinafanya kazi ya utafiti na maendeleo, chanjo ya kwanza itapatikana miezi ijayo “na Ufaransa inasisitiza kuwa chanjo hiyo lazima iweze kupatikana kwa watu wote, yaani wale wanaoweza kulipa na wasio na uwezo wa kulipa.”
Kwa upande wake, Bwana Spahn amesema, “Ujerumani itatekeleza wajibu wake ili kuipatia WHO uungwaji mkono wa kifedha, kisiasa na kiufundi ambao inahitaji. Hii inatokana na matarajio ya dhati kuwa changamoto zilizobakia zinashughulikiwa ipasavyo na marekebisho yanayotakiwa yanafanyika haraka ili kuongeza uwezo wa wa programu ya dharura ya WHO na vile vile WHO ifanye kaiz yake chini ya kanuni za kimataifa za afya.”
Amegusia kwamba, Wizara ya Afya ya Ujerumani, “itatoa zaidi ya euro milioni 500, kwa WHO mwaka huu pekee. Hiki ni kiwango cha juu zaidi kuwahi kuchangiwa na Ujerumani kwa WHO katika mwaka mmoja.”
Tangazo la Ujerumani na Ufaransa limekuja zaidi ya kuwa iansitisha ufadhili wake kwa WHO.