51Թ

Ushirikiano wa kimataifa wazinduliwa kufanya chanjo na tiba ya COVID-19 kupatikana kwa wote

Get monthly
e-newsletter

Ushirikiano wa kimataifa wazinduliwa kufanya chanjo na tiba ya COVID-19 kupatikana kwa wote

UN News
27 April 2020
By: 
Shirika la afya kwa nchi za Amerika PAHO linatoa mafunzo ya upimaji wa virusi vya COVID-19 kwa wataalam wa maabara nchini Guyana
UN Guyana
Shirika la afya kwa nchi za Amerika PAHO linatoa mafunzo ya upimaji wa virusi vya COVID-19 kwa wataalam wa maabara nchini Guyana

Mkakati mpya wa kimataifa umezinduliwa leo ili kusongesha mbele juhudi za maendeleo, uzalishaji na fursa sawa ya nyenzo mpya za kukabiliana na janga la virusi vya corona auCOVID-19hasa katika upatikanaji wa chanjo.

Mkakati mpya wa kimataifa umezinduliwa leo ili kusongesha mbele juhudi za maendeleo, uzalishaji na fursa sawa ya nyenzo mpya za kukabiliana na janga la virusi vya corona au COVID-19 hasa katika upatikanaji wa chanjo.

Uzinduzi huo umewaleta Pamoja viongozi wa dunia, sekta binafsi, wadau wa masuala ya kibinadamu na washirika wengine kuchagiza afya, kuhakikisha dunia iko salama na kuendelema mema kwa umma.

Mhudumu wa afya aktioa chanjo ya polio kwa mtoto Kaloko, Ndola, Zambia.
Mhudumu wa afya aktioa chanjo ya polio kwa mtoto Kaloko, Ndola, Zambia.
UNICEF/Karin Schermbrucke

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika kwa njia ya mtandao na ambao umeandaliwa na shirika la afya la Umoja wa Mataifa, Rais wa Ufaransa, tume ya Muungano wa Ulaya, wakfu wa Bill na Melinda Gates na kuhusisha washiriki wengine mbalimbali, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema “Afya ya binadamu ni faida bora ya kimataifa kwa umma , na leo ytunakabiliwa na adui mkubwa wa umma ambaye hajawahi kushuhudiwa , katika dunia hii iliyounganika hakuna yeyote aliye salama hadi pale sote tutakapokuwa salama.COVID-19 haiheshimu mipaka, COVID-19 popote ni tishio kwa watu kila mhali. Dunia inahitaji maendeleo, uzalishaji na utoaji wa usawa wa chanjo salama na inayofaa ya COVID-19, matibabu na uchunguzi.”

Katibu Mkuu amesisitiza kwamba na“Si chanjo au matibabu kwa nchi moja au ukanda mmoja au nusu ya dunia lakini chanjo na matibabu ambayo ni ya gharama nafuu, salama, yanayofanyakazi, rahisi kuyafanya na yanayopatikana duniani kote kwa kila mtu kila mahali.”

Ameongeza kuwa dunia huru bila COVID-19 inahitaji juhudi kubwa za afya za umma kuwahi kutokea katika historia.

Bwana Guterres amehimiza kuwa“Lazima kushirikiana takwimu, uwezo wa uzalishaji lazima uandaliwe , rasilimali lazima zikusanywe, jamii lazima zishirikishwe na siasa lazima ziwekwe kando. Najua tunaweza kufanya hili, najua tunaweza kuwapa watu kipaumbele cha kwanza na nyenzo hizo mpya lazima ziwe mfano muhimu na wa wazi jambo jema kwa umma.”

Nesi akijaza chanjo katika bomba la sindano
Nesi akijaza chanjo katika bomba la sindano
UNICEF/UN066747/Rich

Katibu Mkuu amesema kwa muda mrefu sana hatujathamini au kuwekeza katika bidhaa za umma kama mazingira safi, usalama mtandaoni, amani na orodha inaendelea.

“Hivyo hebu na tuache hili liwe somo moja muhimu la janga hili la COVID-19, haja ya uharaka wa dharura mpya ya kuunga mkono bidhaa za umma na huduma za afya kwa wote. Tuko katika vita vya maisha yetu, na tuko katika janga hili Pamoja na tutajikwamua katika janga hili tukiwa na nguvu kwa pampja.”

Katibu Mkuu amewashukuru wote walioshiriki mkutano huo na kuonyesha mshikamano wa kimataifa dhidi ya janga la COVID-19 ambalo linaitikisa dunia hivi sasa.