51Թ

Tunawalinda wanafunzi na wafanyakazi dhidi ya COVID-19 hapa SJMC-UDSM

Get monthly
e-newsletter

Tunawalinda wanafunzi na wafanyakazi dhidi ya COVID-19 hapa SJMC-UDSM

UN News
16 June 2020
By: 
Mradi wa sehemu ya kunawa mikono kwa ufadhili wa Mo Dewj Foundation nchini Tanzania.
UN News/ UN Tanzania
Mradi wa sehemu ya kunawa mikono kwa ufadhili wa Mo Dewj Foundation nchini Tanzania.

Nchini Tanzania wanafunzi wakiwa wamerejea vyuoni baada ya serikali kutangaza kufungua vyuo kutokana na hatua iliyopigwa katika mapambano dhidi ya virusi vya corona au COVID-19, Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma SJMC ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, UDSM, imeonesha juhudi ilizozichukua ilikuzuia kusambaa kwa maambukizi ya COVID-19.

Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma SJMC ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam imeonesha juhudi ilizozichukua ili kuwalinda wanafunzi na wafanyakazi kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu wa kujikinga na virusi hivi ambavyo tayari vimesababisha vifo vilivyothibitishwa zaidi ya laki 4 kote duniani. Dkt Kamfipo Gideon Mwakitalu anaeleza hatua walizochukua chuoni hapo

"Kimsingi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimetii maelekezo yote yakitaalamu kuhusiana na namna ya kuwakinga wanafunzi na wafanyakazi wake dhidi ya COVID-19. Unapoingia hapa chuoni unakutana na matenki ambayo yamewekwa maji na sabuni ambayo yanaruhusu mtu kunawa kabla hajaingia ndani, na hanawi kwa kushika koki,kuna maandalizi yamefanyika unakanyaga kwa sabuni na maji unanawa na kuingia lakini kabla ya kuingia vyumbani ukifika pale nje unapokelewa na vitakasa mikono vilivyoko ukutani.Hali iko vivyo hivyo hata maktaba lakini pia hata unapoelekea kwenye vyumba vyetu, tumeweka haya matenki ya kutosha.Kwa hivyo unapotoka darasa la kwanza kwenda lingine kuna matenki na mwanafunzi au mtumishi yeyote anayetoka darasa moja kwenda lingine ananawa."

Dkt Mwakitalu anaongeza

"Zaidi ya hapo tumekuwa tukizingatia zaidi namna ya ukaaji wa madarasani, sasa hivi ukienda darasani utapata wanafunzi wamekaa kwa nafasi na wameachiana nafasi yote hii ni katika kuhakikisha tunatii maelekezo tunayopewa na wizara husika lakini pia na uongozi mkuu wa chuo. Lakini zaidi ya yote tuna vifaa tunavyovaa usoni kama hivi unavyoviona kwa wanafunzi na watumishi. Maelezo ambayo tunatoa pale getini ni kwamba mtu ambaye hajavaa haruhusiwi kuingia kwa sababu miongoni mwa ushauri tuliopewa ni uvaazi wa hizi barakoa. Kwa hivyo ukiweza kuangalia miongozo ambayo tumeelekezwa hata kukaa kwa umbali unaohitajika tumezingatia pia unawaji wa mikono kwa maji yanayotiririka matenki yapo ya kutosha,na kila sehemu unayaona na kuwepo kwa vitakasa mikono pia tunavyo na kadhalika kwa hivyo wastani ni kwamba tumejaribu kutimiza yale yote ambayo tumeelekezwa kuyafanya kwa kipindi hiki.