51Թ

UN yawajulisha nchi wanachama kuhusu mapambano dhidi ya COVID-19

Get monthly
e-newsletter

UN yawajulisha nchi wanachama kuhusu mapambano dhidi ya COVID-19

UN News
30 March 2020
By: 
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Tijjani Muhammad-Bande ashiriki mkutano kwa njia ya mtandao wa wanachama wa UN kuhusu virusi vya corona.
51Թ/Reem Abaza
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Tijjani Muhammad-Bande ashiriki mkutano kwa njia ya mtandao wa wanachama wa UN kuhusu virusi vya corona.

Katika mkutano maalum kupitia njia ya mtandao uliofanyika leo Katibu Mkuu wa moja wa Mataifa, Rais wa Baraza Kuu la Umoja huo, Baraza la Usalama na baraza la kiuchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC wamezijulisha nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu juhudi za Umoja huo katika kupambana na virusi vipya vya Corona,COVID-19na kuendelea na kazi muhimu ya shirika hilo duniani kote.

Mbali ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wengine walioshiriki mkutano huo ulioendeshwa msaidizi wa Katibu Mkuu wa idara ya mawasiliano ya kimataifa Melissa Fleming ni Rais wa Baraza Kuu Tijjani Muhammad-Bande, Rais wa Baraza la Usalama Zhang Jun, na Rais wa Baraza la kiuchumi na kijamii ECOSOC , Mona Juul.

Inawezekana kuvishinda virusi vya Corona

Rais wa Baraza Kuu alianza kwa kusema “Umoja wa Mataifa uko katika fursa nzuri ya kuongozaa juhudi za kimataifa za kukabiliana na janga hili na umekuwa ukifanya hivyo tangu kuzuka kwa changamoto hii.”

Kwa mujibu wa Bwana Bande shirika la afya la Umoja wa Mataifalimekuwa likitoa taarifa za za kuaminika na kusisistiza kila wakati kwamba inawezekana kulishinda gonjwa hili.

Amekumbusha kwamba mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu mwezi septemba mwaka jana ulijikita na suala la afya na kwa mujibu wake “Jamii kote duniani hivi sasa zinaishi katika zama za changamoto kubwa na janga hili la virusi vipya vya Corona ni kumbusho kwamba ubinadamu wetu uko salama kama makundi yasiyojiweza yatakuwa salama.”

Usalama

Kwa upande wake rais wa Baraza la Usalama amesema hali ya sasa inaleta changamoto kubwa katika operesheni za Baraza hilo. Rais huyo ambaye ni balozi wa China kwenye umoja wa Mataifa amewajulisha nchi wanachama kwamba wameanza kufanya mikutano kupitia mtandao wiki hii na kwamba wakati huu wanaendelea kujifuna ni vipi wanaweza kupigia kura maazimio mbalimbali.

Ameongeza kwamba katika wiki mbili zilizopita maafikiano yamefikiwa juu ya suluhu ya muda kuhusu mpango wa Umoja wa Mataifa Somalia, UNSOM, mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika kulinda amani Darfur UNAMID, na usalama wa walindamani. Balozi huyo amesema anaamini kwamba shughuli ya kupiga kura za maazimio mbalimbali inapaswa kuanza hivi karibuni.

Ameongeza kuwa wiki iliyopita Baraza la Usalama lilitoa taarifa kuhusu Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, Afghanistan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, na Libya na wiki ijayo litajadili hali nchini Syria na Afghanistan.

Rais wa Baraza la kiuchumi na Kijamii ECOSOC Juul Mona ambaye pia ni mwakilishi wa kudumu wa Norway kwenye umoja wa Mataifa
Rais wa Baraza la kiuchumi na Kijamii ECOSOC Juul Mona ambaye pia ni mwakilishi wa kudumu wa Norway kwenye umoja wa Mataifa
UN Photo/Loey Felipe

Uchumi

Rais wa Baraza la uchumi na kijamii ECOSOC , Moja Juul akichangia katika mkutano huo amesema“Hatua za maendeleo zilizopigwa mwaka jana ziko hatarini kutoana na mgogoro wa sasa wa COVID-19.”

Ameongeza kuwa“ingawa athari za janga hilo zinamgusa kila mtu madhara yake yatakuwa makubwa zaidi kwa nchi zisizojiweza husuan zenye maendeleo duni.”

Juul amesema kwamba kuendelea kutokuwepo usawa katika masuala ya kijamii na kiuchumi kunaongezwa na janga hili la kimataifa. Na kwamba wale waliosalia nyuma ndio watakaokuwa na mzigo mkubwa zaidi . pia amesema mgogoro wa sasa unawaathiri wanawake na wanaume kwa hai tofauti hivyo suluhu lazima ishughulikie pia pengo la usawa wa kijinsia.”

Kwa mkuu huyo wa ECOSOC janga hili “linadhihirisha kwamba hatua za kulikabili zinahitaji mtazamo wa jamii nzima ikiwemo serikali za kitaifa na mashinani, sekta binafsi, jumuiya ya wnasayansi, asasi za kiraia na vijana.”

Hatua za kuchukua

Na hatimaye Katibu Mkuu Antonio Guterres amesema kwamba Umoja wa Mataifa “unachukua hatua zote zinazowezekana na kwamba kazi muhimu ya Umoja huo inaendelea kwa kiasi kikubwa bila bughudha.”

Amefafanua kwamba kwenye makao makuu mjini New York asilimia kubwa ya wafanyakazi wanafania kazi nyumbani , na safari zisizo za lazima na za muhimu sana zimeshauriwa kutofanyika, ziara za umma kwa UN zimesitishwa na mikutano ambayo si ya lazima imefutwa.

Pia amesema“wavuti maalum umezinduliwa ili kuhakikisha umma unapata taarifa kwa saa 24.”

Guterres ameongeza kuwa wiki iliyopita alizungumza na wawakilishi wa vitengo vyote vya huduma, kamesheni za kiuchumi za kikanda, waratibu wakazi na wawakilishi maalum katika operesheni za ulinzi wa amani na masuala ya kisiasa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres atoa wito kwa ajili ya kupambana na COVID-19
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres atoa wito kwa ajili ya kupambana na COVID-19
UN News/Daniel Dickinson

Katibu Mkuu ana masuala matatu ya ujumbe kwa wawakilishi hawa : “chukua kila tahadhari kulinda timu, hakikisha kwamba kazi muhimu zinaendelea na shirikiana na serikali kusaidia juhudi zao.”

Mapema mwezi februari Umoja wa Msataifa ulianzisha timu ya kudhibiti migogorochini ya usimamizi wa shirika la afya duniani WHO. Wiki iliyopita asilimia 93 ya timu za kitaifa za Umoja wa Mataifa ziliarifu kujihusisha na mamlaka za serikali katika maandalizi na mipango ya kukabiliana na janga hili.

Amesema umoja wa Mataifa pia unafanya mikutano kwa njia ya mtandao kila wiki na waratibu 129 ili kuwpa msaada wa kisiasa na kuendesha operesheni zao. Wachumi wengi wanashirikiana na tumen a timu za umoja wa Mataifa kutathimini athari za kiuchumi na kijamii za mlipuko huu.

Wiki ijayo Guterres amesema atachapisha ripoti kuhimiza wito wa mshikamano wa kimataifa ikiwemo mwelekeo wa umoja wa Mataifa katika kupambana na janga hili.

Na katika kusaidia operesheni za ulinzi wa amani na operesheni za kisiasa Guterres amesema kundi la msaada mashinani linaandaa suluhu mbalimbali.Timu za kitabibu zimetathimini uwezo wan chi ikiwemo upatikanaji wa vifaa vya kufanya vipimo na vifaa vya watu kujikinga.

Maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa wakikutana kwa njia ya mtandao ili kutoa taarifa kwa nchi wanachama kuhusu COVID-19
Maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa wakikutana kwa njia ya mtandao ili kutoa taarifa kwa nchi wanachama kuhusu COVID-19
UN Photo/Eskinder Debebe

Guterres pia amesema kwamba“Umoja wa Mataifa una mfumo imara wa kuratibu msaada wa mnyororo wa thamani kwa nchi na kwamba mtandao huu wa kimataifa unapatikana kwa nchi wanachama ili kusafirisha vifaa vya afya, wahudumu wa afya na bidhaa nyingine.”

Operesheni za kijeshi

Katibu Mkuu amesema Umoja wa Mataifa pia unashirikiana nan chi ili kudhibiti mzunguko wa wanjeshi wa kulinda amani na polisi. Baadhi ya mizunguko imeahirishwa. Akizungumzia juhudi pana Zaidi Katibu Mkuu amekumbusha ombi la usitishaji uhasama kimataifa alilolizindua Jumatatuna ombia la dola bilioni 2 kwa ajili ya masuala ya kibinadamu lilizozinduliwa Jumatano.

Guterres amezitaka nchi zote wanachama “kusaidia na kuunga mkono maombi hayo kwa njia yyoyote ile wawezayo.”

Katibu Mkuu ametetea hatua katika kushughulikia maeneo matatu muhimu: kukomesha maambukizi ya COVID-19 haraka iwezekanavyo, kupunguza athari za kiuchumi na kjamii na mwisho kujiandaa na kujikwamua na kuunda uchumi ambao ni endelevu ukiongozwa na ajenda ya 2030 kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Katibu Mkuu pia ametangaza kuundwa kwa mkakati wa mawasiliano kwa ajili ya mshikamano wa COVID-19 kwa ajili ya kuuhabarisha umma haraka na kuchagiza vitendo vya kibinadamu.Amesema mbali ya janga hili ni muhimu kupambana na wimbi linaloibuka la taarifa zisizosahihi.